M4C imekosewa mahesabu haitafanikiwa

M4C imekosewa mahesabu haitafanikiwa

Ribosome, wakati ule mikutano ya Mrema ilikuwa mikubwa lakini huewezi linganisha na ya CDM.
Mwisho, ile ilikuwa mikutano ya Mrema binasfsi lakini CDM hawana mikutano ya Slaa au Mbowe bali CDM.

Mwambie Heche aitishe mkutano uone atapata watu wangapi.
 
..wanachotakiwa kufanya CCM ni kutekeleza ahadi zote walizotoa ktk uchaguzi.

..pia washughulike na matatizo kama kupanda kwa gharama za maisha, mfumo mbovu wa elimu, matatizo ya umeme, matatizo ya maji, huduma za afya, kumaliza kabisa tatizo la ufisadi, etc etc.

..CCM wanatakiwa kufanya kazi waliyotumwa na wapiga kura, badala ya kuhangaika kuwashambulia Chadema.

JokaKuu CCM ni sikio la kufa
 
Ebu niambie kwann leo?mie nimekwambia impact amabayo ingekuwepo M4C ingeanza 2013...!we niambie logic na impact yake kwa kuanza shv.

Ni leo kwa sababu hii si ya kwanza wala si ya mwisho pili,lengo la move hii ni kuwaandaa watz popote pale kuwa tayari na mabadiliko makubwa na kupata nafasi ya kula na kudigest kuhusu katiba iweje

Lakini kubwa ni kukisimika chama mapema kabisa nchini kote ili kufika 2013 tuwe na hesabu kamili ya matawi na wanachama na kama itakuwepo kazi yoyote iliyobaki ndogo basi imaliziwe 2014,ili 2015 tuingie Magogoni kila kitu kikiwa clear kabisa

Remember,the early the better!
 
Kaka nimekuelewa....tena sana. Lakini kumbuka kuwa chama hakijengwi siku moja.

Kuna maeneo mengi sana CDM haijafika. Kazi kubwa iko Dodoma, Singida, Tabora, Lindi, Mtwara, Sumbawanga, Iringa, Pwani, Dar, Tanga na Zanzibar. Huko kote watu wanahitaji ukombozi. Hii movement haitakuwa na maana kama CDM tutaacha na kurest. Lakin kwa sababu tumeamua kuchangia chama, tutahakikisha kuwa Operation hizi zinaendelea hadi 2015. Na hapo ndipo utaona faida yake.

Kaka kumbuka huu msemo wa kidhungu.....THE EARLIER THE BETTER.

Unataka tushtuke kumekucha!!!!!????

THE EARLIER THE BETTER....unatafsiri vibaya huu msemo wa kidhungu....una apply ukishafanikiwa sio wkt unatafuta fumbuka. Ebu jaribu kutangaza mgombea urais wa CDM 2015 shv si THE EARLIER THE BETTER. Kaka siasa ni kuviziana ka ngumi za cheka na matumla. Nakwambia sasaa hii M4C ndio ilikua fimbo ya mwisho CCM wangechanganyikiwa na kuachia nchi ..shv haiwezi kuvuma hadi 2015 itapoteza muelekeo unatakiwa kujua tabia za watanzani ....imekosewa sn kutumika mapema I stand na huu msimamo
 
Ni leo kwa sababu hii si ya kwanza wala si ya mwisho pili,lengo la move hii ni kuwaandaa watz popote pale kuwa tayari na mabadiliko makubwa na kupata nafasi ya kula na kudigest kuhusu katiba iweje

Lakini kubwa ni kukisimika chama mapema kabisa nchini kote ili kufika 2013 tuwe na hesabu kamili ya matawi na wanachama na kama itakuwepo kazi yoyote iliyobaki ndogo basi imaliziwe 2014,ili 2015 tuingie Magogoni kila kitu kikiwa clear kabisa

Remember,the early the better!

mwenzako daudi kaja na hoja ka hii nimemjibu M4C ni slaa kubwa sana sio ya kutekeleza hayo mnayoyasema...anaglia post za wenzako usikurupuke
 
Kuna mtu aliyekuwa anakusanya watu wengi kwenye mikutano zaidi ya Mrema?

Muulizeni alikosea wapi?

Alichokosea ni pale alipoamua kutumika na magamba na hivyo kuwa pandikizi la magamba katika vyama alivyopitia baada ya kuamua kulivua gamba, hilo ndilo lililokuwa kosa kubwa sana la Mrema.
 
