WHO: Homa ya ini ni hatari kuliko UKIMWI na Kifua Kikuu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,812
Shirika la Afya Duniani WHO Wametoa taarifa walisema ugonjwa wa homa ya Ini ni Hatari sana Kwa Mwandadamu kuliko Virusi vya Ukimwi HIV na Ugonjwa wa Kifua Kikuu..

Tuchukue tahadhari ikiwemo chanjo ya homa ya Ini

===

Mashirika ya afya likiwemo la Afya Duniani (WHO), yanaonya kuwa homa ya ini inaweza kua watu wengi zaidi ifikapo mwaka wa 2040 kuliko HIV, kifua kikuu, na malaria kwa pamoja ikiwa ugonjwa huo utaendelea kupuuzwa na kutofadhiliwa vya kutosha.

WHO, inasema homa ya ini, inaathiri zaidi ya watu milioni 350 ulimwenguni na kua zaidi ya watu milioni 1. Asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa na kuawa na ugonjwa huo ni kutoka nchi zene pato la chini na la kati.

Aidha, licha ya tiba ya homa ya ini aina ya C na chanjo dhidi ya homa ya ini aina ya B, watetezi wa ulimwengu bado hawajafikia lengo lao ambapo gharama ya jumla ya kuponya mgonjwa ilishuka kwa asilimia 96 kutoka zaidi ya dola 2,500 kwa kila mtu hadi chini ya dola 80 kwa kila mtu aliyeponywa.

Chanzo: Dar24
 
Back
Top Bottom