M-Pesa sio salama

Suppose namba zangu ni 075423678 na niliyokosea inasoma 0754233978 . sometime ni ngumu kuona hiyo namba hapo katikati haswa ukizingatia mazingira niliyotumia hela yalikuwa kwenye gari linalotembea.
Sasa hapo makosa ni ya nani??
 
Kwa nini Mng'ang'ane kwenye maumivu ..piga chini huo mtandao.

Angalau Tigo wao wana njia mbadala ya kurudisha muamala wako ..

Kosa ulilofanya ni kuukubali muamala wakati ukijua kabisa unaweza 1 kubali au 2 kukataa.

Kuw makini Bro nyie ndiyo mnazingua ata wakati wa uchaguzi mnaharibu kura zenu.
 
Tatizo la Mitandao yetu ya simu inatumia cheap labour na na watu ambao wamezoea kufanya kazi kimazoea na very short foresight kiasi kwamba kufikiri beyond the horizon ya meza zao ni ngumu sana
Tatizo jingine, baadhi ya wateja wa M Pesa wamezoea kutuma pesa kimazoea bila kuzingatia maelekezo. A slightly mistake inasababisha muamala usomeke kwa mtu mwingine!
 
Aliwahi kuchangia member mmoja humu kuwa alikosea kutuma pesa TIGO, ila akawa tigo wanamzungucha, hivyo akaamua kwendaTCRA, majibu aliyopewa tcra kuwa ni mzembe maana kabla kuweka namba ya siri inakuja Jina, ikabidi awe mpole harudi Tena tigo kufuatilia sijui halifanikiwa
 
huo ni uzembe wa vodacom pia. sasa nini maana ya kusajili namba za watumiaji wa mtandao? kama wao wanaona shida wangekupa taarifa zake alizojisajili nazo umsake vizuri mwenyewe.
Ambacho hamjakitambua ni kuwa kwenye kanuni na taratibu hawaruhusiwi kutoa taarifa za mteja unless wanazihitaji watu wa upelelezi au vyombo vya usalama kama polisi na ndomana akashauriwa aende (akashtaki) kutoa taarifa polisi

Kingine ni kwamba huyo mhudumu yeye ametimiza majukumu yake ya kazi kwa kiwango anachostahili kuishia hayo ya kutaki wateja ni mengine tena ni kinyume na majukumu yake


Tatu, je alishajaribu kuchukua hatua walau moja katika zile alizoshauriwa zikagonga mwamba? Kama hapana hakuna haja ya kuwapakazia vodacom kusema mpesa sio salama mana ikitokea umesaidiwa kivyovyote vile ukarudishiwa hela yako au kwa namna yoyote ile itakubidi uombe radhi au upigwe faini kwa shambulio la uzushi/kupakaza. Mana hicho ukitakacho yawezekekana pengine hawafanyi mpaka kutolewe kibali na baadhi ya mamlaka (kutraki simu sio kirahisirahisi hivyo- it's illegal)

Nne, huyo jamaa anavyomuanika huyo mwenzake hivyo (ambapo yeye anamuita mwizi) je haoni kuwa inawezekana ikamrudi yeye mwenyewe akawa hatiani kwa kufanya shambulio la aibu uzushi au kumvunjia mtu heshima

Mwisho niseme tu kwamba voda ni mtandao makini na unategemewa sana na vyombo vya usalama wa mitandaoni kwahiyo jambo lako dogo tu hilo haliwezi kuwa the big deal
Vinginevyo fuata taratibu halali
 
Daah pole sana mkuu ila hapa nadhan umewashushia faida kwa asilimia 20 maana wateja watapungua.
 
Kama hizi ndizo comments za watanzania walio wengi basi niamini tu nchi inakokwenda ni gizani kuliko tuliko toka.
Washa taa ili uwaangazie watanzania. Kosa ni lako kutokuwa makini kwenye miamala.
 
Sheria za nchi zinasemaje juu ya hilo?
 
Pole sana mkuu. Nakushauri usambaze ujumbe facebook na namba yake ikiwa na caption. Huko watu wanajuana zaidi kuliko hapa JF na nakuhakikishia atajutia sana. Nimewahi kuona kesi nyingi za namna hiyo na hiyo njia ilitatua kwa ufanisi. Voda hawatakupa msaada zaidi ya kuweka deni kwenye namba yake au labda endapo utafungua jalada police na police ndio waamuru voda watoe taarifa za huyo mteja wao aliyechukua hiyo pesa
 
Hv sasa Vodacom na Airtel wanayo hiyo huduma ya kurudisha pesa iliyo tumwa au ulio tumiwa kimakosa.
 
Ndio maana tunatamiwa kushirikisha akili kila hatua tunayofikia ktk kufanya maamuzi
 
Haya ndio tunaita matumizi mabaya ya akili,


Lakini usijali , swala lako linafanyiwa kazi,
 
Tunatumia pia Paypal kuagiza vitu nje kwa mtu usiyemfahamu kabisa na kama akichukua fedha zako bila kutuma item anafuatiliwa popote alipo duniani na atakamatwa
Kama una ujuzi wa PayPal, wape wenzako faida km vp. Inapatkn wapi na jinsi ya kuipata
 
makosa ni ya mtumaji maana kuna kuhakiki no ya unayemtumia mpaka jina sasa kama hukuweza kuona basi .Huwezi kutuma hela then unasema umekosea no kivipi? Tuache lawama ambazo hazina miguu wala kichwa.Hawa Mobile money wameweka kabisa kabla ya kutuma wanaonyesha jina la unayemtumia na no kama zipo sahihi ina maana hukuziona????
Mimi nilifikiri labda kuna shida nyingine kama kuibiwa hela yako iliyoko kwenye akaunti kumbe ni usembe
Pole sana lakini huo ni ujinga na ulipaswa kuwa serious linapokuwa jambo la muamala wa hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…