Nadiriki kusema M4C na gwanda operation ya chadema ni starategy nzuri lakini wamekosea mahesabu... Hii ilitakiwa kuanza si chini ya mwaka mmoja na nusu au mmoja kabla ya 2015. .
Mkuu una wazo zuri sana lakini kuna kitu hujakiona. Mwaka 2010 CHADEMA walifanya makosa mawili. 1. walichelewa kuanza sensitization Campaign, 2. walichelewa mchakato wa kumpata mgombea wa Urais. Hizo ni moja ya sababu zilizosababisha CHADEMA kupungukiwa kura.Hii M4C imeanza wakati mufaka kabisa, kwani CHADEMA inahitaji watu wakati wa uchaguzi watakao kipigia kura. Kupata watu wa kukupigia kura unahitaji watu hao wajiandikishe katika daftari la kudumu la wapiga Kura. CHADEMA inategemea sana vijana kuweza kushinda chaguzi zake, Sasa shida huwa inakuwa vijana wengi huwa hawajiandikishi katika daftari la wapiga kura na unapofika wakati wa kampeni vijana wanahamasika lakini muda unakuwa umisha wa kujiandikisha. CHADEMA kukabiliana na changamoto hiyo inahitaji Operation ambayo itawafanya vijana wawe senitized mapema, na tutakavyokuwa tunaboresha Daftari la wapiga kura basi vijana hao wajiandikishe katika daftari la wapiga kura na wanabaki na kazi moja tu kutuza kadi ya kupigia kura. Na ninadhani katika M4C CHADEMA inahitaji msemaji mmoja atakayeongelea kujiandikisha na kutunza shahada kitu ambacho hakijasemwa leo Jangwani
 
Kwa sababu tunataka mabadiliko basi mabadiliko lazima yawe ya haraka kwa maana tumeachwa sana na nchi za wenzetu. Mwl aliwahi kusema "We have to run while others are walking".

Tumekuwa nyuma sana kimaendeleo kwenye kila sekta, nchi yetu sasa niya 3 kwa kupokea misaada ulimwenguni baada ya Iraq na Afighanistan, tuna dhahabu karibu kila kanda katika nchi yetu, tuna ufukwe mkubwa wa bahari kuliko na ardhi yenye rutuba, tuna mbuga na wanyama hivi vyote vimekosa viongozi wenye utashi wa dhati na mapenzi kwa nchi hii.

Hivyo hatua yoyote ya kuwaamsha wananchi kuelekea mabadiliko ya kweli lazima iwe ya haraka naya mapema lazima tukimbie wakati magamba wanatembea ili siku wakiamka watukute tumepumzika kituo cha magogoni.
 
Freedom is coming tomorrow. . . . Get ready for your freedom . . . .
 
Lakini piwa sisi watanzania huwa tunayumbishwa na tu-issues tusitokuwa twa maana. Kwa mfano nakumbuka katika chaguzi kadhaa huko nyuma viongozi wa CCM walisimama majukwaani na kuwaambia watu wasichague vyama vya msimu, sasa toka baada ya uchaguzi mwaka 2010 CHADEMA imeonyesha kuwa sio chama cha msimu na CCM ndio chama cha msimu maana wamaetulia kama maji kwenye mtungi. CCM sasa hivi sio wabunifu tena, angalia walivokuwa wanakataa siasa mashuleni, walipoona CHADEMA inaibua makada vijana wengi kimeamua kubadili msimamo wake, angalia suala la usajili wa wanachama online, angalia ajenda za katiba, makazi bora etc. Utagundua kuwa CHADEMA ndio wanaobuni na CCM ndio wanaofuata.
 
Hivi wewe ndio umeandika nini hapa sasa? Kwanini mnapenda kupotezea muda watu? Mimi nimefungua huu uzi nikadhani ni very constructive kumbe ni hoja makamasi. Jaribu kuwa na fikra makini kabla ya kupost hapa JF.
 
Chama kinajengwa hivi. Hakuna kukosea mahesabu hapa wala nini. Hili ni nchi kubwa huliwezi kulimaliza kwa mwaka mmoja au miwili. CDM wamejua pakuanzia. Hata hivyo, hii siyo kazi ya kwanza ya CDM, labda hilo jina la M4C. Kumbuka Mbowe kabla hajawa mwenyekiti alizunguka nchi mzima kujenga chama.

