Ludovick Joseph: Kilio cha usaliti - Sehemu ya pili

Sasa imeshabainika kuwa huyo Ludovick unayemtetea aliwasiliana na Mwigulu mara baada ya kunaliza kumrekodi Lwakatare Desemba mwaka jana na siku iliyofuata Mwigulu akatangaza kuwa ana mkanda wa video unaoonyesha viongozi wa Chadema wakipanga mauaji.
Nadhani kuwa Mwigulu hatakuwa mnafiki kama viongozi wa Chadema na kumkana Ludovick
 
Yuda Iskariote alipojuta hata waliomtumia hawakumsikiliza tena, waliuliza:hayo yatuhusu nini sisi?JULIANA PLUS MWAMPAMBA!
 
Umbali wa mawazo haya ni miles kadhaa..,mwenye mawazo mafupi ya sentimeta tatu hawezi kuiona logic na ukweli uliopo katika post hii.
Ingelikuwa kwa ushauri wangu basi ningeliwataka wakuu wa chadema sio kumpinga mtela *so far hakuna cha kupinga hapa coz vyote ni kweli, wajipange katika kuhakikisha kuwa kweli hii haikimalizi chama, wajipange kujisafisha na kujirekebisha mazima.
 
Kinachosikitisha zaidi ni kuwa inafanywa na vijana ambao wanawaza kuwa tegemezi katika taifa kwa kuwawakilisha wananchi ipasavyo badala ya kukesha kila siku kwa kuwaza namna ya uharibifu na uteketezi wa chama kingine! Punguzeni selfshness jamani... Mfikirie na m'Tanzania wa kawaida anaye hitaji ukombozi toka hali mbaya tuliopo sasa!
Suala hapo sio ubinafsi, ila ni hali halisi ya Machadema... Na wananchi wa kawaida wanahaki ya kujua yanayoendelea katika chadema...
 
Nitawaambieni juu ya wachache waliowahi kusalitiwa na kukanwa hadharani na vongozi waandamizi wa chadema kama ifuatavyo:-

i) DEUS MALLYA:nilijaribu na kufanikiwa kukutana na vijana wapambanaji wa Chadema hasa wale waliokuwa wanatumikia Makao Makuu ndipo nilipokutana na DEUS MALLYA ambae alikuwa akitumika katika kuchapisha mabango na vipeperushi ambavyo vilikuwa vinabeba ujumbe wa Chadema na falsafa mbalimbali za Ukombozi ambazo chadema ilikuwa ikinajinasbisha nazo.

Nilipokutana na DEUS tulipanga na kupeana ushauri wa jinsi ya kueneza na kusambaza vipeperushi hivyo na hatimae aliniunganisha na JOHN MNYIKA ambae kwa kipindi hicho alikuwa ni Mkurugenzi wa Vijana na Afisa wake akiwa Marehemu Regia Mtema, ambapo DEUS alikuwa ni mtu wa karibu na maafisa hao, hasa MNYIKA.Na walikuwa pamoja na kufanya mambo mengi, ninayoyakumbuka ni pamoja na;

a) Safari ya DEUS mallya kuelekea LIBYA katika kongamano la vijana akiwa muwakilishi wa vijanakutoka chadema chini ya usimamizi wa Mnyika.
b) Safari ya RUSSIA ambapo DEUS alinieleza kuwa alienda kwa mafunzo maalum.Lakini Mnamo mwezi wa tisa (9) mwaka 2008, baada ya kutokea kwa kifo cha kutetanisha cha Mheshimiwa CHACHA WANGWE ambapo DEUS alikuwa ni Dereva na mshukiwa wa kwanza katika ajali ile.

JOHN MNYIKA alimkana DEUS mara mbili; mara ya kwanza ni pale apohojiwa na maafisa wa polisi juu ya kijana DEUS akamkana, na mara ya pili alipokutana na vyombo vya habari kuzungumzia sakata hilo akamkana kwa mara ya pili.



.

Niweke tu kumbukumbu sahihi. Sijawahi kuhojiwa wakati wowote ule na maafisa wa polisi kuhusu Deus Mallya, ni kweli kwamba kwenye mkutano na wanahabari niliwahi kuulizwa swali iwapo Deus ni mtumishi au afisa wa makao makuu ya chama. Nilikana kwa sababu hakuwahi kuwa mtumishi wa makao makuu ya chama. Kuhusu kwenda Libya, nilikuwa mkurugenzi wa vijana wakati huo, safari yake hakutumwa na kurugenzi niliyokuwa naiongoza.

