Maadili ya Kitaifa

Asalaam Alaikum Wapenzi Watanzania Wazalendo;

Baada ya Malumbano ya muda mrefu ya Ufisadi/Mafisadi, Walarushwa/Rushwa, Watuhumiwa/Wahukumiwa, Mapambano ya Mtu na Mtu, Ukereketwa,Ufurukutwa,Ungangari,Ungunguri, haki sawa kwa wote, Mpaka Kieleweke, na Kila kitu ambacho kinaonyesha mmoja anajua zaidi au anamachungu na nchi yake zaidi ya Mwingine sasa ni wakati muafaka at least kwenye thread hii kuacha mapambano hayo... Kuacha personality issues,

  • sasa tujadili ni maadili gani ya kitaifa ambayo kiongozi yeyote, wa siasa, wa serikali, wa shirika la umma au wa umma kwa ujumla anatakiwa awe!
  • Ni mambo gani ni lazima yafuatwe na viongozi wote bila kujali vyama vyao?
  • Ni Mambo gani ya mwiko na kwa viongozi, kwa maana akifanya kosa na kuthibitika atengwe na jamii au kupewa adhabu kali?

Ninayo ya kwangu ninayoamini lakini nareserve ili kuacha uwanja mpana!

RULES:
Kwenye thread hii sitazamii malumbano ya mtu na mtu! Sitazamii matusi, sitazamii, wewe hujui, mimi najua!!! Kila maoni yana maana, huwezi jua maoni yenu yawaza kuwa ya maana kama Mh. Rais atatekeleza ahadi yake kuhusu kipengele hiki...


Karibuni
Je tunqyo maadili ya kitaifa leo?
 
Back
Top Bottom