Luhaga Mpina amlipua Waziri Makamba, amtuhumu kwa Uhujumu Uchumi. Atoa wito kwa TAKUKURU kumchukulia hatua

Luhaga Mpina Mbunge wa Kisesa amesema Rais Samia alitaka mawaziri wamsaidie katika kujibu hoja za wananchi, hata hivyo jambo hilo halionekani sana kwa sasa, ambapo amesema mawaziri wapo kimya katika kujibu hoja za wananchi.

Mpina amesema wapo mawaziri hawajibu hoja za wananchi au huwa wanajibu kwa hoja nyepesi malalamiko ya raia, hali ambayo ameitaja kuwa sio kumsaidia Rais kama inavyotarajiwa.

Ametoa mfano wa waziri wa Nishati alivyojibu kuhusu ucheleweshwaji wa mradi wa bwawa la Mwl Nyerere ambapo Waziri wa Nishati alianza kulaumu kuwa Wabunge hawakutaka yeye awe waziri badala ya kujibu hoja iliyokuwa mezani.

Waziri ametolea mfano suala la kufuta tozo ya Tsh. 100 katika mafuta bila kufuata utaratibu. Ambapo amesema maamuzi ya waziri kufuta tozo hiyo amekutaja ni sawa na uhujumu wa mapato ya Serikali kwa kuwa fedha ya tozo hiyo ilikuwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/22.

Kwa kushindwa kufuata taratibu za kuondoa tozo, Luhaga Mpina amesema Waziri wa Nishati amekuwa amefanya kosa la Uhujumu Uchumi. Na ameshindwa kutafuta kukielewa chanzo cha upandaji wa bei za mafuta nchini.

Kufuta tozo ya Tsh. 100 bila kufanya tathmini kumeipotezea Serikali Tsh. Bilioni 30. Hivyo, hakuwa na nia njema, achukuliwe hatua, atoa wito kwa TAKUKURU kumchukulia hatua. Amesema suala la kumchukulia hatua sio jambo la hiari, ni kwa mujibu wa sheria.

Mambo mengine aliyoyataja katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari ametaja kuwa Waziri Makamba ameshindwa kujibu kuhusu bei za mafuta na mfumuko wa bei.
CCM imhoji ndg.Luhaga Mpina kwa maneno yake ya CHUSHO.....

#Siempre JMT🙏
 
Kwahiyo unashauri nini, uozo uendelee ?? Hakuna kumtaja mwenzake? Haujaeleweka hoja yako ni nini. Ingekuwa hivyo unavyofikiria hakuna hakimu hata mmoja angemfunga binadamu hata mmoja.
Katiba mpya itaweka viongozi Bora na serikali itakua loyal Kwa wananchi mana ndiyo waajiri wake.

Hakimu anayehukumu mtu aliyeufanya jambo Kwa Nia njema ni Shetani mkubwa.
Ndio maana mtu anatiwa hatiani Kwa kuangalia Nia yake wakati wa kutenda kosa.

Ndio maana watu wengine hawapendi haya masheria yaliyotungwa na watu waovu.
Wanaofuata sharia la Mwenyezi Mungu.

Shabiby na Ndugai muda mrefu sana walishauri suala la mafuta linadilishwe kanuni zake lakini rushwa Kwa wabunge inalitafuna Taifa. Sio wa upinzani kama Tozo Bweka Wala wa CCM wote ni rushwa TU halafu Makamba anawekwa kama chambo TU kulaumiwa.
 
Huyu ni yule Mpina aliyekuwa wazir wa uvuvi na ktk enzi zile za giza totoro kwa Wakerewe na atleast watu wote waliotegemea uchumi wao kwenye uvuvi na mifugo??🙆

Hivi naye bado anabwabwaj utumbo km huu kweli?🤭🤭
Mara hii tu keshasahau jaman kwel...?? Anyway jpm aliwah kuckika akiuthibitishia umati na taifa kwa ujumla km huyo Mpina ni "kichaa" na ndiy cv ilimpa uwazir,na hajawah kutoka hadharan kukanusha.

Basi Makamba amvumilie tu,maana hatukuwah kuckia lolote km Mirembe hosp walimaliza jukum lao kumhusu😂😂😂😂
 
Mpina alikuwa anachukua ng'ombe za wafugaji na kuzipeleka kwenye mazizi yake ? Huyu aliyefilisi wavuvi kwa sababu za kijingajinga kabisa?

Anamuota rafiki yake Kalemani, hatarudi pale nishati.

Huyu Mpina kama anauota uwaziri, asubiri usiku, ni kiongozi wa hovyo sana.

