Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

hii thread haidumu hapa kabla moderator hajaichakachua kwa kuiondoa,kuifungia kama walivyoiondoa/kuifungia ya arusha iliyokuwa imevunja rekodi kwa kuchangiwa mara zaidi 20,000 kwa mda mfupi sana na haijawahi kutokea.RUNGU LA MODERATOR LAJA SI PUNDE.
 
Leo kila mwanacdm anaisifia mahakama eti imetenda haki ila kama maamuzi yangekuwa kinyume na matakwa yenu basi yangemwagika matusi ya ajabu humu.
 
Hii kufutiwa kesi ya ugaidi inaimanisha nini?, Ni kwamba Mawakili wa serikali na DPP hawakujua wanachokifanya? au waliamua kuweka hivyo kwa matakwa yao? Au sheria ililazimishwa kufanya kazi sehemu ambayo sio yake?.

Tukiacha hayo yote, Serikali wanatujengea mawazo gani juu ya ufunguaji wa kesi? huwa zote ziko kihalali au huwa zingine ni kwa ajili ya matakwa ya baadhi ya tabaka?

listi ya watu ambao wangebidi wadondoke pamoja na Lwakatare ilikuwa ndefu sana, haikuwa rahisi lakini iliwabidi wafikie maamuzi hayo.
 
Hongera Lwakatare,dhuluma uliyofanyiwa yote Mungu atakulipa.
 
Leo kila mwanacdm anaisifia mahakama eti imetenda haki ila kama maamuzi yangekuwa kinyume na matakwa yenu basi yangemwagika matusi ya ajabu humu.

pole mkuu,naona wamekuharibia siku kabisa.
 
Mimi pia nitapenda sasa vyombo vya usalama au serikali iweke wazi juu ya undani wa ile video kwa kuwa imeonekana Lwakatare hana hatia lakini wakati huo huo video ipo kwa maana kuna aliyeitengeneza.Sasa mtunzi halisi wa ile movie, director na walioandaa script wakipatikana kwa usahihi ndio sasa tutasema tumekamilisha round moja.

Kumbe na wewe leo unaongea point japo kwa mbali. Hakika ukombozi unakuja
 
naona lumumba team mmekurupushwa huko,haya karibuni tena.
 
Kuna watu humu huwezi kuwaona... Yamewashukaa...
 
Toka lini gaidi akawa winifrid ingekuwa hussein sawa?????
-
Kuna ugonjwa wa akili umeingia, Mtu masaa 24 anawaza UKRISTU/UISLAM alltime.. Ukristu wenu na Uislam wenu Pelekeni huko Kwenye Nchi Zenu.. SISI NI WATANZANIA..

Dini hizi ni propaganda Za kiutawala tu, habu acheni mambo ya Dini-Dini embu njooni wote TUACHENI DHAMBI, TUMWAMINI NA KUMFUATA YESU.. Yesu SIO ukristu wala Uislam Yesu ni YESU TU.. !
 
Ni kwamba Rwakatale amefutiwa makosa yote mawili ya Ugaidi na kubakia na Kosa moja la kupanga njama za kutaka kumteka Msaky ambalo ni la Jinai na lenye Dhamana. Mungu mkubwa Kamanda wetu atarejea tena mtaani kuendeleza harakati.
 
Kuna watu humu ukiandika mazuri ya CHADEMA na ukaandika mabaya ya CCM, wanakuona ni wa kawaida kwa kuwa unaandika wanayoyapenda wao. Lakini siku utakapoandika mabaya ya CDM na kuyasifia mazuri ya CCM, hata kama yana ukweli, watu watakujia juu. Wanadhani ukiwa CHADEMA basi unatakiwa uwe mnafiki na kusifia kila kitu hata kile chenye kutishia mstakabali wa chama.

Ninajua wengi hivi sasa wanapenda mageuzi na wanayatafuta kwa hali na mali, kiasi cha kwamba wapo tayari kuona chadema inaingia madarakani despite mapungufu yake. Lakini mageuzi ya namna hii yatatuumiza. kama hatutaclear baadhi ya weakness zetu, basi tunaweza kuingia madarakani halafu tukafanya vibaya kuliko hata hao CCM. Jifunzeni kutoka kwa Fredrick Chiluba kule Zambia.

Ni lazima tujenge utamaduni wa kukosoana. Na ni lazima tutambue kwamba CHADEMA kinaongozwa na binadamu wenye tabia kama za wale wa CCM. Kunahitajika kuonyana na kukaripiana ili kurudishana kwenye mstari na kuweza kujitofautisha na CCM. Kama tutaamini kila wafanyacho chadema ni kizuri, na hata wakikosea tunatafuta namna ya kuyapaka mafuta makosa yao, basi tutakimaliza hiki chama yumkini hata ikulu kinaweza kisiingie. Tukosoane ili tujengane.
cc. Kdm255

FIKIRI KWA USAHIHI MKUU. CCM WAMEFANYA ZURI LIPI?. Tuwasifie!. Ni lipi hilo unaloliona peke yako?. CCM WAMEIHARIBU SANA NCHI HII KWA UFISADI WA KUTUPWA NA MIPANGO ISIYO TEKELEZEKA?. Tuwasifie kwa lipi?. Litaje. CHADEMA kukosoana hakuna tatizo, ni wazo zuri sana.
 
ataenda kuutoa huo ushahidi wake mbinguni alikosema anakujua yeye
hapa mwigulu namfananisha na mtu anaejaribu kuzuia maporomoko ya maji kwa mikono
chadema ni poromoko kali CCM hawataweza kulizuia, mbinu zao zote zimeshindwa
Nape, TBC na star tv walikomalia sana hii habari
wacha leo nione single zao kwenye habari watasemaje.

Kwahiyo ule ushahidi wa mwigulu aliosema tumuombee mungu atautoa mahakamani umekwenda na maji?
 
Ushauri wangu kwa CHADEMA wachunguze mazingira ya uamuzi huu kufikiwa na kama hakuna mkono wa mtu uliochangia.hawa jamaa wa Lumumba hawaaminiki na wala hawakati tamaa bwana,isijekuwa ni njama ndani ya njama ndani ya njama....

ulichosema kinaweza kuwa na ukweli kwa asilimia nyingi.. Naamini imetoa faraja ili wakija kuhukumu kwa kosa la jinai.. Watu waishiwe cha kusema. So far they want to show and prove to people that judiciary is working so hard and independently.. So far we should be as calm as we can to see their next move.. But still this saga doesnt not justify the innocence of lwakatare with the charges until further judiciary steps taken
 
Back
Top Bottom