Lubuva Mwenyekiti mpya Tume ya Uchaguzi!

Kazi ipo hawa ndio watakuwa tayari kutoa matokeo ya kweli na katiba mpya??kazi kubwa sana sana wanayo maana CDM wakishinda watakuwa tayari kutangaza kweli na haki??
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Aidha, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011.

Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.

Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu, 2011.

Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.

Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. **Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.

Imetolewa na:

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

22 Desemba, 2011
kuuliza si ujinga ni kutaka kufahamu
1.hivi post ya chairman wa nec lazima mtu awe mstaafu?
2. Hivi atuna young blood ambao wanaweza kufanya hiyo kazi?
Katika pekuapekua zangu inaonyea hii tabia ya wastaafu kuongezewa mikataba au kupewa ajira mpya ipo kwa kiasi kikubwa hapa kwetu ambayo inafanya tuwe tanzania special .wenzetu ambao wanajua nini maana ya kustaafu wameanzisha ngo mbali mbali na wastaafu wote wanajiunga katika hizo ngo ili watu na mashirika mbalimbali wanawatumia hao wastaafu katika issue za utaalam katika nyanja mbali mbali wanaslogan yao.retired but not tide.nashangaa hapa kwetu wanaendelea kukumbatiwa.
Mytake.kati ya vitu ambavyo vinatakiwa viwe wazi kwenye katiba mpya ni
1.kuondoa powers za raisi kuteua watu kushika nafasi nyeti katika taasisi na mashirika mbalimbali badala yake ziwe na interview kwa wenyevigezo na interview iwe public.hii itazingatia ueledi na siyo ushikaji
2. Mtumishi wa umma akisha staafu akapumzike ataombwa ushauri itakapo bidi tunaamini katika miaka 4o ya utumishi wake atakuwaamewagroom wa chini yake.
3.kuwe na kusign perfomance contract kwa viongozi katika ngazi zote.na kuwe na review every after six month kama hajadeliver na hana sababu ya msingi tunapiga chini.
 
Sijaona lolote jipya katika uteuzi wa rais.The big problem of our country is weak institutions an their working system and their setup in combination with their constitutional Mandate on which tume ya uchaguzi operate, we can have very good people but the system is not their best allies
 
Kwa nini hizi kazi ziende kwa majaji wastaafu?licha ya kuingiliwa utendaji wa tume na mteuaji hata wao wenyewe wanatia huruma,nilimhurumia Jaji L Makame siku alipotakiwa kutoa ufafanuzi na vyombo vya habari kwenye uchaguzi wa mwaka jana.
 
The same old story.

Hivi kweli kuna sababu ye yote mfanyakazi wa Bongo kustaafu kazi? Mtu anastaafu kazi halafu ghafla from nowhere mfanyakazi huyo huyo anazaliwa upya na kuwa mwari anabebeshwa bonge la kazi mpya.

Nauliza swali nini maana ya kustaafu hasa?? Au ina maana Bongo tumeishiwa kabisa wasomi mpaka kila siku tunasikia recycling ya makapi yale yale.

Halafu hivi Bongo tutapata lini tume huru ya uchaguzi?

Ooh samani nimejisahu kweli, Raisi alishatangaza ajira mpya million moja!
 
Wote Makada watiifu wa CCM! Hivi kwa mwendo huo demokrasia ya kweli Tanzania itakuwepo?
 
Damian Lubuva ni mwanachama wa CCM, kwani hata amepata kuwa Mbunge na Waziri wa Sheria. Umri wake ni zaidi ya miaka 70. Hata Jaji Mkuu anatakiwa kustaafu afikapo miaka 65. Iweje kazi nzito ya tume ya uchaguzi apewe kibabu? Hivi atakua na umri gani ifikapo 2015?

Halafu, eti Regina, mke wa aliyekuwa Waziri Mkuu Lowasa, ni mdogo wa mke wa Lubuva. Itakuaje Lowasa akigombea urais na Lubuva ndio tefa?

macinkus
 
Damian Lubuva ni mwanachama wa CCM, kwani hata amepata kuwa Mbunge na Waziri wa Sheria. Umri wake ni zaidi ya miaka 70. Hata Jaji Mkuu anatakiwa kustaafu afikapo miaka 65. Iweje kazi nzito ya tume ya uchaguzi apewe kibabu? Hivi atakua na umri gani ifikapo 2015?

