Lucky Dube ana mziki mzuri kuliko Bob Marley.

Lucky Dube ana mziki mzuri kuliko Bob Marley.

lucky dube utamuona bora coz enzi za BOB technology iliyokuwa inatumika haikuwa sophisticated kiivyo!
 
Hapa inategemea kila mtu anavutiwa na kitu gani kwenye mziki.
Wote Lucky Dube na Bob Marley waliimba reggae, lakini kila mmoja alikua na vionjo vya aina yake na uimbaji wa aina yake.

Binafsi, napenda reggae ya Lucky Dube kuliko mwimbaji yeyote yule, naomba nieleweke vizuri hapo, sijasema Lucky Dube ni bora zaidi ya waimbaji wote wa reggae ila mimi binafsi, navutiwa sana na uimbaji wake, na mpangilio wake wa vyombo achilia mbali mashairi yake.

Kingine kilichokua kinanivutia zaidi ni uwezo wake wa kuimba reggare katika mitindo mbalimbali kama vile I wanna know what love is, God blessed the women, ding ding licky licky ni reggae zilizoimbwa kwa style tofauti na kuongeza utamu.

Mwisho, mapenzi yangu kwa Lucky Dube ni yeye kutokutumia bangi kama kilevi.

Tujikumbushe kipande cha wimbo wa one love kivivyoimbwa na Lucky Dube na kuona ujazo wa mziki.


 
Last edited by a moderator:
huyo Dube kaimba wakati gani na Bob kaimba wakati gani so beat haziwezi kuwa na ubora sawa,pili hata kwenye mpira jezi za zamani ni duni kuliko za sasa..Jiulize Bob aliimba katika kipindi kipi na dunia ilikua unahitaji nini?

Technologia ya sasa nyimbo hata iwe na ubovu gani kwa sasa tech inarejesha au kuongeza utamu wa muziki nyimbo za zamani za Bob zile za miaka ya 60s ndio zilirekodiwa kwenye system ya kale ila kila siku zilivyokuwa zinasogea zilirekebishwa ndio maana kuna album zilitoka baada ya yeye kufa...

Wewe nadhani kiasi si mtu wa live music umezoea kusikiliza tu ndio maana unaishi kwa hisia tu... vyombo vya music vimeboreshwa tu. Luck Dube hajawafikia kwa ubora U40 sembuse Bob Marley Mfalme...! Ukitaka tukuwekee site za nyimbo za kale na baada ya kubadilishwa kuwa digital nadhani utaduwaa tu... hata hizo jezi pia zinaweza fanyiwa mambo zikaonekana ni bomba kama za kisasa utashangaa tu... ushaona makochi ya kale watu wanayachange na kuwa masofa?
 
Mkuu tuweke hansadi vizuri.Peter Tosh alimfundisha Bob kupiga gitaa tu na sio mziki kama mziki.
Ndio hapo sasa. Hawa vijana wa leo sidhani hata kama wanamfahamu Joe Higgs (baba lao) ambaye ndiye haswa aliewafunda akina Bob, Peter na Bunny!
 
Bob alipiga hard raggae wakati akina Luck Dube wanapiga sweet raggae

Dube labda umlinganishe na UB40 ambapo naamini anasubiri pia sema tofauti yao ni ujumbe

Enzi za Bob bana kila chombo kilipigwa manually, ubora wa vifaa pia haukua mkubwa but still unau feel muziki kiuhalisia

Akina Lucky dube wamekuja na mavinanda automatically, vifaa vya hali ya juu nk
 
Bob alipiga hard raggae wakati akina Luck Dube wanapiga sweet raggae

Dube labda umlinganishe na UB40 ambapo naamini anasubiri pia sema tofauti yao ni ujumbe

Enzi za Bob bana kila chombo kilipigwa manually, ubora wa vifaa pia haukua mkubwa but still unau feel muziki kiuhalisia

Akina Lucky dube wamekuja na mavinanda automatically, vifaa vya hali ya juu nk

Luck Dube yeye alishamzungumzia Bob Marley ni Nabii wa Reggae na watu walishajaribu kumuua wakashindwa (Ambush in the Night - Song ya Bob Marley baada ya kukoswa kuuliwa japo alipigwa risasi..)
They tried to kill it
Many years ago
Killing the prophets of reggae
Destroying the prophets of reggae
But somebody said
To all the bald heads
Respect the rastaman
´Cos he ´s the only one
Only one left in jah creation
 
Naona mnamvunjia heshima lejendare, bob wa kulinganishwa na dube?
 
