M-Pesa sio salama

M-Pesa sio salama

Somo. ukituma pesa kimakosa kwanza unegotiate na mhusika isionekane unampa gharama na bugudha yeye wakati aliyekosea ni wewe. Mpe hata proposala ya kubakiza kiasi fulan kwa ajili ya kufudia usumbufu atakaoingia

Ilikuwa bahati yake tu alikukuta mtu mstaarabu, siyo kila mtu atafanya hivyo
 
Siyo salama kwa sababu hakuna mechanism ya kuhakikisha usalama wa hela ya mteja. Huyu mtenja ndiye anayeifanya MPESA iwe MPESA. Na kama hutamjali akaogopa kuitumia huduma lazima mpesa itayumba
Ni makosa yako usilaumu VODA kwa sababu unapotuma hela jina la unayemtumia linaonekana
 
Kunatakiwa angalau kuwepo na mfumo wa kuzuia kutoa pesa mara tu uipokeapo kwa angalau dakika 10, ili kuwezesha mtumaji kama amekosea aweze kuwasiliana huduma kwa wateja na pesa irudishwe
Bado tutasema wanauweka. Hakuna jema kwa bin adam. Umeambiwa hakikisha kabla hujathibitisha. Hapa hukupaona? Waache kazi wakusaidie wewe mzembe?
 
Vodacom wapuuzi sana. Wameshindwa hata kuweka withdraw code ambazo angekuwa anatumiwa anayetuma pesa naye anamtumia aliyemtumia pesa kwa msg ya kawaida.
Upuuzi na ujinga sana
Hapaa umenena mkuu
 
Siyo salama kwa sababu hakuna mechanism ya kuhakikisha usalama wa hela ya mteja. Huyu mtenja ndiye anayeifanya MPESA iwe MPESA. Na kama hutamjali akaogopa kuitumia huduma lazima mpesa itayumba
ahaaaa!
 
Kama utatoa pesa usiyoijua chanzo chake hutakwepa kuitwa mwizi. Na ukijifanya kushtaki utanyea ndoo tu kwani sheria ni msumeno na watoa hukumu mahakamani Hutumia references mbalimbali kabla ya kutoa hukumu.
Siijui chanzo chake kivipi...si imetoka kwa mzembe mmoja huko Buguruni, au chanzo gani unataka? Mwizi ni mtu aliyeiba, aidha mali au mke wa mtu, sasa mimi nimetumiwa pesa, utaniitaje mwizi?
 
Huyo sio mwizi. Ni Kama my aliyeokota kitu kurudisha ni uungwana wake tuu
 
Kwanza pole kwa tatizo hilo. Kwa maoni yangu sioni kama ni busara kuwalaumu Voda pekee wakati wewe ndio chanzo cha tatizo. Hii kesi ni ngumu kuamua Kwa sababu kumekuwa na matapeli ambao mfano anakuja dukan ananunua bidhaa halafu anakwambia anakulipa kwa kukutumia kwenye Simu. Na anakurushia kweli ila akizunguka nyuma anapiga simu kuwa alikosea kutuma hela na ile hela inazuiwa na mwishowe inarudishwa kwa yule tapeli(hii nimewahi kushuhudia Kwa mtu). Kwa hiyo inakuwa ngumu kwa wao kujua nia yako. Na ndio maana njia sahihi hapa kama utakuwa umekosea basi ni vizuri ukaanzia Polisi halafu Voda watoe ushirikiano kwa Polisi ili kumtrace huyo mtu(sababu pia kumfuatilia Mteja bila ridhaa yake na bila kibali cha Polisi pia ni kosa kisheria)
Nimetuma hela kwa mtu anaitwa Samweli Deus kimakosa na in ten minutes nikawapigia MPesa kwa dial 100 na niliongea na dada aliyeko kitengo cha lugha ya Kiingereza na akaniambia nimpe receipt number ya hiyo transaction. Amekuwa fasta kucheki na kuniambia niliyemtumia hela ameshazichukua kwa wakala na THEY CAN DO NOTHING na itanibidi mimi nimpigie mwizi wa hela zangu na akikataa niripoti polisi. Hii ilikuwa accident na sijawahi kosea tangu nianze kutumia hii huduma. Nimesikitika kuwa MPESa haina mechanism ya security kuhakikisha watumiaji wa huduma hawaibiwi. Kwao wanahesabu wamefanya business bila kujali mteja kaibiwa;. Nimejiuliza maswali yafuatayo:
1. VODA hawana uwezo wa kumtrack mteja wao aliyewaibia wateja wengine?
2. Namba ya aliyechukua hela zangu ni 0759548521 inakuwaje Vodacom wanashindwa kunisaidia kupata hela zangu na badala yake kuniambie is non of their business.
3. TCRA inawabanaje hawa wenye kutoa hizi huduma kuhakikisha fedha za mteja hazichopolewi hata pale anapokosea namba au ni kilio cha samaki.
4. Im sure voda wanamjua hata wakala aliyetoa hela na ni rahisi kwa wao kumtumia kumtia mbaroni mwizi ; how come hawataki kujishughulisha na kumwachia aliyeibiwa afanye negotiation na mwizi?

