Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani: Una ufahamu wowote juu ya ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Siku ya Ini Duniani huadhimishwa tarehe 28 Julai ya kila mwaka, leko kuu ikiwa ni kuelimisha na kuikumbusha jamii katika athari za ugonjwa huu, jinsi unavyoambukizwa na namna ya kujikinga.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani kupitia taarifa ya Homa ya Ini yam waka 2021 zinaonesha kuwa, mwaka 2019, watu milioni 296 duniani, walikuwa wanaishi na homa sugu ya Ini aina ya B ambapo Zaidi ya nusu (66%) ya maambukizi hayo yalikuwa yanatoka katika Bara la Afrika.

Je, una ufahamu wowote juu ya ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga?

photo_2023-07-28_01-45-37.jpg
photo_2023-07-28_01-45-49.jpg
photo_2023-07-28_01-45-58.jpg
 
Hatari,

Kwa mujibu wa taarifa kutoka WHO, takribani Watanzania milioni 1 wanafariki kwa Ugonjwa wa Homa ya Ini Nchini Tanzania huku wengine zaidi ya milioni 3 wakiambulizwa kila mwaka.

Kama hali ni mbaya hivi kwa nini Wizara ya Afya haifanyi Kampeni yeyote ya awareness kwa wananchi ili kuchukua tahadhari na kupata chanjo? Tunasubiria wafe wangapi?

Mwanzo TV Plus
 
Chanjo ya homa ya ini hutolewa mara tatu, ni baada ya kupimwa na ukakutwa huna. Vituo vingi vya binafsi vya kawaida gharama ni 15,000 kila ukichanja. Jumla shilingi 45,000. Nadhani chanjo ya pili inafuata mwezi baada ya ile ya kwanza, ya tatu sijui.
Kama uko positive hamna dawa wala tiba
 
Siku ya Ini Duniani huadhimishwa tarehe 28 Julai ya kila mwaka, leko kuu ikiwa ni kuelimisha na kuikumbusha jamii katika athari za ugonjwa huu, jinsi unavyoambukizwa na namna ya kujikinga.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani kupitia taarifa ya Homa ya Ini yam waka 2021 zinaonesha kuwa, mwaka 2019, watu milioni 296 duniani, walikuwa wanaishi na homa sugu ya Ini aina ya B ambapo Zaidi ya nusu (66%) ya maambukizi hayo yalikuwa yanatoka katika Bara la Afrika.

Je, una ufahamu wowote juu ya ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga?

View attachment 2701237View attachment 2701238View attachment 2701239
Tiba ninayo mimi ya kuweza kumtibu mgonjwa wa Homa ya ini aka Hepatitis B Virus kama kuna mtu anataka tiba yake anitafute kwa wakati wake ili niweze kumtibia maradhi yake.
 
Kwa sasa bongo wanaohamasika kuchanja ni either watumishi wa afya au waliowahi kuuguza mwenye hili tatizo.

Na wanaojitambua wachache.
 
Back
Top Bottom