Luhaga Mpina amlipua Waziri Makamba, amtuhumu kwa Uhujumu Uchumi. Atoa wito kwa TAKUKURU kumchukulia hatua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Luhaga Mpina Mbunge wa Kisesa amesema Rais Samia alitaka mawaziri wamsaidie katika kujibu hoja za wananchi, hata hivyo jambo hilo halionekani sana kwa sasa, ambapo amesema mawaziri wapo kimya katika kujibu hoja za wananchi.

Mpina amesema wapo mawaziri hawajibu hoja za wananchi au huwa wanajibu kwa hoja nyepesi malalamiko ya raia, hali ambayo ameitaja kuwa sio kumsaidia Rais kama inavyotarajiwa.

Ametoa mfano wa waziri wa Nishati alivyojibu kuhusu ucheleweshwaji wa mradi wa bwawa la Mwl Nyerere ambapo Waziri wa Nishati alianza kulaumu kuwa Wabunge hawakutaka yeye awe waziri badala ya kujibu hoja iliyokuwa mezani.

Waziri ametolea mfano suala la kufuta tozo ya Tsh. 100 katika mafuta bila kufuata utaratibu. Ambapo amesema maamuzi ya waziri kufuta tozo hiyo amekutaja ni sawa na uhujumu wa mapato ya Serikali kwa kuwa fedha ya tozo hiyo ilikuwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/22.

Kwa kushindwa kufuata taratibu za kuondoa tozo, Luhaga Mpina amesema Waziri wa Nishati amekuwa amefanya kosa la Uhujumu Uchumi. Na ameshindwa kutafuta kukielewa chanzo cha upandaji wa bei za mafuta nchini.

Kufuta tozo ya Tsh. 100 bila kufanya tathmini kumeipotezea Serikali Tsh. Bilioni 30. Hivyo, hakuwa na nia njema, achukuliwe hatua, atoa wito kwa TAKUKURU kumchukulia hatua. Amesema suala la kumchukulia hatua sio jambo la hiari, ni kwa mujibu wa sheria.

Mambo mengine aliyoyataja katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari ametaja kuwa Waziri Makamba ameshindwa kujibu kuhusu bei za mafuta na mfumuko wa bei.
 
Ametoa mfano wa waziri wa Nishati alivyojibu kuhusu ucheleweshwaji wa mradi wa bwawa la Mwl Nyerere ambapo waziri wa Nishati alianza kulaumu kuwa wabunge hawakutaka yeye awe waziri badala ya kujibu hoja iliyokuwa mezani.
Kumbukeni awamu ya 4 mpango kazi wao ulikuwa ni 'gas' ndio maana ule mchezo mchafu ukachezwa tena bungeni!

Kumbukeni walioleta wale wazungu wapo na wapo ktk level kubwa ya system iliyopo madarakani.

Kumbukeni ni wakubwa sana na tayari wameanza na ununuzi wa makampuni makubwa ya...
 
Mpina alikuwa anachukua ng'ombe za wafugaji na kuzipeleka kwenye mazizi yake ? Huyu aliyefilisi wavuvi kwa sababu za kijingajinga kabisa?

Anamuota rafiki yake Kalemani, hatarudi pale nishati.

Huyu Mpina kama anauota uwaziri, asubiri usiku, ni kiongozi wa hovyo sana.

Luhaga Mpina anampinga sana mama Samia, asidhani 2025 ni mbali
 
Back
Top Bottom