Lusinde na kampeni za matusi umeambulia aibu kubwa

Alikua akipingana na nguvu ya MUNGU, tangu lini shetani akamshinda MUNGU?????????????
 
Wana JF,

Hakika matendo ya Mungu ni makuu. Mungu anazo njia nyingi za kuwaokoa watu wake. Alitenganisha maji watu wake wakapita jeshi la farao lilipojaribu kuwafuata likaangamia.

Ninajiuliza ilikuwaje CCM yenye vijana na wazee kama kina Salim, Warioba, Malecela na angalau Januari Makamba ikawaacha ikawaleta kwenye kampeni kina Wasira, Maji marefu, Lusinde Mkapa nk! Hapa ni Mungu aliwatia upofu au ni Mungu aliifanya mioyo yao kuwa migumu wasiwaone watu wenye uwezo wa kutumia busara? Toka nikiwa mdogo sijawahi kumsikia Wasira kaongea hata punje ya Busara, Maneno ya Mkapa hayajawahi kuwa na ladha kwa mwananchi wa kawaida toka alipotutangazia kufunga mkanda mwaka 1995/6.

Sala fupi.
Ee Mwenyezi Mungu, twakuomba uendelee kuwatia upofu wote wanaokumbatia ufisadi, ili wasiweze kumwona miongoni mwao mwenye busara. Waendelee kuamini kuwa pesa ndio kila kitu. Wasipate kujua kuwa nguvu ya uma yashinda utajiri wa aina yoyote. Waendelee kujua kuwa maneno ya busara ni matusi na kuwa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam ndo wawakilishi wa watanzania wote. Amen!
 
sasa hilo ndo jembe lenu pekee limebaki mkilifukuza shamba mtaendaje? Wakati wote anatukana mlikuwa wapi si mlishangilia matusi yake mkaona ametoa hoja za ushindi na mkaendelea kumpandisha jukwaani. Sauti ya Mungu imeshinda
 
usitarajie kuvuna maharage wakati umepanda pilipili, CCM imejaa uozo, usitarajie jambo lolote jema kutoka kwenye hilo genge la wahuni.
 
Wakuu najaribu kukumbuka jinsi campaigns zilivyokuwa zinaendeshwa Meru. Hasa kwa makada wa CCM ambao walikuwa kama wameshajihakikishia ushindi. Ila kilichoniuma ni lugha na dharau waliyokuwa wakiionyesha wakati wakiwa majukwaani. Namkumbuka sana Lusinde aka Mzee wa Matusi, Kibajaji etc. Kwa hali ya kawaida mtu mwenye busara huwezi kutamka au kutumia maneno aliyokuwa anayaongea Lusinde/Mzee wa Matusi..nilitahadharisha hapa kama akiendelea hivi hatafika mbali. Hata hivyo kuna haja ya CCM kuhakikisha hawa vijana hawatumiki kwenye campaign yoyote kwa sababu ya ukosefu wa busara na hekima. Sikutegemea hata BWM mzee niliyekuwa namheshimu naye angekuwa amelewa sifa na kuongea alichoongea Arumeru. Tujifunze kutokana na uchaguzi huu wa Arumeru Mash.:smash:
 
Tatizo la kulewa siasa..Naamini atakuwa amejufunza kitu. Kuna haja ya CCM kutafuta vijana wengine kuliko hawa waliokosa busara na hekima..Lusinde, Mwigulu. Hata mzee Wasira hawafai kutumika katika siasa ya sasa..
 
Sasa hivi hatuendi kwa hisia. Tunaenda kwa facts. Hisia zao kweheriiiiiiiiiii.
 
Back
Top Bottom