Luninga kwenye chumba cha kulala

Luninga kwenye chumba cha kulala

kwa sisi tuliokuwa na wake wenye mishahara mikubwa kuliko sisi ni bora miaka 100 kuwa na Tv chumbani maana ukimgusa mkeo akikukaripia basi unachukua series yoyote ya kikatili na kuiangalia ili ujifanye umesahau kumbe unaumia.
Nalog off


ha ha ha ha!!!!!!!!!!!!!

dah! umeongea ukweli hapo kwenye maumivu na namna ya kupotezea..........

swali la kizushi; mkuu umeoa lini tena?
 
Hebu tupe jibu ambalo utawapa kama wakikuhoji.

Hivi Bro, serious unataka nipange insha hapa za mjadala wangu na Malaika wangu jinsi nitakavyokuwa namfanya aelewe?

Kama Baba nina ushawishi wa kutosha kwa mwanangu na mawasiliano yanafanyika kwa amani tu na ananielewa kuwa kila ninachomuelekeza nafanya kwa nia nzuri tu...
 
Kwa mimi TV should be kila room kwenye nyumba. Sometimes I need peace of mind nachill room nawasha Xbox 360 yangu nacheza Devil May cry au GTA nikichoka nazima nalala.
 
ha ha ha ha!!!!!!!!!!!!!

dah! umeongea ukweli hapo kwenye maumivu na namna ya kupotezea..........

swali la kizushi; mkuu umeoa lini tena?
nimeoa jumatatu iliyopita mkuu ila samahani kwa kutokualika.
Nalog off
 
Ha ha ha ha, kwa nini series ya kikatili?
unajiafanya wewe ni katili utamuona mwenyewe anageuka na kuanza kukukaripia na kukwambia nakupa mara moja na usinisumbue tena sawa?basi unapewa shughuli na wewe unashughulika.
Nalog off
 
unajiafanya wewe ni katili utamuona mwenyewe anageuka na kuanza kukukaripia na kukwambia nakupa mara moja na usinisumbue tena sawa?basi unapewa shughuli na wewe unashughulika.
Nalog off

Mkuu hapo unaweka move ya zombie then unalisupport pale linapofanya ukatili..Akikugusa unajifanya kumpotezea na kumpush na kiwiko..Mwenyewe atachange
 
Kids are tricky, very, unaweza kuona watoto wanalala saa 1, kumbe wanalala asubuhi.

Kuna familia moja, watoto wako shule ya msingi, wana games chumbani, na tv iko sebuleni full dstv. Sijui kuna kipindi gani, walikuwa wanakipenda na kinaonyeshwa saa 9 za usiku. Wakawa wanaamka na kuangalia hadi asubuhi, wanajiandaa kwenda shule.

Na hii ilitokea tu sababu tv iko sebuleni ambako ni chini, na watoto na wazazi wanalala juu, wananyata kutoka chumbani kwao wanaenda sebuleni na kuangalia. Kilichokuja kufanya ikajulikana, mooja wao alikuwa darasa la 2, akawa analala sana darasani. Walimu wakaita mzazi na kumwambia tatizo la mtoto, baada ya huyo mdogo kubanwa sana ndio akasema, nakuwa nimechoka sababu naamka saa 9.

Sasa ndio uwawekee tv chumbani ndio kabisa, kama hakuna atakayechoka darasani ndio hutakaa ujue nini kinaendelea.

Kuhusu games, si tu siwez kuweka chumbani, bali hata kununua iwepo nyumbani siwezi hata kidogo. Games zina jinsi ya kula ubongo wa mtoto, sijui ni aje, but nachoamini ni kuwa mtoto akianza kupenda games tu, shule inakuwa matatani. Mie walishaomba games hadi wakasalenda, na wameshajua game halitakiwi nyumbani kwangu kabisa.

