Lucky Dube ana mziki mzuri kuliko Bob Marley.

Lucky Dube ana mziki mzuri kuliko Bob Marley.

Ukisikiliza mziki wa Lucky Dube vizuri utagundua kamshinda Bob Marley kwa vitu vingi,sauti,beats,ingawa kiujumbe wanafanana,ila mziki wa Lucky Dube unavutia zaidi ukisikiliza.
Nadhani Bob Marley alipata umaarufu zaidi baada ya kufa,angekuwa hai angefunikwa sana na Luck Dube.
Kumbuka Technology pia ilikuwa imeendelea zaidi kipindi cha Dube tofauti na Marley Bob
 
Tatizo lucky mziki wake una ala nyingi kiasi kwamba inageuka kua kelele ila ukija kwa Bob unaskia ile ladha halisi ya gitaaa ...ambayo ni nzuri sana wakati wa tahajudi na ule mmea pendwa
 
Huyu bwana mdogo alisababisha siku nimesoma thread yake nisile kwa huzuni.nlisikitika sana na nikatamani atuombe radhi sisi na wana reggae na ninaamini hata lucky dube alikwazika sana kusikia anafananishwa na robert nesta marley.itakuwa ali mind sana.

Kabisa hata yeye anaona hakutendewa haki.ni sawa na kulinganisha kichuguu na mlima kilimanjaro. Namsisitizia aombe msamaha kwa hili kosa.alinifanya weeke nzima nimsikilize bob tu then nije msikiliza lucky.nikasikitika sana anaweka ulingoni bondia wa heavy weight apambane na fly weight. Its totally unfair na unyama mkubwa sana.

Umenena ilivyo haki mkuu bob Marley kumfananisha na luck dube ni sawa na kufananisha meli na mtumbwi,,, dube bado ni mdogo sana na kinachomfanya mtoa thread amkubali zaidi luck dube ni aina ya reggae aliokuwa akipiga.
Kwa sisi tunaojua asili na kufuatilia mziki wa reggae tunasema hakutawahi kutokea mwimbaji kama Bob Marley.
Utofauti ni kwamba Luck dube alikuwa akitumia sana kinanda na trumpets hii inaitwa "modern reggae" yaani kama kwenye taarab umchukue hayati Issa Matona au Bi Kidude ufananishe nyimbo zao na za akina Mzee Yusuph au Khadija Kopa, zote ni taarab lakini midundo na aina ya uimbaji ni tofauti kwa msikilizaji. Robert Nesta Marley alikuwa akitumia zaidi ngoma na gitaa zito (base) na hii ndiyo asili halisi ya reggae.
 
Usimfananishe Bob Marley na luck dube hata Siku moja , dube bado sana labda umfananishe na hao wengine aisee
Ukisikiliza mziki wa Lucky Dube vizuri utagundua kamshinda Bob Marley kwa vitu vingi,sauti,beats,ingawa kiujumbe wanafanana,ila mziki wa Lucky Dube unavutia zaidi ukisikiliza.
Nadhani Bob Marley alipata umaarufu zaidi baada ya kufa,angekuwa hai angefunikwa sana na Luck Dube.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi kabisa mkuu
Naona Unatumia nguuvu nyingi katika kutofautisha Marekani na Haiti nani Zaidi... Jibu Utapata Marekani zaidi ni hivyo hivyo kwa Bob Marley na Luck Dube... Bob atakuwa juu au mshindi kwa kila idara za mziki wa Reggae ndio maana aliitwa Mfalme wa Reggae... Hata Kwenye Soccer Pele na Messi Pele atakuwa juu kumzidi Messi.... hiyo ndio hali halisi...

Radio One Walishajaribu kuweka Shindano kama Lako na Nani Zaidi Bob Marley akaibuka mShindi Luck Dube Album yake ya Kwanza na ya Pili Ndizo zilimuweka juu sana... hadi watu wakaona labda wamempata Mrithi wa Mfalme wa Reggae baada ya wakongwe wengine kuchemsha kama Alfa Blondy na Geogery Isaac kuweweseka...

Ukitaka kuwasindanisha tuende kwa vibao vyao.. Wimbo ulio Best kwa Dube ni Back to My Roots na kwa Bob naweza Sema ni Natural Mystic sasa ukienda head to head mwishowe Bob anakuwa mshindi kwa Point nyingi hivyo tafuta mwenye level ya Bob japo hajapatikana kwa head to head. pole Sana.....

Vibao vya Bob Vingi ni vikali sana... Visikilize utambue...

Stiff naked Fool,
Buffalo soldier,
Rastaman Give Up, kitu hakuna kukata tamaa
Satisfy my soul,
Natural My stick,
Time will tell,
Jamming,
Kaya,
Jump Nyabighi,
Real Situation,
One Drop,
Stir it up, huu hata wasiopenda reggae hutabasamu kimoyo moyo
Comining from the cold, hichi kitu ni noma sana...
Easy Skanking, Tulizo haswa
Crazy Baldheads, Hii kitu ukisikiliza vyombo vinavyonyonwa nyongwa ni fantastic
Blackman Redemtion, kwenye album ya Confrontation yaani ni hatari tupu
Bad Card..