Mwampamba kwa kuwa uko CCM sasa waulize wakina Makamba mawasiliano ya CCM wakati huo ikiwemo ile fax, kabla na baada ya kifo cha Wangwe (Mungu amlaze mahali pema), badala ya kuandika tu uongo wenye mwelekeo wa propaganda chafu.

JJ
 
Ukionamtu tena kijana mdogo kama wewe anashangilia ccm juwa anaupungufu wa upeo wa hakili kuna vitu viwili 1. unaweza kuweza dalasani lakini kwenyejamii ukashindwa kuiongoza 2. kusoma kusikufanye ukajiona unajua kila kitu hatamatahila hufanya vizuri
 
Umegundua mwenyewe jinsi ulivyochemka. kumbe Ludovik na wewew ni sawa wote tajiri yenu alikuwa ni Mwigulu Mchemba. kiko wapi sasa. wasaliti wote tutawajua kabla ya 2014. bila haya anaenda kumrekodi mzee wa watu kwa ajili ya vipande thelathini vya fedha, hivi kweli huyu mtu ndio unataka atetewe kwa usaliti kwa ajili ya njaa. na baada ya kumaliza kazi yake akampigia simu mwigulu kumjulisha ya kwamba kazi aliyotumwa amemaliza na bado akaendelea kujiita yeye ni mwanachama wa chadema. TRAITORS ARE VERY DANGEROUS .adhabu yake ni kupigwa risasi hadharani.
 
Kweli nimeamini unatumiwa. ss watanzania si wa jana nawatu wa aina yako ni wengi mno kwenye jamii mnaitwa wachumia tumbo. mlikuwa CHADEMA kwa nia ya kufanya ushushushu sasa yamewatokea puani hata vitu ambavyo havina mantiki mnataka tuvione ni issue kubwa . there is no way. Kaendelezeni propaganda zenu pale lumumba.Kiko wapi sasa suala la mauaji ya Kibamba mmefanikiwa kupoteza attention ya watanzania kwa ajili ya single yenu na Mwigulu lkn ni lazima tuje tuhoji. sisi tun Mungu nyie mna pesa na mamlaka.
 
Mimi naona hoja za Mwampamba zina mashiko sana, na kwa wale vijana na watu wanaoona Mwampamba anatapata hapa wamelamba galasa. Mtela kabadirika sana kwa sasa anakuja na hoja za maana zinazoamsha fikra na mawazo ya vijana kujitambua. Kuna thread iliwahi kuletwa humu kwamba Mtela Mwampamba na Juliana Shonza ni watu hatari sana kwa ustawi wa Chadema watu watu wakachukulia mzaha.

Nimekupata mkubwa wangu unapojaribu kuitikia chorus ya wimbo unaouimba mwenyewe na kubadili sauti katika kiitikio kujisapoti! Poa!
 
Mtela Mwampamba... Kusema kweli haijalishi kama haya ni kweli ama ni uongo. Inachojalisha ni kuwa wewe ndiye umeyatoa, baada ya kuwa mwana CCM baada ya kushindikana kuwa mwana CDM. Kwamba siku zote uliona sawa kumezea na sasa ndiyo wakati wa kuyaanika?

Kwa mwananchi yeyote atakae kuwa anatumia habari hizi ama Siasa za gutter politics zinazotumika kama kigezo pekee cha kuki judge Chadema atakuwa bado ni mchanga katika kutambua vigezo vya kuchagua chama na ni dalili ya kuwa ndiyo wale washabiki hata kura siku ya mwisho hapigi!

Hakuna Chama kisicho na madhaifu, kama ilivyo Chadema na madhaifu yake... Ila hii nguvu na devotion yenu juu ya Chadema na Viongozi wake inatupa walakini wa nia yenu huku ikitoa picha ya woga mkubwa mlio nao juu ya Chama na viongozi wa Chadema.