Komputa, yes lakini hata kuweka internet wawe na access nayo bado najiuliza. Sijui nitawa-monitor vipi kwa sasa bado wadogo, labda wakue kue kwanza.
mimi ni kati ya watoto tulilelewa tukiwa free.....
mama yetu alikuwa anasema sana lakini alikuwa anatuambia kabisa kuwa hawezi kukufwatilia kila sehemu. yeye ana kazi, wewe una shule, hawezi toka kazini kuangalia shule unafanya nini. Ila atakuambia mabaya yoooteee, amua wewe unachotaka kufanya.
Na sijisifii, but sijawahi wapa wazazi wangu shida katika malezi, nilikuwa mtoto mzuri sana pamoja na freedom niliyokuwa nayo.
Wanangu huwa nina tabia ya kwenda chumbani kwao mara kadhaa usiku, kuwatoa wakasusu lakini pia kuangalia wamelalaje, maana wanangu huwa nawalaza chumbani kwao tangu wakiwa wadogo sana, kwa hiyo nalazimika kuwachungulia mara kwa mara.
kuna siku niliwahi kuamka saa 9 usiku nikamkuta binti anaangalia TV, nikaizima, nikachukua kitabu chake cha hesabu, nikampa hesabu 100, nikamwambia nitazisahihisha nitakapoamka saa 12. akazifanya, nilipoamka nikakuta kamaliza, ila ndo ilikuwa siku ya kwanza na ya mwisho kurudia huo mchezo.
wanangu wanacheza sana games lakini kwa masaa niliyowaambia. huo muda ukifika hata umsemeshe wala hakusikii jinsi alivyo busy. na kuna games za masomo (angalia leapfrog), kuna masomo mbalimbali anajifunza huku anacheza, kama hutaki kuwanunulia hizo za akina ben10.
Kwangu bado hatujaona hayo madhara ya games kwa masomo, maana wanafanya vizuri sana shule na wanacheza games. siku nikiona inawasababishia wasisome itakuwa ndo mwisho wao wa kupewa games
 
unajiafanya wewe ni katili utamuona mwenyewe anageuka na kuanza kukukaripia na kukwambia nakupa mara moja na usinisumbue tena sawa?basi unapewa shughuli na wewe unashughulika.
Nalog off

mwambie aache kukupa kwa mgao utadhani yeye tanesco
 
aisee hapo NAMNAANI SINZA nasikia ni chimbo zuri kwa kugegeda wake za watu mi mwenyewe na mke mmoja wa mtu namvizia ikitiki tu na mpeleka hapo NAMNAANI nasikia ni bonge la chimbo limetulia kuna vyumba kama 100 hivi yaani hapo unaweza ukawa hapo hapo na mke wako anachapwa hapo bila kujua.
 
Mkuu hapo unaweka move ya zombie then unalisupport pale linapofanya ukatili..Akikugusa unajifanya kumpotezea na kumpush na kiwiko..Mwenyewe atachange
umeona eh! lazima ujitutumue kidogo.
Nalog off
 
ha haaa, EMT kweli unajua kuchokoza watu walikojificha.......
sidhani kama nazijua hasara za kutokuwa na TV katika chumba cha kulala, ila naweza kusema najua faida za kuwa nayo.
Nakubaliana na point nying ulizoziandika, kama ukiangalia kwa mtazamo wako...... lakini mimi (sisi) tunaangalia kwa kutumia pembe nyingine.
1) Itambulike kuwa siyo sababu una TV basi utakuwa unaiangalia masaa yoote. kama huna umuhimu wa kuangalia haina haja ya kuiwasha.
2) Mimi labda niseme ni wale wa old school, kuna sinema au program kwenye TV ambazo siruhusu wanangu kuziangalia, lakini kwa wakati huo huo mimi napenda kuziangalia. huwezi kujua hiyo sinema itaanza saa ngapi. badala ya kufukuza wanangu kwenda kucheza wakati naangalia kitu roho inapenda, ni bora nikaingia chumbani kwangu nikakaa na kuangalia kwa raha zangu.
3) sidhani kama kweli kuangalia TV kunapunguza muda wa sex katika ndoa, labda niseme inategemea unaangalia vipindi gani kwenye hiyo TV ya chumbani. Mimi napenda sana kuangalia romantic movies (siyo porns), na imeshatutokea mara nyingi tu tukashindwa kuimalizia sinema na kuendelea na mambo yetu. kuna sinema nakumbuka tuliiangalia kwa siku 3 ndo tukaimaliza, siku 2 za mwanzo zote tulikuwa tunaishia njiani.
4) siyo kila program unayoiangalia unakuwa na concentration 100%, mnaweza kuongea huku mnaangalia TV na mkaelewana tu, na kama kuna kitu serious cha kuhitaji 100% basi huwa tunazima TV na kuendelea na maongezi yetu. hatujawahi kukosa/ kupunguza muda wa maongezi sababu ya TV.
5) siyo kila siku wanandoa mnakuwa pamoja katika chumba cha kulala. kuna kusafiri. mmoja akisafiri basi mwingine anakuwa mpweke sana chumbani. kwangu wanangu wanalala latest saa 2. sasa kama mtu kasafiri na mimi nilale saa 2?
6) kusoma huwa nasoma saaana..... hili pia ninalo, ninakuwa na vitabu vya kutosha beside my bed, yaani nikifungua macho kabla sijatoka kitandani lazima nasoma angalau kurasa 2 za kitabu nitakachoguswa kukisoma siku hiyo. kwa maana hiyo kuwa na TV chumbani hakumaanishi utashindwa kujisomea, kuna wakati wa kufanya kila kitu, ni kujipanga tu.
7) ha haaaa, watoto walianza kuwa na TV kabla yangu baada ya kuchoshwa na kuangalia cartoons muda wote wanaotaka kuangalia TV. wao hakuna program wanayotaka kuiangalia zaidi ya cartoon, hata kukiwa na mgeni wanamshauri aangalie cartoon. njia rahisi ya kuwafukuza ni kuwa na TV yao chumbani (NB: hapa haimaanishi wanangu wanaangalia TV muda wote. wana muda wao wa kuangalia, na muda wa kulala huwa unaheshimiwa sana, hawawashi TV wanapotakiwa kulala).
8) kama kuna watu wanayaishi maisha yao ni sisi, tuna vitu vya peke yetu kabisaaaa, hatuyaigi hayo ya kwenye TV, tunaishi ya kwetu.
9) Mimi siyo mpenzi wa kuangalia mpira, mwenzangu ndo ugonjwa wake na mara nyinga anatamani sana niangalie naye. Muda pekee ambao atani-hook kwenye mpira ni kama tutaangalia kwa kitanda, tumejilaza..... huko sebuleni, no thanx.

