EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,356
Kuna baadhi ya watu wa mujini waliobahatika kumiliki au kupanga nyumba yenye vyumba zaidi ya kimoja wanapenda sana kuwa na luninga kwenye chumba cha kulala aka kile chumba chenye nanii ya sita kwa sita. Watu kama Fixed Point watakwambia wazi kwamba:
sijui kwa nini chumba cha kulala napenda kiwe na kitanda na TV ya ukutani tu......
Kwa hiyo, hapo unawezakuta subuleni kuna luninga, chumbani kuna luninga na baadhi ya wale waliobahatika kupata watoto nao wanawawekea luninga kwenye nyumba vya watoto. Watu kama akina Fixed Point watatupa hasara za kutokuwa na luninga kwenye chumba cha kulala. Mie nitaweka hapa faida za kutokuwa na luninga kwenye chumba cha kulala.
- Kutokuwepo na luninga kwenye chumba cha kulala ina maana kutakuwa na mazungumzo zaidi baina ya wanaokitumia chumba hicho. Kwa wale ambao wanakitumia chumba hicho peke yao, bado kuna faida nyingi tuu hapo chini.
- Kila chumba kwenye nyumba kina shughuli yake. Chumba cha kulala ni mahususi kwa ajili ya shughuli mbili kuu. Wengi mnazijia, sina haja ya kuzitaja hapa.
- Maisha ni kuyaishi. Badala ya kupoteza muda wako kuangalia maisha ya watu wengine kwenye luninga ishi maisha yako. Usifanye maisha ya watu wengine kuwa ndiyo burudani ndani ya chumba chako cha kulala. Of course, ni vigumu kuepuka kufuatilia maisha ya watu wengine kwenye luninga lakini weka mipaka hasa ukiwa kwenye chumba chako cha kulala. Don't faill in the trap of watching other people living their lives. Instead live your life: T.I ft. Usher - My Life Your Entertainment Lyrics - YouTube
- Kuongezea namba 4 hapo juu, kuyaishi maisha yako ni pamoja na kuwa na muda kutafakari jinsi siku yako ilivyokwenda, ikiwa ni pamoja na kujifunza kutokana na makosa uliyoyafanya siku hiyo. Badala ya kuangalia luninga tumia muda huo chumbani wakati kumetulia na tafakari wapi unaweza kufanya vizuri zaidi kwenye maisha yako. Wanadai kinacho-matter zaidi ni kile unachofikiria mwishoni.
- Kama una watoto kuwa mfano kwa watoto wako. Kama nao wakitaka kuwa na luninga kwenye vyumba vyao kama ilivyo kwenye chumba chako utawakatalia kwa kigezo gani?
- Kama unasumbuliwa na kutolala kusoma ukiwa kwenye chumba chako hata kama ni threads za JF ni vizuri zaidi kuliko kuangalia luninga. Kusoma ni kuzuri sana kwa ubongo wako. Faida za kusoma zinazidi faida za kuangalia luninga.
- Kwa wanandoa kutokuwa na luninga kwenye chumba mean more sex. Inasemekana kuwa wanandoa walio na luninga kwenye vyumba vya kulala wanafanya sex nusu ya wa wanandoa wasiokuwa na luninga. Piga mahesabu mwenyewe hapo.
- Hata kama luninga inakaa ukutani bado inachukua nafasi ya chumba. Kama ilivyo kwa vyombo vingi vya kieletroniki, luninga inaleta vumbi chumbani. Luninga inakula umeme pia.
N.B. Huu uzi hauwahusu wale ambao wanamiliki au wamepanga chumba kimoja tuu ambacho wanakitumia kama chumba cha kulala, sebule, jiko, n.k.