Lusinde: Sisi wabunge tulipitisha Sheria tu lakini Kiwango(cha tozo) kilipangwa na Wizara ya Fedha

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (MNEC) na Mbunge wa Mvumi mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde amefunguka kuhusu makato ya miamala katika simu za mikononi ambapo amedai Bunge wao walipitisha sheria na kiwango kilipagwa na Waziri wa Fedha.

5EE4E288-7FA0-491F-A45A-A20B07AB6759.jpeg
 
Hoja kubwa sio hata hayo makato bali ni matumizi ya hizo pesa zitakazopatikana. Uwajibikaji katika matumizi ya serikali bado ni mdogo na hapo ndipo ilipo shida. Wanaotajwa na CAG hawafanywi lolote, wilaya, wizara na taasisi zenye shida katika mahesabu hakuna uwajibikaji.
 
Sasa tuambie wewe unajitoaje kwenye lawama,au wawakilishi,ni ipi kazi yenu,ilikuwaje hamkutaka kujua sheria inafanyaje kazi,au ni shida ile ya kuiwakilisha sirikali badala ya wananchi wa eneo lako,au kwa kuwa nafasi ilipatikana kwa hisani ya mwenye mamlaka ya kisirikali na sii sanduku lile la kula.
 
Wao kama wabunge hawakuuliza wizara kiwango cha makato?

Waliipa wizara kupanga viwango wanavyotaka?

Sasa walijadili nini kama hawakujua viwango vitakavyokatwa?

Ni sawa na uweke signature kwenye open cheque halafu umpe ruhusa mhasibu aandike kiwango anachotaka, atafanya anavyotaka tu na lawama zitakurudia wewe ulieweka sahihi.
 
Tozo ipo kwenye Kanuni (Regulations) siyo ktk sheria iliyopita Bungeni. Kanuni huwa haipiti bungeni, mwisho wake ni kwa waziri wa wizara husika. Kwa hiyo hata wabunge wenyewe hawana habari na viwango vya tozo, wamejikuta wakikubwa na makato. Sasa ni wakati wa Waziri husika kurekebisha tozo husika kupitia Kanuni husika. Hii hata johnthebaptist anajua pamoja na ubumbumbu wake wa sheria.....hahahahaha. Salama bwashee?
 
Nilitaka kushangaa kwamba hivi kuna chombo gani cha habari makini kinachoweza kumtuma mwana habari wake akamsikilize huyu zero...nilivyoona ni Channel 10 (TV ya CCM) sikushangaa.
 
Nakuelewa mkuu.

Hapo kwenye kanuni ndio shida ilipo, wizara zinajificha kwenye kanuni.

Kama wawakilishi wa wananchi wangekua makini basi wangeweka floor na glass ceiling that no body is allowed to break, hata kama kanuni zinatungwa basi zifuate sheria hiyo yenye ceiling.

Sasa wabunge hawajui waziri atakuja kuwatoza wananchi zao kiasi gani huoni hapo kuna shida?

Yaani wabunge wamekua surprised kama sisi wananchi, hao ni wabunge ama genge la wahuni?

Maana yake ukimuuliza mbunge wako uliweka sahihi kwa niamba yangu mwananchi nitozwe kiasi gani, hajui, sasa alipitisha nini?
 
Nilitaka kushangaa kwamba hivi kuna chombo gani cha habari makini kinachoweza kumtuma mwana habari wake akamsikilize huyu zero...nilivyoona ni Channel 10 (TV ya CCM) sikushangaa.
Walijua wanakipamba chama kumbe ndio wameharibu.
 
Mwambieni aaache genye, akakae kwa kutulia dawa imuingie vizuri, CCM ni kama kenge tu huwa hawasikii hadi masikio yapasuke
 
Back
Top Bottom