Halafu, eti Regina, mke wa aliyekuwa Waziri Mkuu Lowasa, ni mdogo wa mke wa Lubuva. Itakuaje Lowasa akigombea urais na Lubuva ndio refa?

macinkus
 

picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 28 December 2011

Gumzo la Wiki


RAIS Jakaya Kikwete ameendelea kukabidhi usimamizi wa masuala muhimu ya umma kwa watu waliozeeka, waliochoka na, au wanaokabiliwa na shutuma, tuhuma na lawama za kushindwa kuwajibika huko walikotoka.

Wiki iliyopita, alikabidhi kazi ya kuongoza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), viongozi wawili wastaafu, mmoja kati ya hao wawili akikabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Aliyekabidhiwa kuongoza NEC, wakati akiwa amechoka na kuzeeka, ni Jaji mstaafu Damian Lubuva ambaye amefanywa kuwa mwenyekiti wa tume hiyo.


Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, Jaji Lubuva ameshika nafasi mbalimbali
serikalini. Amekuwa mwanasheria mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), waziri wa sheria na katiba wa serikali ya Muungano na mwanasheria mkuu wa serikali hiyo.


Amewahi pia kuwa jaji wa mahakama ya rufaa nchini na mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma. Jaji Lubuva alistaafu utumishi wa umma miaka mitatu iliyopita na kwa umri hatofautiani sana na mtangulizi wake – Jaji Lewis Makame.


Anayekabiliwa na lundo la tuhuma, shutuma na lawama za matumizi mabaya ya madaraka, ni jaji mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid, ambaye Kikwete amemkabidhi jukumu la makamu mwenyekiti.


Jaji Mahamoud, kama ilivyo kwa Jaji Lubuva, ni mstaafu. Alikuwa askari polisi kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu ya Zanzibar, alikostaafu Aprili mwaka 2011.


Ameingia kwenye chombo hicho kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Omari Makungu, ambaye Julai 2011 aliteuliwa na serikali ya Zanzibar kuwa mwanasheria mkuu (AG) na baadaye jaji mkuu.


Ndani ya mahakama kuu ya Zanzibar, Jaji Mahamoud ameondoka bila kujibu madai yaliyokuwa yanamkabili yeye binafsi. Alidaiwa kupokea mlungula wa mamilioni ya shilingi kutoka kwa Mohammed Raza, mfanyabiashara na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), visiwani Zanzibar ili kumfanyia upendeleo kwenye shauri lililokuwa likimkabili mahakamani hapo.


Raza alidaiwa na wakurugenzi wenzake wawili wa kampuni ya upakuzi na upakiaji wa mizigo kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar (ZAT) na kuendesha kampuni yao kinyume cha utaratibu. Alituhumiwa pia kujipatia dola za Marekani 40 milioni kinyume cha sheria na kanuni za fedha za kampuni hiyo.


Mmoja wa mashahidi Marhoon Seif Marhoon alieleza mahakama kuu ya Zanzibar, chini ya hati ya kiapo, jinsi jaji alivyohongwa; kiasi alichopewa, mahali alikokabidhiwa, siku alipochukua kile anachodai kuwa mlungula na nani aliyemkabidhi.


Kupitia ushahidi wa shahidi wake huyo, upande wa madai ulimtaka Jaji Mahamoud kujiondoa kusikiliza shauri hilo ili kulinda kile kilichoitwa "hadhi yake binafsi na ile ya mahakama."


Pamoja na uzito wa madai hayo, Jaji Mahamoud alikataa kutekeleza ombi hilo. Aligoma kuunda jopo la majaji kuchunguza tuhuma dhidi yake na alikataa kujiuzulu wadhifa wake wa Jaji Mkuu.


Hadi anaondoka kwenye nafasi yake, wananchi wa Zanzibar hawakuweza kupata ukweli wa tuhuma dhidi ya aliyekuwa jaji mkuu wao. Hawakujua kama ni kweli alihongwa au alikuwa anasingiziwa.


Hadi sasa, hawajaweza kufahamu kama Raza alitoa mlungula huo ili kumlainisha jaji mkuu. Walichobahatika kukifahamu, ni uamuzi wa Jaji Mahamoud kutaka Raza na wenzake wapatane na kumaliza suala hilo nje ya mahakama. Basi!


Si hivyo tu. Jaji Mahamoud ameondoka kwenye utumishi huku akituhumiwa na Chama cha Wanasheria wa Zanzibar (ZLS), kufanya upendeleo wa kumteua mmoja wa watoto wake – Fatuma Hamid Mahamoud Hamid – kuwa jaji mahakama kuu ya Zanzibar, kinyume cha taratibu.


