Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Amemwagiwa maji ya baridi mida hii

Kweli kabisa kabisa kwani maji na mafuta haviwi pamoja, yeye wa hovyo analeta mambo ya hovyo yaani hili chemba ni bure kabisa halifai kwa kila pahala.
 
Kinachotufanya tushangilie ni kwamba CCM hawataweza tena kukiita CHADEMA chama cha kigaidi. Maana mahakama imeshatoa hukumu kwamba hakuna ugaidi. Kwahiyo ile single ya ugaidi dhidi ya CHADEMA haina mvuto tena. Itabidi watafute single nyingine, bile kujali kama Lwakatare anapata dhamana au hapati.

Actually ile singo haikuuzika kabisa maana ndiyo Kinana na Nape walibebea bendi wakaenda nayo Kilosa. wiki moja baadae wakagalagazwa kwenye uchaguzi wa kijiji...
 
Wakili mkuu wa serikali aliyoongoza kesi hii namfahamu vyema kwa uadilifu wake!

Namfahamu vyema ndugu yangu Wakili Prudence Rweyongeza toka anasoma Rubya na baadae UDSM na baadae kupangiwa kituo cha kazi Tabora na baadae kurudishwa Dar;ni wakili mzuri mwenye msimamo na SIELEWI KWA NN ALIKUBALI KUCHUKUA KESI YA UONGO KAMA HII ILIYOMPA AIBU SASA!

Wakili Prudence Rweyongeza jinsi nimjuavyo sidhani kama alikubaliana nao wakuu wake kuongoza kesi hii ya ajabu;kuna kitu tu walimtishia!

Sijapata kuona kesi ya ajabu kama hii
 
Mbona wale wapambe hawachangii au wapo bize kuandaa hujuma nyingineeeeeeeeeeeeeeeeeeeee????????????????????????? Penye mungu shetani hana nafasi......"Walianza kwa kukimbia wamevunjika miguu wanaomba kubebwa...bora walioanza taratibu sasa hamna mpinzani"
 
Nakumbuka maneno ya kamanda Tundu Lissu
quote_icon.png
By Tundu Lissu
Hivi tunavyoandika humu ndani Wilfred Lwakatare yuko mahabusu ya Segerea kwa sababu amenyimwa dhamana kwa makosa ya kutunga ya ugaidi aliyoshtakiwa nayo. Na kwa wasiomfahamu, basi niseme kwamba hali yake ya kiafya sio nzuri kwa sababu anasumbuliwa sana na ugonjwa wa kisukari. Kwa mazingira aliyo nayo, dhana kwamba alitumwa na maCCM ili aihujumu CHADEMA is a bit far-fetched, to say the least. Kwanza kabisa, angekuwa ametumwa basi angetoa kauli ambazo ni more damaging kwa CHADEMA kuliko ilivyo sasa. Nimeisikiliza sana hiyo video clip na narudia kusema kwamba there's nothing in there inayothibitisha chochote kati ya makosa aliyotuhumiwa nayo. Nothing!!! Na hiyo ni kama tuna-assume kwamba video clip yenyewe inaweza kukubalika.mahakamani Kama ushahidi, kitu ambacho sheria ninayoifahamu mie inaniambia hapana. Pili, angekuwa ametumwa basi video hiyo ingemwonyesha yeye pamoja na 'mtumwa' mwenzake Joseph Ludovick Rwezaura ili kukamilisha ushahidi wa njama. Kwa hali ilivyo, video clip hiyo haimwonyeshi mla njama mwenzake na kwa hiyo haiwezi ikawa ushahidi wa kuthibitisha njama zozote. Kosa la kula njama linahitaji wakosaji wawili au zaidi. Aidha, kosa la kufanya mkutano wa kigaidi linahitaji 'magaidi' watatu au zaidi, sio wawili Kama inavyodaiwa katika kesi ya Lwakatare. Kama hakuna mkutano wa kigaidi hakuwezi kuwa na njama ya kufanya makosa ya kigaidi na wala hakuwezi kuwa uhamasishaji wa ugaidi, ambayo ni makosa mengine anayotuhumiwa nayo Lwakatare. Tatu, Ludovick na Dennis Msaki walikuwa na mawasiliano makubwa kati yao kwa zaidi ya mwezi mzima kabla ya tarehe 28 Desemba, siku ya kufanyika kwa makosa yanayodaiwa. In brief, katika kipindi hicho, Ludovick aliongea muda mrefu na Msaki kuliko alivyoongea na mie wake mwenyewe!!! Na hayo ni mbali na mawasiliano kati yake na Mwigulu Nchemba na kale ka-payment ka shilingi 50000 kwa M-Pesa wiki mbili baada ya Mwigulu Nchemba kuutangazia ulimwengu kuwa ana video ya mipango ya mauaji ya viongozi wa CHADEMA!!! Kitu kikubwa inachokithibitisha video clip hii, ukiachia njama dhidi ya CHADEMA na viongozi, ni jinsi ambavyo wahusika ni amateurs kwenye mambo hay a!!! Kwa maneno ya Sugu, 'wanahitaji kurudi studio', maana hii picha imeharibika!!!! !!!!
 
