"Hospitali za Serikali kuacha jukumu lake la msingi na kuanza kufanya kazi za anasa kama kuongeza ukubwa wa makalio badala ya kujishughulisha kikamilifu kutibu maradhi yanayosumbua wananchi, tunao uhaba mkubwa wa raslimali fedha katika kutatua matatizo ya huduma za afya, mfano leo ni zaidi ya miaka 3 tumeshindwa kutoa mtaji kwa MSD wa takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba kutokana na ukosefu wa fedha, hizi fedha za kununua mitambo na vifaa vya kuongeza ukubwa wa makalio zimetoka wapi?" -Mpina
Luhaga Mpina ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM) amezungumza hayo alipokutana na Wanahabari kwenye Uwanja wa New Amani Complex, Zanzibar wakati wa maadhimisho ya miaka Sitini (60) ya Mapinduzi ya Zanzibar