Tuhuma dhidi ya Jaji Mahamoud zilifikishwa hadi kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein. Inadaiwa hata uamuzi wa serikali wa kutoongeza mkataba wake kwa mara ya pili, ulitokana na kukabwa na tuhuma hizo.


Aidha, Jaji Mahamoud, wakati wa utumishi wake, alituhumiwa kuchelewesha kwa makusudi, upatikanaji haki kwa waliokwenda mahakamani.


Mfano hai, ni shauri Na. 3 la mwaka 2006, lililofunguliwa na S/LT Ahmed Khatibu Said na P.O. Juma Maulid Jecha, dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali ya Zanzibar, mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) na mwenyekiti wa mahakama ya kijeshi ya KMKM.


Wadai waliwasilisha mbele ya mahakama kuu ya Zanzibar ombi la kutaka mahakama hiyo ibatilishe uamuzi uliotolewa na iliyojiita "mahakama ya kijeshi ya KMKM" ya kuwafunga kifungo cha miaka 5 gerezani. Faili la kesi hiyo lilikaa kwa jaji huyo kwa zaidi ya miezi mitano bila kulipangia jaji wa kulisikiliza.


Hata pale mahakama ya rufaa ilipoamuru kesi hiyo isikilizwe upya na mahakama kuu ya Zanzibar, kutokana na hatua ya Jaji Mbarouk Salum Mbarouk kusema mahakama yake haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo, bado faili la kesi hiyo liliendelea, kwa zaidi ya miezi saba, kubaki bila kupangiwa jaji mwingine wa kuisikiliza.


Baada ya shinikizo kutoka kwa familia na mawakili wa wadai, hatimaye Jaji Mahamoud alikabidhi kesi hiyo kwa Jaji Abraham Mwampashe ambaye alikubaliana na madai yaliyowasilishwa mahakamani hapo na kusema mahakama ya kijeshi ya KMKM ilikosoea katika kufikia uamuzi wake huo.


Maamuzi ya Jaji Mwampashe yalitolewa mwezi mmoja baada ya Ahmed Khatibu Said na P.O Juma Maulid Jecha kumaliza kifungo chao.


Ni chini ya utawala wa Jaji Mahamoud, gari la mahakama lilifanya kazi za CCM katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.


Gari hilo liliondolewa namba za usajili za serikali (JM) na kubadikwa namba binafsi na kisha kukabidhiwa kwa Ummy Mahfoudha Mahamoud, mke wa jaji na makada wengine wa CCM ili kufanyia kampeni.


Katika mazingira haya, bado Rais Kikwete anapata ujasiri wa kumteua Jaji Mahamoud kusimamia jambo zito kama Tume ya Uchaguzi.


Je, rais anataka kusema wasiotuhumiwa, waandilifu wamemalizika kwenye taifa hili? Kama Mahamoud ameshindwa kusimamia mahakama, atawezaje kusimamia uchaguzi? Atawezaje kuendesha uchaguzi huru na haki? Je, huu waweza kuitwa mzaha?


Hata uamuzi wa rais kumteua Julius Benedicto Mallaba, kuwa mkurugenzi wa uchaguzi, hauwezi kukosa doa. Mallaba aliyechukua nafasi ya Rajabu Kilavu, alikuwa mkurugenzi wa mikataba (Contracts and Treaties) katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG).


Kwa wadhifa wake huo, Mallaba alikuwa mtendaji na msimamizi mkuu wa mikataba kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.


Hivyo basi, kama kuna mtu ambaye hawezi kujiondoa kwenye ufisadi wa mikataba uliolitafuna taifa hili, basi ni Mallaba. Kwa vyovyote vile, atakuwa ameona, ameshiriki au kunyamazia, mikataba kadhaa ya kinyonyaji ambayo imefunga taifa hili.


Na hili linathibitishwa na Rais Kikwete mwenyewe pale aliposema, "Tunatafunwa na mikataba mibovu iliyoingiwa kutokana na ufahamu mdogo walionao wanasheria wetu waliopo kwenye eneo hilo." Hapa bila shaka Kikwete alikuwa anamtaja Mallaba.


Je, kama Rais Kikwete anakiri kuwa waliotuingiza mkenge kwenye mikataba ni akina Mallaba na wenzake, vipi ameteua mtu huyohuyo kusimamia uchaguzi? Uzalendo huo anautoa wapi?