Tumuache Mfalme awe Mfalme... kumfananisha Bob na Dube ni sawa na TL Kumtukana Nyerere

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu .. nikweli kwamba tunapaswa kuheshimu maoni ya watu hata kama yanapingana na maoni yetu ... ila naomba nikwambie wazi kwamba ume puyanga ..tena Sana Bob ni habari nyingine. Nampenda sana lucky dube napenda uandishi wake lakini kwa bob akasome tena .... halafu unapaswa kutambua kwamba Bob amefanya mziki katika liposuction ambacho technology ilikuwa bado haiko matured kama ilivyokuwa technology ya kuanzia miaka ya 90, kuja juu ",= nachomaanisha ni kwamba sounds ya music ya mwaka 75, haiwezi kuwa sawa ki-quality na sounds ya mwaka 90 kuja juu .... so naomba nimalize kwa kusema tu kwamba .... Bob ni extraordinary

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya ngoma za msondo na twangapepeta unazizimia zipi,same as Bob na lucky by the way Bob is the best amepenya kwenye dunia zaidi ya Lucky hata kabla hajafa umaarufu was Dube uko Afrika sana
 
Nakubaliana nawe kwa asilimia kadhaa.

Lucky Dube...

Slave,

Sent using Jamii Forums mobile app
Bob na Dube kuwalinganisha ni Ukosefu tu wa Abadu...

Chukua Idadi ya Nyimbo alizoimba Bob na Dube Jibu utapata za Bob ni Nyingi
Chukua zile Best za Dube na za Bob utapata za Bob best ni Nyingi Sana
Ukichukulia Sweet reggae za Bob na za Dube utapata za Bob ni Nyingi zaidi
So Bob ni wa Kumshindanisha na Timu kubwa ya Wana Reggae yaani Team against One na sio Dube pake yake.

Ukiweka Album ya Legend na Confrontation ni Balaa tupu Bado Uprising, Kaya, Babylon by Bus Mwendo ni Mabalaa tupu
 
Mkuu .. nikweli kwamba tunapaswa kuheshimu maoni ya watu hata kama yanapingana na maoni yetu ... ila naomba nikwambie wazi kwamba ume puyanga ..tena Sana Bob ni habari nyingine. Nampenda sana lucky dube napenda uandishi wake lakini kwa bob akasome tena .... halafu unapaswa kutambua kwamba Bob amefanya mziki katika liposuction ambacho technology ilikuwa bado haiko matured kama ilivyokuwa technology ya kuanzia miaka ya 90, kuja juu ",= nachomaanisha ni kwamba sounds ya music ya mwaka 75, haiwezi kuwa sawa ki-quality na sounds ya mwaka 90 kuja juu .... so naomba nimalize kwa kusema tu kwamba .... Bob ni extraordinary

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hapo kwenye Sound kuna zile records ambazo hazikuwa na sauti poa zilisharekebishwa zikawa Bomba sana huwezi Amini... Kama One Love ni ya Mwaka 1965 Original version yake haiko poa ila iliporekebishwa na kurecordiwa upya ni Moto....
 
Okay
Mkuu hapo kwenye Sound kuna zile records ambazo hazikuwa na sauti poa zilisharekebishwa zikawa Bomba sana huwezi Amini... Kama One Love ni ya Mwaka 1965 Original version yake haiko poa ila iliporekebishwa na kurecordiwa upya ni Moto....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Peter Tosh ndiye mwalimu wao wote sema Bob alipendelewa na island records iliyopo nchini uingereza kwa sababu ni mixed race baba yake alikuwa mwenzao wakabadisha jina kutoka wailers to Bob Marley and the Wailers,peter Tosh akauliza why Bob Marley and the Wailers what about me and Bunny wailer sisi bendi haituhusu au,Tosh na Bunny wakanza solo career,na ikumbukwe Tosh kashinda Grammy award ya reggae Bob hajawahi kushinda,baada ya kifo cha Bob tosh aliulizwa jibu alilotoa ni kwamba mwache atangulie wengine wapate nafasi kwa sababu alikuwa anapendelewa,na hakuna mtu enzi hizo alikuwa na ubavu wa kumpinga Bob zaidi ya Tosh,RIP steppin Razor.
 
Wakati Bob marley anafariki luck dube alikuwa anaimba?
Alikuwa anaimba kwa kizulu,Tosh alivyoenda kuperform south ya Makaburu uwanjani kukawa kumejaa wazungu tupu,akauliza nipo Afrika mbona sioni waafrika uwanjani,wakamwambia wengi wao hawakuwa na uwezo wa kununua ticket,akasema hata perform,ndiyo wakafungua mageti watu wakaingia bure.
 
Watu wengi hawajui kwamba Peter Tosh amemfundisha hata Bob Marley Muziki baada ya Bob kurudi Marekani aliwakuta wenzake Bunny na Tosh wameshakuwa Marasta na wanapiga muziki aina ya SKA. Tosh akamfundisha gitaa na akamuunganisha Bob na Rita Marley.
 
Back
Top Bottom