Luhaga Mpina anampinga sana mama Samia, asidhani 2025 ni mbali
Katika post yako sijaona utetezi wa hoja zaidi ya personal attack.Nikupe faida moja mkuu Kinembe.Katika hotuba ya mwaka mmoja wa mama Samia katibu mkuu CCM komredi Chongolo alitamka bila ya kupepesa macho kuwa ... wajanja walitaka kuingiza nchi gizani ili wauze majenereta" ni dhahiri muhusika ni January
Chongolo nae ni sukuma gang? Kama January hakufanya kosa kwanini rais amerejesha tozo aliyoiondoa January kwa hotuba tu?

Naona Mange nae anajaribu kupotosha akidhani huu ni umbea wa kuchafua hewa wakati ni jinai imetendeka. Kosa linaendana na sheria za nchi na ukiukwaji kanuni kama huna weledi wa hayo mambo kuwa msikilizaji tu.Haisaidii kutukana watu.

Tukutane kaanani
 
Wana chuki na Makamba wa watu kisa mjinga mwenzao kawaaminisha anahusika na kifo cha mungu wao!

Wamejaa ujinga tu ndo mana wanaua vikongwe kwao kwa kuwahisi tu kuwa ni wachawi
Bro jikite kwenye hoja! achana na hizi personal attack...
jitahidi kuwa tofauti na wajinga
 
Amejaa chuki tu dhidi ya Makamba!

Saivi Hakuna mgao na hali ya umeme umerudi kuwa kawaida! Kama kukatika umeme umeme haijaanza kukatika Leo wala jana!

Kuhusu bei ya Mafuta inabidi atuambie ni wapi duniani Mafuta hayajapanda bei!

Amejawa na chuki tu Huyu mpuuzi na mkabila! Wana hasira na Makamba wa watu Kwa kuendekeza upuuzi wao wa roho mbaya
Kama ww ulivyo na hasira nae, umejaa chuki na masimango
 
Kupanda kwa mafuta sio tatizo la Tanzania peke yake bali nila nchi nyingi duniani. Kunatoka na kuongezeka gafla kwa demand kuanzia mwishoni mwa 2021 na pia vita ya Ukraine.
Kumlaumu January kupanda kwa bei ya mafuta ni chuki, vita ya urais 2030 au uwezo mdogo wa akili!
 
Kumbukeni awamu ya 4 mpango kazi wao ulikuwa ni 'gas' ndio maana ule mchezo mchafu ukachezwa tena bungeni!

Kumbukeni walioleta wale wazungu wapo na wapo ktk level kubwa ya system iliyopo madarakani.

Kumbukeni ni wakubwa sana na tayari wameanza na ununuzi wa makampuni makubwa ya...
Jibu hoja wewe ya kuondoa tozo acha kupiga miluzi kwenye glasi
 
Hata hivyo anawaza kuondolewa makamba awekwe yeye hiyo ni ndoto.

Sipo na makamba, naweza kusema kawekwa mahali palipojaa ile AS USUAL, mpaka mfagizi ni mwizi.

Huo umeme ushakua kama ndonda ndugu, leo zima kesho gonjwa.

Vile amewekwa hiyo wizara kimkakati akomae, sie watoto wetu wanasota mitaani huko.
 
Angalia hapo chini bei za mafuta Europe mid March. Bei zao ni zaidi ya mara mbili ya bei zetu.
Euro 1 = Tshs 2527
99EED465-03C1-4487-85F7-3AC96B36F4AF.png
 
Mpina alikuwa anachukua ng'ombe za wafugaji na kuzipeleka kwenye mazizi yake ? Huyu aliyefilisi wavuvi kwa sababu za kijingajinga kabisa?

Anamuota rafiki yake Kalemani, hatarudi pale nishati.

Huyu Mpina kama anauota uwaziri, asubiri usiku, ni kiongozi wa hovyo sana.

Luhaga Mpina anampinga sana mama Samia, asidhani 2025 ni mbali
Umeongea meeng ila umesahau kusifia.. kauli yenu.. "mama anaupiga mwing"
 
Amejaa chuki tu dhidi ya Makamba!

Saivi Hakuna mgao na hali ya umeme umerudi kuwa kawaida! Kama kukatika umeme umeme haijaanza kukatika Leo wala jana!

Kuhusu bei ya Mafuta inabidi atuambie ni wapi duniani Mafuta hayajapanda bei!

Amejawa na chuki tu Huyu mpuuzi na mkabila! Wana hasira na Makamba wa watu Kwa kuendekeza upuuzi wao wa roho mbaya
Umeongea meng umesahau "mama anaupiga mwing"..

A. K. A wazee wa kusifia
 
Mpina ni mpumbavu kipindi akiwa waziri kanyanyasa sana watu! Na 2025 jina wanakata ubunge atausikia tu! Angekuwa mungu wao yupo madarakani angesubutu kulopoka hivyo?
 
Hivi gesi imeishiaga wapi wajameni. Kelele zote zile enzi hizo lakini sioni lolote
 
Back
Top Bottom