Last edited by a moderator:
. thatha Ritz chama hii habari hamjaipata ama? mpaka thatha
alijiabiza asubuhi hii, sijui anajisikiaje na huyo mwizi wa majina Mwigulu Nchemba, Tofauti ya maCCM na CDM, Maccm mnaanza na mashetani na mapepo kwenye harakati zenu, CHADEMA tumeanza na Mungu na tutamaliza na Mungu...

shetani kazi yake ni kukuingiza kingi kisha anakuanika,, shame on mwinepi+ kale kabibi
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo yuko nje kwa dhamana au bado yuo rumande.

Hata kama yupo bado rumande ni suala la muda tu atatoka maana shtaka lake la kula njama kudhuru mtu lina dhaminika tu tena kirahisi Mahakamani!
 
Ameedit sana hii habari. Habari original iliyoletwa hapa ilikuwa na sentensi moja tu. Nashukuru kwamba mods wameondoa post yangu maana kwa sasa haina maana tena. Lakini kwa wakati huo ilikuwa ni mhimu sana.
Hili ni pigo lingine kwa CCM. Tunamshukuru Mungu kwa kuwa upande wa wapigania haki.
Sasa unasomeka.
 
Nimepata simu toka kwa jamaa yangu kutoka pale Iramba, wamedai ole wake Mwigulu 2015 labda wampe ubunge wa viti maalum!
 
:clap2::lalala::welcome:karibu sana nyumbani lwakatare, tunakusubiri utandikiwe 'RED CAPET' hata mizinga ikiwezekana, " sign of victory'
 
Mashetani CCM wameshindwa vibaya sana, hongera Chadema
 
Hua sielewi, mkuu wa kaya anamsifiaga sana huyu jamaa, mbona project zake nyingi hua zinafeli mapema hata kabla ya majaribio? Kulikua na ile project ya kutishiwa kuuawa kwa njia ya sms, Marando akampa kubwa, alitengeneza mauaji kule Singida mjini, Igunga, Arumeru n.k, lengo likiwa nikifanya CDM kionekane ni chama cha mauaji lakini kilichotokea ndio hicho tena, watu wanazidisha imani kwao, hii movie nayo ilianza kuoesha dalili za kudoda sokoni mapema kabisa hata kabla ya kuingia huku kwenye mauzo, ilipigiwa promo ya kutosha kabisa, hivi ndio kusema huko magambani huyu ndio genus au?
 
Mwenyezi mungu hawezi kushindwa na shetani.Inasikitisha kama inawezekana kwa mti mbichi akina lwakatare wanaweza kupata mawakiri nawakabambikiwa kesi,je itakuwaje kwa mti mkavu? je wanyonge niwangapi wameuliwa,kubambikiwa kesi na kufungwa na serikali hii yakishetani?
 
Back
Top Bottom