Watu wengi hawajui kwamba Peter Tosh amemfundisha hata Bob Marley Muziki baada ya Bob kurudi Marekani aliwakuta wenzake Bunny na Tosh wameshakuwa Marasta na wanapiga muziki aina ya SKA. Tosh akamfundisha gitaa na akamuunganisha Bob na Rita Marley.




hapana mkuu. bob alianza muziki kitambo na wimbo wake wa kwanza ni "judge not" alioutoa mwaka 1962 akiwa na miaka 16 tu. alikuwa anafanya sanaa akiwa na bunny. baadae ndo wakakutana na peter tosh wakiwa kwa mwalimu wa muzic joe higs wakaamua kuungana nae. kuhusu kumuoa rita ni kwamba bob alimuoa few days kabla hajaenda marekani kwa mamake. aliporudi akaungana tena na kina peter na buny wakatoa kibao cha "bend down low". kuhusu rastafarianism bob alifundishwa na muhubiri martima planno. there is no where peter amemfundisha music bob
 
nikirejea kwenye mada iliyoko mezani nadhani si sahihi kumlinganisha bob na msanii yeyote yule wa reggae. namheshimu sana dube lakini watu wa kuwashindanisha nae labda Alfa Blondy. wale kina bob na tosh walikuwa wahubiri wa rastafarianism kuptia music, mtu aliyefuata nyayo zao ni Senzo peke yake. dube aliimba music tu kwa melody ya reggae but he was not spiritual
 
nikirejea kwenye mada iliyoko mezani nadhani si sahihi kumlinganisha bob na msanii yeyote yule wa reggae. namheshimu sana dube lakini watu wa kuwashindanisha nae labda Alfa Blondy. wale kina bob na tosh walikuwa wahubiri wa rastafarianism kuptia music, mtu aliyefuata nyayo zao ni Senzo peke yake. dube aliimba music tu kwa melody ya reggae but he was not spiritual
kwani ubora wa mziki ni kuimba spiritual?iwe spiritual au isiwe kwenye mziki cha msingi ni wimbo kuvutia
 
Naona Unatumia nguuvu nyingi katika kutofautisha Marekani na Haiti nani Zaidi... Jibu Utapata Marekani zaidi ni hivyo hivyo kwa Bob Marley na Luck Dube... Bob atakuwa juu au mshindi kwa kila idara za mziki wa Reggae ndio maana aliitwa Mfalme wa Reggae... Hata Kwenye Soccer Pele na Messi Pele atakuwa juu kumzidi Messi.... hiyo ndio hali halisi...

Radio One Walishajaribu kuweka Shindano kama Lako na Nani Zaidi Bob Marley akaibuka mShindi Luck Dube Album yake ya Kwanza na ya Pili Ndizo zilimuweka juu sana... hadi watu wakaona labda wamempata Mrithi wa Mfalme wa Reggae baada ya wakongwe wengine kuchemsha kama Alfa Blondy na Geogery Isaac kuweweseka...

Ukitaka kuwasindanisha tuende kwa vibao vyao.. Wimbo ulio Best kwa Dube ni Back to My Roots na kwa Bob naweza Sema ni Natural Mystic sasa ukienda head to head mwishowe Bob anakuwa mshindi kwa Point nyingi hivyo tafuta mwenye level ya Bob japo hajapatikana kwa head to head. pole Sana.....

Vibao vya Bob Vingi ni vikali sana... Visikilize utambue...

Stiff naked Fool,
Buffalo soldier,
Rastaman Give Up, kitu hakuna kukata tamaa
Satisfy my soul,
Natural My stick,
Time will tell,
Jamming,
Kaya,
Jump Nyabighi,
Real Situation,
One Drop,
Stir it up, huu hata wasiopenda reggae hutabasamu kimoyo moyo
Comining from the cold, hichi kitu ni noma sana...
Easy Skanking, Tulizo haswa
Crazy Baldheads, Hii kitu ukisikiliza vyombo vinavyonyonwa nyongwa ni fantastic
Blackman Redemtion, kwenye album ya Confrontation yaani ni hatari tupu
Bad Card..

Tumuache Mfalme awe Mfalme... kumfananisha Bob na Dube ni sawa na TL Kumtukana Nyerere

ongeza na wimbo wa bob Slogan.najua wengi hawaujui
 
Back
Top Bottom