Lusinde: Sisi wabunge tulipitisha Sheria tu lakini Kiwango(cha tozo) kilipangwa na Wizara ya Fedha

Wameanza kugeukana ukoo wa panya.
Ukoo huo ni haribifu kupita maelezo, haujali wanacho haribu iwe vazi la sikukuu, harusi ama suti ya gharama, ilimradi ameharibu na kuwatengenezea wanae kirago cha kulaalia, ilmradi akuthibitishie kuwa yeye ni hodari wa kuharibu.
 
Nakuelewa mkuu.

Hapo kwenye kanuni ndio shida ilipo, wizara zinajificha kwenye kanuni.

Kama wawakilishi wa wananchi wangekua makini basi wangeweka floor na glass ceiling that no body is allowed to break, hata kama kanuni zinatungwa basi zifuate sheria hiyo yenye ceiling.

Sasa wabunge hawajui waziri atakuja kuwatoza wananchi zao kiasi gani huoni hapo kuna shida?

Yaani wabunge wamekua surprised kama sisi wananchi, hao ni wabunge ama genge la wahuni?

Maana yake ukimuuliza mbunge wako uliweka sahihi kwa niamba yangu mwananchi nitozwe kiasi gani, hajui, sasa alipitisha nini?
Ndugu yangu hiyo ndiyo nchi yetu, wabunge ni rubber stamp! Hakuna wanachojua zaidi ya posho yao. Hii nchi ingeendelea zaidi bila hii genge. Serikali ikishaandaa madudu yake kibajeti inaitisha hilo genge ili kuaminisha kuwa bajeti ya nchi ilipitaga bungeni na kuungwa mkono na majority ya wabunge. Otherwise hatuna wabunge. Ingekuwa nchi ya watu wenye akili tayari hiyo sheria ingesharudishwa bungeni au waziri husika ameshapewa order ya revise Regulations husika.
 
Sasa tuambie wewe unajitoaje kwenye lawama,au wawakilishi,ni ipi kazi yenu,ilikuwaje hamkutaka kujua sheria inafanyaje kazi,au ni shida ile ya kuiwakilisha sirikali badala ya wananchi wa eneo lako,au kwa kuwa nafasi ilipatikana kwa hisani ya mwenye mamlaka ya kisirikali na sii sanduku lile la kula.

Tuna shida kubwa sana!! Badala ya Bunge kuwa kweli chombo cha kutunga sheria imekuwa ni chombo kinachopitisha sheria. Ni aibu kuwa na wabunge wanaosema wanasimamia wataalamu wa wizara huku elimu zao na ujuzi ni wa chini! Ni aibu kusikia kuwa “mtunga” sheria anapigwa mkwara akitaka “kutoa shilingi” kutopitisha kitu alicholetewa!!

Ukishapitisha sheria unakuwa fully responsible na uzuri au madhara yake hasi!! Anachosema Lusindw hapa ni sawa na kumruka Mwigulu huku Mwigulu akisema hii ni sheria iliyotungwa na Bunge na huku Spika akitema cheche “anayepinga hii tozo atupe njia mbadala wa kupata fedha”.
 
Lusinde anazidi kuonyesha uwezo wake mdogo sana wa kufikiri, iweje unajiaibisha mwenyewe na wabunge wenzako wote.

Kwanza tozo zilivyoletwa bungeni kwanini hamkuhoji kiasi gani, pili Mh. Rais kashasema tozo zitaendelea, Mh. Spika kasema tozo zitaendelea, na watu tushakubali tozo iendelee, haoni yeye kama mbunge anaongelea kitu ambacho viongozi wake wa juu washalifunga tayari, yeye anazidi kuharibu. Low IQ kabisa
 
Sasa tuambie wewe unajitoaje kwenye lawama,au wawakilishi,ni ipi kazi yenu,ilikuwaje hamkutaka kujua sheria inafanyaje kazi,au ni shida ile ya kuiwakilisha sirikali badala ya wananchi wa eneo lako,au kwa kuwa nafasi ilipatikana kwa hisani ya mwenye mamlaka ya kisirikali na sii sanduku lile la kula.
Usimuonee bure Shule hamna hapo
 
Hoja kubwa sio hata hayo makato bali ni matumizi ya hizo pesa zitakazopatikana. Uwajibikaji katika matumizi ya serikali bado ni mdogo na hapo ndipo ilipo shida. Wanaotajwa na CAG hawafanywi lolote, wilaya, wizara na taasisi zenye shida katika mahesabu hakuna uwajibikaji.
Bunge la vilaza,kwa nini hamkumbana Waziri atoe rates nyie mkapitisha tu? Yaani mumeuziwa mbuzi kwenye sandarusi. Pumbavu zenu.
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (MNEC) na Mbunge wa Mvumi mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde amefunguka kuhusu makato ya miamala katika simu za mikononi ambapo amedai Bunge wao walipitisha sheria na kiwango kilipagwa na Waziri wa Fedha.

View attachment 1879248


Wizara ya fedha wanaoiba mabilioni kwa malipo hewa? WAnapata wazpi ujasiri wa kusema nchi inahitaji kuongeza mapato? Wana uchugnu gani na nchi hawa? Wameona wizi wa hazina hautoshi sasa wanaona wafkike hadi mifukoni mwetu? Hli jambo halipo.
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (MNEC) na Mbunge wa Mvumi mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde amefunguka kuhusu makato ya miamala katika simu za mikononi ambapo amedai Bunge wao walipitisha sheria na kiwango kilipagwa na Waziri wa Fedha.

View attachment 1879248
Huyu jamaa kweli mkichwa hakuna kitu kabisa.
Sasa huo utetezi wa kijinga , anaenda bungeni kufanya nini?
Kukusanya posho na kusugua viti kwa maka...li..!
 
Back
Top Bottom