AU umesahau zile operesheni za Chadema zilizokuwa zinafanywa na wabunge wake? Walikuwa wa4 tu na wakati huo chama kilikuwa kinapata ruzuku ya Sh. 3.2 milioni.

Tunataka kila penye Balozi wa Shina AKA, mwizi wa kura wa CCM - kuweka balozi wa shina wa CDM - mlinzi wa kura na amani. Hiyo ndiyo pekee ya kuondoa hawa MAGABA.
 
Magamba hayana uwezo wa kujipanga tena kwani watu wameshawagundua uongo na ufisadi wao!! Wamewachoka na hawadanganyiki tena....
 
Elimu ya uraia ingeweza kutolewa kwa approach nyingine sio hii ya M4C..kwa kufanya hivyo utakua unatumia silaha kubwa kwa swala mdogo.../
Nadhani hujaelewa vizuri kama kuna kazi kubwa kuliko zote kwa wananchi wa Tz ni hii ya elimu ya uraia maana ndiyo inayoweza kubadilisha mind set. Once that is accomplished the rest is easy!!
 
Kuna mtu aliyekuwa anakusanya watu wengi kwenye mikutano zaidi ya Mrema?

Muulizeni alikosea wapi?

Huyu ni shushu alitumwa na CCM mahusisi kwenda kuvuruga upinzani na alifanikiwa na kisha akachoka na sasa karudi CCM.
 
Hakuna mwenye akili timamu anaeweza kufananisha movement za aliyekuwa mwenye kiti wa nccr A. Mrema na Chadema. Mrema alikuwa anafuatwa na washabiki wake kama person Mrema, na hilo ndilo lililokuwa kosa kubwa sana. Chadema pale hafuatwi mtu ila chama ambacho kimekaa kitaasisi na chenye mtandao unaoenea nchi nzima.

Hivyo chama hiki anaweza kuondoka yeyote na kikabaki bado ni imara. Kwa Lyatonga tofauti iliyokuwepo ni kwamba ukimwondoa yeye chama kimekufa. Na huo ndio ulikuwa msiba wa chama alichojiunga Mrema.


like x 1000000
 
Nasema M4C ni strategy nzuri ila ki ukweli operation wameiwahisha sn hilo ni kosa la kiufundi, ebu fikiri ingefanywa 2013 juni hv..! Kipindi hicho magamba wengi watakua hawana wanalotegemea kiutawala bali wanaangalia mbele maisha yao. Hivyo kwa presha ya M4C wengi wangeweza kumwaga ugali na kuvaa gwanda kujiandaa na 2015 after. Hali hiyo ingewachanganya magamba wakashindwa kujipanga ndio ulikua ushindi wa magwanda....too late magamba lzm wajipange.
Ni wasiwasi wako tu lakini unatakiwa kujua kuwa watanzania wanatakiwa kuondolewa U-CCM kwenye akili zao mapema kabla hawajaingia kwenye mchakato wa katiba mpya ambao unaanza soon. Wasipofanya hivyo kuna hatari kubwa ya watanzania kupitisha katiba ya CCM kwa mara nyingine. Katiba mpya inatakiwa iwe na mtazamo wa kimabadiliko; nafikiri hata mkutano wa Jangwani umesisitiza hilo kwa upana sana. Usiogope, CCM hawana jipya zaidi ya kuiga CDM; tunazo mbinu nyingi ambazo bado magamba hawajui; wakiiga tunawaachia tunaanzisha nyingine mpya.
 
Mwambie Heche aitishe mkutano uone atapata watu wangapi.
Mwambie Heche aitishe nini; M4C same kwa Ana Kilango (mnafiki) ni utumbo wako uliitisha mikutano?? mbona nyomi ilikuwepo kama kawa? Au ulikuwa umelala??
 
1) Hii nchi ni kubwa kijiografia.
2) Pia tatizo la usugu wa umaskini na ujinga vilihitaji immediate attendance.
3) Kuonesha tofuati kati ya opportunism and strategism ilibidi ianze sasa.
4) Baada ya kupita kila kijiji na kona za nchi hii (kufungua njia), then hiyo sehemu ya pili unayotamani itakuwa ni mahali sahihi
5) Usiwe na -ve view, baada ya kupractice wataalam watakaa na kuchambua/kupima kisha kuboresha. Kama hujafanya utajuaje udhaifu?
 
Back
Top Bottom