Hata kama angekuwa hajaoa katika familia ya mke wa Lowasa, ili aweze kuteuliwa kushika nafasi hiyo, lazima atakuwa na mafungamano na mkuu wa nchi kwa namna nyengine.
Kwa hali ya siasa za sasahivi ndani ya ccm, sidhani kama kikwete anaweza kumteua mtu mwenye ukaribu wa aina yoyote na Lowasa.
Nijuavyo mimi Lubuva ana undugu na mke wa lowasa aidha kaoa ktk ukoo wa mke wa lowasa nijuavyo ni jamaa yao
Hongera Jaji(Mst) Lubuva!
Nafasi hii ni changamoto kubwa sana kwa miaka hii, na unahitaji kuchezea kwenye fair playground, vinginevyo utakuwa KIMUNYA wa Kenya!
Na huyu naye mkataba wake wa ajira ya umma unaisha lini?UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENTS OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Aidha, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.
Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu, 2011.
Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.
Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. **Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.
Imetolewa na:
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22 Desemba, 2011
Sijui ina maana gani kwa kweli - ni kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya au ni kupokezekana kwa sababu ya kupokezana. Sina sababu ya kumpongeza bali namtakia pole kwa kuingia kwenye ukuti ukuti wa CCM. Zamu yake tu "kuingia upepo". Akitenda haki atapongezwa so far. Nasema karibu.
Hongera Jaji(Mst) Lubuva!
Nafasi hii ni changamoto kubwa sana kwa miaka hii, na unahitaji kuchezea kwenye fair playground, vinginevyo utakuwa KIMUNYA wa Kenya!
kWANI UMETHIBITISHA KUWA HAWA JAMAA NI MAADUI? JAMAA HAWA WANAJUA KUCHEZA NA AKILI ZA WATATNZANIA, WANAIBUA BIFU KATI YAO HALAFU NO FA BALI KUJENGEANA MAZINGIRA YA KULINDANA TU
Na huyu naye mkataba wake wa ajira ya umma unaisha lini?
Hongera Jaji(Mst) Lubuva!
Nafasi hii ni changamoto kubwa sana kwa miaka hii, na unahitaji kuchezea kwenye fair playground, vinginevyo utakuwa KIMUNYA wa Kenya!
Twaihuka ki? Eleza waitu, unawapongeza/unatupongeza niniWaitu mwaiyuka!