Kwa matatizo yaliyopo ndani ya NEC; malalamiko yanayoibuka kabla na kila baada ya uchaguzi, Watanzania wasitarajie mapya kwenye tume hii. Watarajie mfumo wa uchaguzi kuwa uleule; ukandamizaji dhidi ya wagombea wa upinzani kuwa palepale; wizi wa kura kuendelea kushamiri na uchakachuaji wa matokeo kuzidi kushika kasi.


Kama Rais Kikwete angekuwa analitakia mema taifa hili na pengine yeye mwenyewe, asingejaza ndani ya NEC watu waliochoka, wanaotuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka na walioshindwa kazi huko walikotoka.


Rais angeweka kwenye chombo hiki watu makini, mahiri, waaminifu, waadilifu, wachapa kazi na ambao utendaji wao hautiliwi shaka; watu wanaoweza kusimamia haki na ukweli; wanaotaka haki hiyo itolewe kwa kila anayestahili na waliotayari kumwambia rais kuwa chombo hiki kina mfumo mbaya, hivyo kiundwe upya.


Ni nadra sana kwa wateule wa aina hii kumshauri rais kuhusu umuhimu wa muundo mpya wa NEC na majukumu yake. Hata ikitokea "wakashauri," basi ushauri utakuwa mwepesi, mweroro na usioweza "kuwaharibia kipato cha mwisho" maishani mwao.


Mbona nchi hii ina watu wazima na vijana wanaoinukia; wenye sifa za kufanya kazi ambazo sasa wanasukumiwa waliochoka mwili na kwa mujibu wa umri na sheria; achiliambali wanaotuhumiwa? Tutafakari.




 
Kiwete.... sory, Kikwete ni yule yule jana, leo na hata baada ya uongozi wake huu kumalizika. Ana majibu mepesi kwa maswali magumu. Ni muendelezo wa fikra za kifedhuli za "VIJANA NI TAIFA LA KESHO". Hana jipya na wala hatarajii kulipata. kinachonifurahisha zaidi, ni kwamba; Kikwete ni MTUME. Tena Mtume wa Mungu aliyetumwa kuja KUIMALIZA CCM. KWA HILO, NINAMSHUKURU.
 
Lubuva amechoka ana baggage yaani kazeeka toka niko darasa la kwaza mpaka sasa yeye yuko serikalini mimi nimemaliza sekondari chuo kukuu nimeoa na watoto na kurukaruka

Mohmod Hamid ana issue na Mohamed Reza kuwa alihogwa peza na kupoteza $ 40mil za co workers lawyers'''
 
Nchi ya ajabu sana hii. Rais anafanya uteuzi wa watu ambao wanashutumiwa kwa kukosa uadilifu kwenye nafasi nyeti kama tume ya uchaguzi, kisha aje atueleze kuwa uchaguzi utafanyika kwa uadilifu?
 
Labda Jk alimwambia Shein kama kuna watu huko zenj wanahatarisha muungano lete majina yao niwatafutie nafasi huku. Dk shein kwa akili ana offload wana rushwa.
 
Yaani kwa watu niliochoka nao ni huyu sijui mnamwita Kiwete! Haki ya nani huyu jamaa ni mvivu wa kufikri na ni janga kwa Taifa letu. Nakosa ushawishi tu kwa wanajeshi wetu. Walah alikuwa wa kupindua huyu! Ama ningekuwa na uwezo wa ki-Mungu ningemchukua kwa manufaa ya Taifa.
 
Labda Jk alimwambia Shein kama kuna watu huko zenj wanahatarisha muungano lete majina yao niwatafutie nafasi huku. Dk shein kwa akili ana offload wana rushwa.

Kuna wengine wanafumbiwa macho madhambi yao ili kulipa fadhila za kuwa mwanachama hai, mpenzi, mfurukutwa wa CCM tu
 
Hiyo ni namna nyingine ya kulindana na kulimbikiziana pesa. Watu wameshastaafu na kama pensheni walishapokea alafu wanarudishwa tena kwenye payroll wakati wako watu ambao hata umri unawaruhusu kufanya hiyo kazi kiufanisi zaidi.
Alafu eti tunashangaa na kulalamika tukiambiwa nchi yetu haina maana.
 
Moja ya tatizo letu kubwa Watanzania ndani ya serikali............ni succession programs..........
 
Back
Top Bottom