SoC01 M-pesa Kibubu, Tigo Pesa Kibubu n.k: Njia nyepesi ya kuweka akiba kwa wananchi

Stories of Change - 2021 Competition

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
778
Habari ndugu!
Imekuwepo changamoto kubwa kwa watu kupata pesa toshelevu kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za maendeleo. Hii inatokana na ugumu wa maisha unaozikumba familia nyingi hivyo kila kiasi kidogo kinachopatikana kinaishia katika manunuzi ya maitaji ya muhimu kama chakula na kulipa kodi za nyumba.

Kusipokuwepo na mbinu nyepesi za wananchi kujiinulia uchumi wao, zinakuja siku ambazo ni mbaya zaidi kwa sababu hata hao wenye vipato wachache hawataishi kwa amani kutokana na kutegemewa na idadi kubwa ya wategemezi.
Kwa sababu mafanikio ya biashara kubwa zinaitaji mtaji wa kutosha na wananchi wengi ni wazuri katika kuwaza biashara za mafanikio kikwazo kinakuwa namna ya kupata pesa ya kutosha kwa ajili ya kufanikisha biashara hiyo.

Changamoto ya njia (vibubu) hizi za kawaida tulizozizoea kujiwekea akiba ni

1. Mtu kuwa na uhuru wa kuingilia akiba yake muda wowote anapoitaji pesa kwa sababu hakuna kitu kinachomuzuia asichukue, hivyo ngumu sana kutumiza malengo kwa watu wengi kwa staili hii.

2. Rahisi sana kuibiwa akiba yako kama unahifadhi kwa njia za vibubu vya kuchonga.

images (5).jpeg

Picha kutoka mtandaoni

Sasa njia nyepesi ya watu kudunduliza na kujitunzia akiba kwa ajili ya kupata pesa toshelevu kwa ajili ya biashara zao baadae ni;

Mashirika ya mawasiliano kuanzisha vibubu vya mtandaoni ili kuwezesha uwekaji akiba kwa wananchi wengi.
Namna itakavyo fanyika;

1. Serikali kupitia BoT isajiri na kukusanya mitaji ya haya mashirika ya mawasiliano yatakayo wiwa kufanya shughuli hizi za kibenk.

2. Mashirika ya mawasiliano yatakazo anzisha Huduma hii yatapaswa kusajiri wateja wa Huduma hii kupitia mawakala wao wa simu ambao wapo nchi nzima.

3. Kwenye menu ya either tigopesa au mpesa au NMB mobile au Halopesa, wanaongezea kitu kinasomeka hivi: Mpesa kibubu, tigopesa kibubu au NMB Kibubu au Halopesa kibubu.

3. Baada ya mteja kupitia simu yake kuingia kwenye kibubu chake ataweza kuhamisha pesa zake kutoka kwenye account yake mfano ya tigopesa kwenda kwenye kibubu chake ndani ya huo mtandao husika.

4. Akiba ndani ya kibubu itaweza kukaa bila kutolewa kwa kipindi cha miezi 6, au mwaka 1, au na zaidi kulingana na mteja anataka pesa yake aweke kama akiba kwa muda gani.

Faida zitokanazo na Huduma hii endapo itaanza.
1. Serikali hasa Bot itaongeza makusanyo ya pesa hasa kutoka kwenye mashirika ya mawasiliano yatakayo anzisha Huduma hii. Kama their reserve deposit ya kulinda akiba za wateja in case of insolvency.

2. Mashirika ya mawasiliano kuwa na uhakika wa mapato ambayo yemewekwa na wateja kama akiba zao. Hivyo mashirika haya ya simu na benk ni rahisi kuchukua pesa hizo na kuzifanyia uwekezaji mwingine ili kujiongezea mapato zaidi.

3. Malengo ya watu wengi kuanza kufanikiwa kwa sababu baada ya muda furani waliojiwekea wanaweza kuchukua akiba zao walizokuwa wameweka kwenye vibubu vya mtandaoni visivyofikiwa na tamaa yoyote ile kwa sababu vinakuwa vime lokiwa kwa muda fulani.

4. Uchumi wa Tanzania hasa wa wananchi wengi kuanza kukua kwa sababu mtu anaweka akiba akiwa ametageti kufanya jambo kubwa la uwekezaji baada ya kuwa amedunduliza pesa yake kwenye kibubu. Na pia tukumbuke level ya uwekezaji itakuwa kubwa kwenye nchi kama level ya kuweka akiba pia ni kubwa.

Asante kwa kusoma uzi huu.
 
Hv ile NSSF si kibubu kile,sasa mbona inakuwa ngumu sana kuchkua hela kwenye kile kibubu
 
Back
Top Bottom