Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
Mh mbona tundu lissu yupo bungeni leo na sasa anapanda ndege kuelekea arusha?
 
Haya sasa magamba wameshakula za uso mahakamaa kuu. Hakuna cha ugaidi wala ndugu yake na ugaidi, sasa Mwigulu aende akatoe ushahidi mbingu ya shetani kwakuwa anao kama alivyokuwa anapiga propaganda.

Tulishawaambia tangu mwanzo kwamba hii kesi imetengenezwa tu na hakuna substance ya kuifanya iwe kesi ya ugaidi, zaidi ya kuwa makosa ya kanuni ya adhabu lakini hawakutaka kuelewa, haya sasa mahakama kuu imewaumbua.

tata maranya wananchi waelewa wa tanzania sasa wanaona ukweli umewekwa wazi na korti. chezea cdm weye. magamba wanahara mida hii.
 
Huyu Mwigulu asifikiri tumesahau bado tunasubiri ile ishu kua alitishiwa na viongozi wa CDM kuuwawa
 
Mwigulu Nchemba njoo huku nyumba inawaka moto usisahau kututengenezea filamu mpya....
 
Lwakatare alipendwa sana na vijana wa Bukoba mjini na maeneo ya jirani kabla Mh. Kagasheki hajawa mbunge wa hilo jimbo. Haya mateso waliyomptatia safari hii kwa kumdhalilisha na kumtesa kisaikolojia ni dhahiri yalikuwa makubwa sana lakini muda sio mrefu yatalinganishwa na tone la maji baharini pale yatakapo kudhihirisha uonevu huu na huo ni mwanzo tu.
Pole sana Lwakatare (angalau) maana kikombe hiki ni kichungu lakini historia itawakumbuka daima nyie na wengine wajao ambao watakipitia. Mbegu moja ya mahindi haitakaa izae mbegu nyenzake zaidi ya 1000 pale isipopandwa na kuoza ili itoe mche!
 
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare naye akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
Mkuu hebu tukumbushe mashitaka hayo yaliyofutwa badala ya kuongea kiujumla tu kuwa amefutiwa mashitaka yote ya ugaidi
 
Good move, makamanda msonge mbele. Pole Lwaka na familia yako, hongereni CHADEMA kwa msimamo wenu muda wote wa hujuma na usanii wa TISS/CCM.

Ni wazi huu sio muda wa kusherehekea kwani kazi mbele bado ni kubwa! Tusonge mbele.

kwa hiyo yuko nje kwa dhamana au bado yuo rumande.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

Daima Ukweli utashinda Uongo na haki itashinda dhuluma; Mwigulu Nchemba na vikaragosi vyako jifunze kuandika business plan before you embark on a project!
It appears Mwigulu Nchemba has a very very low IQ hawezi kuplot njama inayoweza kufaulu. hamna honours degree pale ni debe shinda!
We can give you free consultancy!
 
Mh mbona tundu lissu yupo bungeni leo na sasa anapanda ndege kuelekea arusha?

Nadhani wakati mwingine huwa wanatoa nondo kwa kutumia makaratasi kwa maana ya kuandika.
Na huyu kumbuka ni Mtaalamu wa Kupangua Hoja. Yani kama kocha ni Guardiola na Barcelona ya 2008/2010
 
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare naye akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

Siku zote kwenye uongo ukweli hujitenga sawa maji na mafuta hayawezi kuchanganyika pamoja.
 
Back
Top Bottom