5. Aliyeibiwa yuko Arusha na aliyeiba yuko kanda ya Ziwa na wao wana muscles za kufuatilia nchi nzima ni kwa nini tusione kuwa MPESA siyo salama?

Naomba tusaidiwe hata kama tulikosea ili kupata hela zangu na bado ninaamini wana uwezo wa kufanya hivyo onlu nimekutana tu na VERY WRONG IRRESPONSIBLE AND SHORTSIGHTED STAFF.
 
bado na jina nalo hukuliona wakati unatuma?wakati mwingine uwa nawaza kwamba ebu tuendelee kulizwa hivyohivyo watanzania tuliowengi ni careless
 
Hapana mhusika yuko sawa kuwaomba Vodacom kumfuatilia aliyetoa fedha kimakosa. Hata kama taratibu zinakutaka uhakikishe namba unayemtumia lakini binadamu tunafanya makosa ambayo yako nje ya uwezo wetu. Ni jukumu la Vodacom kumfuatilia. Kuwepo na utaratibu kuwa mtu akituma hela katika muda wa dakika kumi mtu aliyetuma hela anaweza kufanya masahihisho kwa hela alizotuma.
 
Walichoniambia MPESA nimwombe mwizi arudishe hela zangu na ameamua kukaa kimya.
Jina la mwizi ni SAMWELI DEU MWENYE NAMBA 0759548421 na anaolafudhi ya kisukuma yet wanajidai hawawezi kumpata
Pole ndugu. Haya maoni unayopata hapa yanawakilisha mawazo ya Watanzania. Kama unavyoona maoni hapa, Watanzania wengi tuna roho mbaya. Na ndio hao hao tunaofanyakazi Voda na makampuni mengine. Badala ya kusaidiwa utalaumiwa wewe!
 
Nadhani huwa unapata Ujumbe kuwa Hakikisha Namba Kabla ya kutuma Fedha zako, Makosa ni yako hapo sio yao!
Hiyo ta kuhakiki majina haifanyi kazi mara zote kuna transactiin za mpesa huwa hazitoi majina ya mtu unayemtumia , sijui kwa nini voda wameshindwa kulifanyia kazi hili, tigo ndio wako vizuri kwa hilo sijawai kutanya transaction ya tigo pesa isilete jina la mtumiwa pesa
 
Kwa upande fln bahat mbaya lkn km kuna chembe za uzembe maana Kabla hujaruhusu ziende kuna kusoma taarifa as km we unaharaka hyo in sawa na kuishi kwa mazoea km utakavyokufanya mtihan unaacha kusoma instruction ukiamn ni zilezile za chagua jibu lililo sahihi
 
"Hiyo kitu haipo. Hatua ya mwisho ni kuthibisha kwa kubonyeza 1, au kubatilisha kwa kubonyeza 2"
Hatua ya kuhakiki majina ya unakotuma pesa ipo mkuu, shida ni kuwa kwa voda huwa haifanyi kazi wakati wote, hata kwenye app yao ya android , kuna wakati haitoi majina
 
huo uzembe wako mkuu halafu huyo sio mwizi ila nimegundua ni mtu mwenye akili nyingi ila za kijinga na hujitambui yaani lawama zote hizo wakati wewe ujinga wako ndio chanzo
 
Kunatakiwa angalau kuwepo na mfumo wa kuzuia kutoa pesa mara tu uipokeapo kwa angalau dakika 10, ili kuwezesha mtumaji kama amekosea aweze kuwasiliana huduma kwa wateja na pesa irudishwe
Tulihama mabank ATM tukaja M pesa kwa sababu ya uharaka leo unataka turudi tulipotoka sio.? Ushawahi kuwa na emergence ya hela na upo fasta la sivyo kila kitu kinaharibika?
 
Back
Top Bottom