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa inafanywa na vijana ambao wanawaza kuwa tegemezi katika taifa kwa kuwawakilisha wananchi ipasavyo badala ya kukesha kila siku kwa kuwaza namna ya uharibifu na uteketezi wa chama kingine! Punguzeni selfshness jamani... Mfikirie na m'Tanzania wa kawaida anaye hitaji ukombozi toka hali mbaya tuliopo sasa!
wee dada wee, unakaa kimya mda mrefu wee, ukija unakuja jumla jumla,
ubarikiwe sana aisee.
 
Tatizo la hawa vijana hawakuwahi kusikia ule usemi wa CCM ina wenyewe. Nafikiri walikuwa wototo. Ndiyo maana ikina Nape wanaanzisha CCJ halafu wanarudi CCM na kuendelea kupeta. Hao ndiyo wenye CCM!!!
Yeye hajui hata sherehe ya tarehe 29 December 2012 katika kituo cha star TV, Yahaya alipigiwa simu tu Na Zitto Kabwe na Mwigulu Nchembe ,,Julius Itatiro yeye alikuwa hajui kitu nadhani,Yahaya baada ya kuombwa audience akawaruhusu makanjanja non planners ambao hawajawahi kushinda vendetta yeyote, Zitto na Mwigulu wakatukana chadema wee kwa tani yao, Kwa sababu Zitto alikuwa hamgombezi Mwigulu na kuweka sawa mambo ambayo Mwigulu alikuwa anatuhumu chama chake , baada ya mwigulu kurudia rudia rudia kuhusu video kama kawaida yake Zitto akaslide watu wakaanzisha thread hapa akajifanya eti alikuwa anawahi ndege kwenda Ruaha ,Zitto leo ameumbuka mchana peupe anaruhusu watu kuhujumu chama chake kwa kushirikiana na rafiki zake Mwigulu ,Ludovicky,Ridhiwani,January Makamba,Nape jamani dunia kweli usiku wa giza
 
Niweke tu kumbukumbu sahihi. Sijawahi kuhojiwa wakati wowote ule na maafisa wa polisi kuhusu Deus Mallya, ni kweli kwamba kwenye mkutano na wanahabari niliwahi kuulizwa swali iwapo Deus ni mtumishi au afisa wa makao makuu ya chama. Nilikana kwa sababu hakuwahi kuwa mtumishi wa makao makuu ya chama. Kuhusu kwenda Libya, nilikuwa mkurugenzi wa vijana wakati huo, safari yake hakutumwa na kurugenzi niliyokuwa naiongoza.

Mwampamba kwa kuwa uko CCM sasa waulize wakina Makamba mawasiliano ya CCM wakati huo ikiwemo ile fax, kabla na baada ya kifo cha Wangwe (Mungu amlaze mahali pema), badala ya kuandika tu uongo wenye mwelekeo wa propaganda chafu.

JJ
mkuu umetuacha na fumbo kubwa mno
 
Mtela, ningependa kukushauri tu kuwa km kijana ni mhm ujifunze kuwa "kiongozi" wa watu. Siasa ni nyenzo ya kusaidia wenye ideology inayofanana kuomba kushika dola ili itumie raslimali zilizopo kuwaletea maendeleo wananchi (ambao pia ndio wapigakura).

Kiongozi bora si anayewanyooshea wengine vidole (iwe kweli au si kweli). Siasa safi ni kushughulisha vichwa vya wenye itikadi ya juu ya namna ya kuwashawishi wananchi waamini muongoze. Pia, iwe ni za halali au la, kiongozi shupavu ni yule anayetunza siri za serikali, taasisi, au kampuni anayoifanyia kazi. Na kiongozi bora akibadilisha ideology (km ww), hutumia knowledge yake ya wapinzani kuweka mikakati ya ndani kupanga mbinu sahihi za kupata uungaji mkono wa umma. Kamwe huzunguki na kukashifu (iwe ni jambo la kweli au la) kule ulikotoka.

Kumbuka viongozi karibu wote waanzilishi wa upinzani nchini walitokea CCM na sijawahi kuwasikia wakieleza kiunaga ubaga vifo vya akina Stan Katabaro (Mwandishi wa Gazeti la Mfanyakazi - aliyeandika khs Loliondo kuuzwa), kifo cha Mama Salome Mbatia (akiwa M/Hazina CCM wakati wa EPA), kifo cha Imran Kombe, upotevu wa fedha za Import Support, kifo cha Horace Kolimba (Katibu Mkuu - CCM), nk.