NB: nakubaliana nawe kila chumba kina kazi yake lakini haimaanishi haziwezi kuingiliana. ndo maana kuna siku hapa tulikuwa tunajadili kuhusu wamama kuhifadhi household stocks chumbani wakati wana stoo sababu tu ya ufujaji wa matumizi ya vitu. Ukiona nina TV chumbani ujue ina matumizi yake ambayo naona yana faida kwangu na kwa mwenzangu

Nimeipenda hii
Like km mia nane hiv
Kiukwel napenda tv chumbani lol
Nimejifunza kitu
Thanx
 
Last edited by a moderator:
Nimeipenda hii
Like km mia nane hiv
Kiukwel napenda tv chumbani lol
Nimejifunza kitu
Thanx
TV chumbani siyo mbaya.... inategemea tu inaku-drive kiasi gani.
kama unakuwa-glued kwenye TV muda wote ukiwa room, hata kama upo peke yako inakuwa siyo nzuri hata kwa afya. lakini kama unaitumia tu kama kiburudisho muda muafaka, tatizo liko wapi?
Mimi kuna kipindi nakaa hata 2 weeks sijaangalia TV, hata ya sitting room
 
TV chumbani siyo mbaya.... inategemea tu inaku-drive kiasi gani.
kama unakuwa-glued kwenye TV muda wote ukiwa room, hata kama upo peke yako inakuwa siyo nzuri hata kwa afya. lakini kama unaitumia tu kama kiburudisho muda muafaka, tatizo liko wapi?
Mimi kuna kipindi nakaa hata 2 weeks sijaangalia TV, hata ya sitting room
ehehehhehehhehe sijui kakufunyuaje kwenye chimbo lako
af weeewe!ahahahahhaha SA NDIO NINI?eti cacico umeona dada kubwa alivo na makusudi!chaaaaaaaaaaaaa!twaaaafa!
 
Last edited by a moderator:
Wengine sisi tunaishi uswazi kule ambako chumba ni hicho hicho na sebule ni hiyo hiyo huku unaweza kusikia yale yanayoendelea kwenye chumba cha mpangaji mwenzako kwa kutokuwa na silling board

Bila kusahau kelele za muziki kwenye radio ndogo za kuchaji[hapa nawashukuru wachina kwa kutuletea hizi radio za kuchaji maana tunaishi nyumba zisizokuwa na umeme] ambapo kila mtu anakuwa anasikiliza stesheni yake,sasa hapo utaiwaza tv kweli?

:focus::focus:
Kwenye suala hili japokuwa ninakubaliana na mtoa mada lakini napenda kusema yafuatayo

Ili maisha yaende inatakiwa tuwe in control kwenye miili yetu,kitendo cha kuacha kuweka TV chumbani kwa kuhofia hili au lile wakati ukiamua hata hiyo TV unaweza usiiwashe hata mwezi mzima naona ni kama kutokujitendea haki sisi kama binadamu

Kuwa na amri kwenye miili yetu itasaidia sana kuwa na heshima kwayo na wengine pia!

napenda sana namna yako ya kufikiri!
 
Back
Top Bottom