Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

kila hila inayofanywa na ccm lazima ile kwao na kwa upande wa chadema lazima iwaongezee sifa na wanachama
 
Tufanye maandamano nchi nzima kufurahia ushindi huu,people's power...!!

:behindsofa:
 
kwa hiyo ile video imeamliwa kuwa kweli ni yeye amehusika lakini kosa kama lile ni la jinai siyo kigaidi kwa mujibu wa mahakama sasa hatujui kama atatoka mahabusu.
 
Wapi zemarcopolo, Bungeni Thatha, Sumu, Tuntemeke, Lukosi, Juliana, Mtela, na Lumumba Team?
mwigulu,Nape nao wapo humu jamvini.
jitokezeni hapa.
 
Mh mbona tundu lissu yupo bungeni leo na sasa anapanda ndege kuelekea arusha?
Acha aende Arusha na mheshimiwa spika.
Wametoka mbali.

IMG_3649+jpg.JPG
 
Naam,goma lina-backfire taratiibu!chezea Marando na Lissu wewe!wamelipuliwa kwa madogo wakaona wasisubiri yale makabrasha ya chini ya kabati itakuwa soo!mie nadhani uamuzi huu umetoka Lumumba na ulifikiwa siku ile makamanda walipomrusha hewani mwanamfalme ktk yale mawasiliano ya simu.siasa bhana!
 
Haa nimejua ndio maana jamaa Madelu akaanza kujitangazia mapema ulokole ili ahurumiwe ha ha ha ha ha'
 
hujui kusoma lakini kuandika unajua.

wewe ndio unasoma kama unakimbizwa mleta mada amesema lwakatare kabakiziwa shitaka moja la utekaji ambalo lina dhamana soma vizuri.

Wewe ndio umekurupuka

HAhahahaah! akipata seat kwenye daladala atatuma vizuri ujumbe huu.
Ameedit sana hii habari. Habari original iliyoletwa hapa ilikuwa na sentensi moja tu. Nashukuru kwamba mods wameondoa post yangu maana kwa sasa haina maana tena. Lakini kwa wakati huo ilikuwa ni mhimu sana.
Hili ni pigo lingine kwa CCM. Tunamshukuru Mungu kwa kuwa upande wa wapigania haki.
 
Wapi zemarcopolo, Bungeni Thatha, Sumu, Tuntemeke, Lukosi, Juliana, Mtela, na Lumumba Team?
mwigulu,Nape nao wapo humu jamvini.
jitokezeni hapa.

Maeneo kama haya wote wanaingia kama guests
 
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
Vip dhamana Bado ...?
 
Back
Top Bottom