M-Pesa sio salama

M-Pesa sio salama

Mm nina miak 10 natumia mpesa sijawah kukosea kutuma pesa, najiuliza how mnakiseaga
 
Nimetuma hela kwa mtu anaitwa Samweli Deus kimakosa na in ten minutes nikawapigia MPesa kwa dial 100 na niliongea na dada aliyeko kitengo cha lugha ya Kiingereza na akaniambia nimpe receipt number ya hiyo transaction. Amekuwa fasta kucheki na kuniambia niliyemtumia hela ameshazichukua kwa wakala na THEY CAN DO NOTHING na itanibidi mimi nimpigie mwizi wa hela zangu na akikataa niripoti polisi. Hii ilikuwa accident na sijawahi kosea tangu nianze kutumia hii huduma. Nimesikitika kuwa MPESa haina mechanism ya security kuhakikisha watumiaji wa huduma hawaibiwi. Kwao wanahesabu wamefanya business bila kujali mteja kaibiwa;. Nimejiuliza maswali yafuatayo:
1. VODA hawana uwezo wa kumtrack mteja wao aliyewaibia wateja wengine?
2. Namba ya aliyechukua hela zangu ni 0759548521 inakuwaje Vodacom wanashindwa kunisaidia kupata hela zangu na badala yake kuniambie is non of their business.
3. TCRA inawabanaje hawa wenye kutoa hizi huduma kuhakikisha fedha za mteja hazichopolewi hata pale anapokosea namba au ni kilio cha samaki.
4. Im sure voda wanamjua hata wakala aliyetoa hela na ni rahisi kwa wao kumtumia kumtia mbaroni mwizi ; how come hawataki kujishughulisha na kumwachia aliyeibiwa afanye negotiation na mwizi?

5. Aliyeibiwa yuko Arusha na aliyeiba yuko kanda ya Ziwa na wao wana muscles za kufuatilia nchi nzima ni kwa nini tusione kuwa MPESA siyo salama?

Naomba tusaidiwe hata kama tulikosea ili kupata hela zangu na bado ninaamini wana uwezo wa kufanya hivyo onlu nimekutana tu na VERY WRONG IRRESPONSIBLE AND SHORTSIGHTED STAFF.


Ndugu yangu.....kwanza nitangaze maslahi mimi sio staff wa Vodacom ingawa nilishawahi kufanya nao kazi mwaka 2011 - 2015 (five solid years)

Umekosea kutuma pesa (nasema hili ni kosa la kujitajia kwa sababu mitandao almost yote wameweka ile menu yao ioneshe namba ya simu na jina la unayemtumia ili uhakikishe kabla ya kuthibitisha muamala kwenda); bado unawalaumu mtandao?

Umeuliza Vodacom wanashindwaje kumtrack.......kama mteja ameshatoa pesa, wewe ndo unatakiwa uwe unapiga angalau mara kwa mara ili wao Vodacom wawe wanaingia kwenye account yake kuangalia kama ameweka pesa ndo wairudishe kwako, otherwise hawawezi kublock account ambayo haina pesa maana ndo kwanza utakuwa umem-alert yule mpokeaji asiwe anaweka pesa kabisa kwenye Mpesa yake, so njia bora wanaiacha bila kuiblock ili awe free kutumia account yake miamala iwe inapita ili siku akijisahau na akaweka pesa, na wewe ukipiga ikakutwa mle ndo inareversiwa. (Kumbuka hapa ni ww unatakiwa kuwa unapiga na sio wao customer care uwaachie jukumu la kuwa wanamfuatilia kila siku maana wale wanapokea tu calls na kureport cases kwenye idara zingine......unless otherwise kama unataka ifuatiliwe specifically ya kwako tu basi uende na taarifa ya polisi na ufike kitengo cha Fraud & Forensic Investigation hapo hapo Vodacom ndo waanze procedure za kumtrace huyo mpokeaji

Umesema uko sure kwamba Voda wanamjua wakala ambaye mpokeaji ametoa pesa kwake, why washindwe kumtambua "mwizi wako"......nadhani ww ni mteja wa muda mrefu wa Mpesa na ulishawahi kutoa pesa kwa wakala, hvi ww ukitoa pesa kwa wakala akakupatia fedha zako ukaondoka (ingawa watarecord taarifa za muamala wako), je huyu wakala akibanwa anawezaje kujua ww ni wa wapi na unapatikanaje sasa? assume umetoka Dar kwa bus na unaelekea Dodoma, ukashuka Msamvu pale ukatoa pesa kwa wakala na ukarudi kwenye bus na kuendelea na safari. je huyu wakala wa Msamvu atakujuaje hata kama Voda watambana vipi,.....yeye zaidi ya kuwapa tu namba yako ya simu (ambayo hata ww mtumaji tayari ulikuwa nayo) anawezaje kusaidia sasa kama sio kumlaumu bure?

Mwisho umedeclare kwa maandishi makubwa kabisa kuwa MPESA sio salama!. Je kwa muamala wako mmoja uliokosea (kwa kujitakia) ndio umepata mandate ya kisheria ya kuutangazia umma kwa Mpesa sio salama? Je huoni kwamba hapa unaweza kuwa sued hata mahakamani kwa kutoa maneno yenye kutishia biashara za watu kwa kuandika kwenye forum inayosomwa na umma kuwa biashara ya fulani sio salama?

Najua upo ktk panic hasa kwa kuzingatia huenda muamala uliokosea ni fedha nyingi, ila ukishatulia na kurejelea ulichoandika hapa utaona umekosea big time!

USHAURI WANGU;
Toa taarifa police utaandikiwa RB kisha nenda nayo pale Vodacom makao makuu utaelekezwa kitengo cha Fraud and Forensic Investigation watafanyia kazi case yako. Kama upo mkoa tofauti na Dar basi nenda Vodacom Shop iliyo karibu na ww ukiwa na RB yako, wahuduma wa hapo Vodacom Shop watachukua taarifa yako na kuscan RB yako na kuituma ktk kitengo nilichotaja hapo juu na suala lako litafanyiwa kazi vizuri (hata kumpata mwizi wako physically) manake hiki kitengo kinashirikiana na jeshi la Polisi ktk kufanya ufuatiliaji wa watu kama hao.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom