Sasa ni wakati wakufanya kongamano la kitaifa kutafuta dawa ya wahuwaji washenzi /vibaka kwa wananchi

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
5,979
6,784
Ndugu zangu wana jf kwanza heli ya sikukuu popote mlipo na niwatakie kheli pia ya mwaka mpya 2024 popote mlipo na kwa kipee wanaccm na mwenyekiti wenu maana siasa sio ugonvi, ila ikumbukwe mwaka tunao maliza mmeliumiza sana Taifa la Bwana.

Wakuu rejea kichwa tajwa hapo juu, mwaka 2023 unaenda kuisha kukiwa na watanzania wenzetu ambao wanauwawa kinyama kwa kupigwa Marisasi , wengine kupotea bila kujua wahusika ni wakina nani na hii hata juzi imetokea hapo jijini Dar es Salaam kwa mjibu wa vyombo vya Habari.

Kwa maumivu makubwa naomba kuja kwenu na pendekezo kwenu, Watanzania wenzangu la kufanya kongamano mahalum la kujadili ni namna gani ya kuweza kujihami kama wananchi kuondokana na maumivu ya kikatili kwa ndugu zetu watanzania bila kusahau kuacha familia zao wajane na bila msaada wowote kisa haya majangili machache ambao wameamua kufanya kujimilikisha haki za kupora uhai wa binadamu wenzao.

Napendekekeza liwepo kongamano na kua na kauli moja kwamba yoyote anaekuja kukamata mtu bila uniform , basi atambulike kama kibaka na kwa vyovyote vile zana za jadi zitumike kujihami na kuwashughulikia kikamilifu namanisha

Iwe panga, jembe , mshale n.k ili hali ametambulika ni kibaka tu kwa kutokua au kutokufuata sheria kukamata mtuhumiwa ,bila kusahahu kutofaa uniform na kuwa na vitambulisho vinavyo mtambulisha mkamataji ,

Inatosha sasa kuzika vifo vya ndugu na jamaa visivyokua na kichwa wala Miguu

Mwisho niwatakie mwaka mpya mwema.
 
Pole sana kwako mleta mada pamoja na wadau wote ambao wamekumbwa na madhila kama hayo.Inauma sana.
 
Umesema vyema mimi ni muhanga wa vifo vya ajabu binti yangu mpemdwa na wapekee kidato cha tano PCB alifia mikononi mwa Mkuu wa Wilaya ya LINDI mpaka sasa nimefungua shauri sijui kinachoendelea nawataka wajue tu its not over untili its over ntakufa mimi au wao.
Uzuri nina taarifa sahihi wataeleza

Kwa nini walimuua mwanangu?nikishindwa Duniani ntapambana nao kinvingine nawasihi tu wajiandae kwa yote
 
Umesema vyema mimi ni muhanga wa vifo vya ajabu binti yangu mpemdwa na wapekee kidato cha tano PCB alifia mikononi mwa Mkuu wa Wilaya ya LINDI mpaka sasa nimefungua shauri sijui kinachoendelea nawataka wajue tu its not over untili its over ntakufa mimi au wao.
Uzuri nina taarifa sahihi wataeleza

Kwa nini walimuua mwanangu?nikishindwa Duniani ntapambana nao kinvingine nawasihi tu wajiandae kwa yote
Pole sana mkuu, na familia kwa ujumla
 
Back
Top Bottom