Kwa post yako hii Mtela umetuonesha sisi tusio na vyama kuwa:
1. Umetumwa kuleta hili ikiwa ni mkakati usio endelevu wala wa kuijenga nchi ambao CCM unautumia kwa sasa,
2. Alignment ya post yako haina umakini and inakosa central theme,
3. Huna ukomavu kabisa wa kisiasa na kiuongozi ambayo ni kwa kuwa uliingia kwenye siasa ukiwa hujapevuka,
4. Hujui km unatumika km bulldozer na uki-depreciate utaanza kuitukana CCM na kuhamia UPDP,
5. Unahitaji counseling na niko tayari kukusaidia.

Hiwezi msaidia kitu kwani wewe ni m.na.f.k unaejifanya huna chama wakati post yako inajipambanua,ni bora ya mwampamba ambae kaamua kuvaa mabom hadharan kuliko wewe unaejificha usijulikane ulietumwa na mabosi wako kwa maslah binafsi na wala si maslah ya chama
 
Hivi Mtela mwampamba umetumwa? na je nani kakutuma? Kuwa makini ndugu yangu maisha ni upendo na sio vita.

Leo magwanda na mikakati yao yakudhuru wanahabar unasema siasa ni upendo,chacha kaondoka hivihivi kimasihara kwasababu ya uroho wa watu wachache wa kwenda mogogoni
 
Leo magwanda na mikakati yao yakudhuru wanahabar unasema siasa ni upendo,chacha kaondoka hivihivi kimasihara kwasababu ya uroho wa watu wachache wa kwenda mogogoni
Uwe na kumbukumbu KIkwete aliyemtuma Deus Mallya alimtoa gerezani baada ya miezi mitatu tuu angallia utaja mpeleka the hague bure Kikwete
 
Deus Malya mwenyewe anasemaje kuhusu hizi hadithi ?, sababu haya mambo ya kumsemea mtu wakati mwenyewe ni member humu ndani na ana access na computer nadhani ni kuandikia mate wakati wino upo
 
Last edited by a moderator:
huyu jamaa Mwampamba hawezi kuwa mwanasiasa nadhani hata siasa hajui ni kitu gani,hivi sasa anaanika siri za chadema baadae akikerana na CCM ataanika siri za CCM,hali itaendelea kwa kila anakokwenda,inaonesha huyo jamaa ni mbinafsi sana
 
CDM.... mnahaha sana mnashindwa kujibu kabisa hoja hapa....mnaandika upuuzi..CDM imekuwa ikiwatumia vijana kwa operesheni zenu chafu, wakikamatwa mnawakata kwa kisingizio hawakuwa watumishi wa chama...hii mbaya sana.

Bora muwaweke wazi kwamba mnawatumia kwa kazi maalum kikinuka shauri yao.....acheni kuandika ujinga hasa wewe mnyika ndio umeandika pumba sana..na kwa vile uozo wenu tunao..kaeni tayari utakuwa wazi soon....
 
Deus Mallya kashaweka ukweli wote kule facebook kwamba ulimuomba msamaha kwa kumkana wewe unaendeleza porojo hapa pole sana .Ama kwa hakika siku ya kufa nyani miti yote huteleza .R.I.P CHACHA WANGWE
 
Umbali wa mawazo haya ni miles kadhaa..,mwenye mawazo mafupi ya sentimeta tatu hawezi kuiona logic na ukweli uliopo katika post hii.
Ingelikuwa kwa ushauri wangu basi ningeliwataka wakuu wa chadema sio kumpinga mtela *so far hakuna cha kupinga hapa coz vyote ni kweli, wajipange katika kuhakikisha kuwa kweli hii haikimalizi chama, wajipange kujisafisha na kujirekebisha mazima.

Ukweli ungekisaidia zaidi Chama Cha Majangili, kwasababu kwa upande wa CHADEMA hapo sijaona ukweli wowote katika post ya huyu stela mwampamba zaidi ya muendelezo wa majungu yake na chuki zake kwa viongozi wa chadema baada ya kutimuliwa. Inaonyesha kuwa kutimuliwa kwake bado hajakubaliana nako ndio maana kila kukicha anatafuta mambo yake ya kipuuuzi ya kutunga ili aichafue CHADEMA lakini mwisho wa siku kila uchafu anaouleta humu unamrudia yeye mwenyewe na masalia wenzake.
 
Back
Top Bottom