M4C imekosewa mahesabu haitafanikiwa

JF-MBUNGE

JF-Expert Member
May 1, 2012
421
160
Nadiriki kusema M4C na gwanda operation ya chadema ni starategy nzuri lakini wamekosea mahesabu...

Hii ilitakiwa kuanza si chini ya mwaka mmoja na nusu au mmoja kabla ya 2015. CCM kama wanaweza kutumia udhaifu huu basi ndio itakua mwisho wa CDM...lkn kama wataendelea na propoganda na kuuza zura kwenye media bila kupambana basi ndio hali si swali tena.

Source=Nilivyoona jangwani leo.
 
..wanachotakiwa kufanya CCM ni kutekeleza ahadi zote walizotoa ktk uchaguzi.

..pia washughulike na matatizo kama kupanda kwa gharama za maisha, mfumo mbovu wa elimu, matatizo ya umeme, matatizo ya maji, huduma za afya, kumaliza kabisa tatizo la ufisadi, etc etc.

..CCM wanatakiwa kufanya kazi waliyotumwa na wapiga kura, badala ya kuhangaika kuwashambulia Chadema.
 
Kuna mtu aliyekuwa anakusanya watu wengi kwenye mikutano zaidi ya Mrema?

Muulizeni alikosea wapi?
 
Suala la muda, siyo issue hapa; CDM wameanza mapema operations zao, thats good, wanahitaji muda mwingi ili ku sweep, nyumba kwa nyumba, kijiji kwa kijiji n.k. ili sera za CDM zifike kwa watu wote. Tatizo liko wapi?
 
Kuna mtu aliyekuwa anakusanya watu wengi kwenye mikutano zaidi ya Mrema?

Muulizeni alikosea wapi?

Alichokozea Mrema, kwanza alikuwa very weak academically. So far CCM wakatumia vyema udhaifu wake huo kumkolimba kisiasa. Na ndiyo maana mpaka leo anarufu ya CCM.
 
Hii inaendelea wala co nguvu ya soda, nawashukuru viongozi wa cdm kwa kuanza mapema. Hadi tutoboe 2015 SISIMWEWE watakuwa wamesahauliwa!!!!
 
Kuna mtu aliyekuwa anakusanya watu wengi kwenye mikutano zaidi ya Mrema?

Muulizeni alikosea wapi?
Hakuna mwenye akili timamu anaeweza kufananisha movement za aliyekuwa mwenye kiti wa nccr A. Mrema na Chadema. Mrema alikuwa anafuatwa na washabiki wake kama person Mrema, na hilo ndilo lililokuwa kosa kubwa sana. Chadema pale hafuatwi mtu ila chama ambacho kimekaa kitaasisi na chenye mtandao unaoenea nchi nzima.

Hivyo chama hiki anaweza kuondoka yeyote na kikabaki bado ni imara. Kwa Lyatonga tofauti iliyokuwepo ni kwamba ukimwondoa yeye chama kimekufa. Na huo ndio ulikuwa msiba wa chama alichojiunga Mrema.
 
Suala la muda, siyo issue hapa; CDM wameanza mapema operations zao, thats good, wanahitaji muda mwingi ili ku sweep, nyumba kwa nyumba, kijiji kwa kijiji n.k. ili sera za CDM zifike kwa watu wote. Tatizo liko wapi?
Nasema M4C ni strategy nzuri ila ki ukweli operation wameiwahisha sn hilo ni kosa la kiufundi, ebu fikiri ingefanywa 2013 juni hv..!

Kipindi hicho magamba wengi watakua hawana wanalotegemea kiutawala bali wanaangalia mbele maisha yao. Hivyo kwa presha ya M4C wengi wangeweza kumwaga ugali na kuvaa gwanda kujiandaa na 2015 after. Hali hiyo ingewachanganya magamba wakashindwa kujipanga ndio ulikua ushindi wa magwanda....too late magamba lzm wajipange.
 
Jokes aside, kuna haja ya cdm kuboresha approach yao.... leo jangwani kulikua na tatizo kubwa la flow ya message to waliohudhuria
 
Jokes aside, kuna haja ya cdm kuboresha approach yao.... leo jangwani kulikua na tatizo kubwa la flow ya message to waliohudhuria

sasa mkuu ulitaka viongozi waongee nn tena maana mi naona kila kitu mlishaambiwa na sasa mnakumbushwa 2, au mnataka viongozi waseme nn tena? Cha kufanya sio kuona wataongea nn maana wao kazi wameshamaliza kukufumbua macho so ss hivi ni kazi yako imebaki na ww kuibadilosha jamii yako na kuvua gamba kama ulikuwa nalo na kuvaa gwanda ww pamoja na jamii yako. Full stop !
 
Ni mitizamo ila siyo kweli kwamba ishu ya muda haieleweki bali ungependa ujue ni kwanini leo na si 2013,na je huko mbele kuna ipi ya kuingilia 2015

Hivi ni vipigo mfululizo mkuu mpaka mwisho.
 
Ndio madhara ya demokrasia ya uhuru wa mawazo! Sasa mbona hukusema mapema tangu pale Arusha ilipozinduliwa alafu unakuja kusema leo!
 
Kuna mtu aliyekuwa anakusanya watu wengi kwenye mikutano zaidi ya Mrema?

Muulizeni alikosea wapi?
Labda ungesema na Mtikila basi. Wakati huo wa Mrema haikuwa kama sasa, watu walikuwa wanashabikia kumpenda Mrema, lakini leo watu wanazungumzia mabadiliko.
 
Ni mitizamo ila siyo kweli kwamba ishu ya muda haieleweki bali ungependa ujue ni kwanini leo na si 2013,na je huko mbele kuna ipi ya kuingilia 2015

Hivi ni vipigo mfululizo mkuu mpaka mwisho.

Ebu niambie kwann leo?mie nimekwambia impact amabayo ingekuwepo M4C ingeanza 2013...!we niambie logic na impact yake kwa kuanza shv.
 
Kuna mtu aliyekuwa anakusanya watu wengi kwenye mikutano zaidi ya Mrema?

Muulizeni alikosea wapi?

Ribosome,

..tatizo la Mrema lilikuwa ni uchanga wa chama chake NCCR.

..pia alikuwa na washabiki wengi waliokuwa wanaiunga mkono NCCR kwasababu yake yeye Mrema.

..sasa hivi ndani ya CDM kuna watu wa kila aina, kuna wanaofuata viongozi kama Zitto na Slaa, kuna wakereketwa wa katiba mpya, kuna wanaotaka mabadiliko, etc etc.

..pia walivyoanza mapema inaweza kuwasaidia kupata muda wa kurekebisha makosa yao na kujiimarisha. chaguzi ndogo nazo zinawasaidia CDM kujitangaza hata kama watashindwa ktk baadhi yake.

..lakini kubwa kuliko yote ni REKODI ya miaka 35 ya UTAWALA MBOVU WA CCM.
 
Ebu niambie kwann leo?mie nimekwambia impact amabayo ingekuwepo M4C ingeanza 2013...!we niambie logic na impact yake kwa kuanza shv.

Logic ni kufundisha elimu ya uraiya na kutafuta mtaji mkubwa wa kura z 2015, hatuvizii bali tunajitokeza mapema coz tuna bonafide.
 
Back
Top Bottom