Hivyo unaona ni sahihi kumteua kwa kuwa ni mwanachama wa chama kilichozoeleka! Hapo ndipo unapokosea; mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ndiye refa wa uchaguzi, akisema huyu kashinda hakuna wa kuuliza wala kukata rufaa mahakamani, sasa kama mwanaccm anataeuliwa kwa uccm wake atatoaje haki kwa cuf? - Tafakari, mnaipeleka nchi pabaya!
Bwana Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Halafu kwa nini hawa wenyeviti wote wanakuwa majaji?
Majaji ndio wanaonekana wana gravita katika kuamua with impartiality na wanaelewa mambo ya katiba na sheria za uchaguzi zaidi it seems.
But as long as they are chosen by the president all that aura of impartiality is tainted.
wasio jitambulisha na chama chochote = na wasio na chama chochote? Human action can not be fully understood.haya ndiyo mamlaka ya raisi kwa mujibu wa katiba iliyopo... Pengine kwa katiba mpya tunanotarajiwa kuiandika wote tutaainisha nini maana ya tume huru ya uchaguzi na inapatikanaje? Wenzetu walio kwenye demokrasia zilizoendelea ( za miaka mingi) tume hizi zinaongozwa na watu wasiojitambulisha na chama chochote cha siasa ili wawe kweli huru na ushawishi wa siasa za vyama!!! Si vibaya sisi tukaiga hilo..
Thats the bottom line, so lets hope he has good intentions on the new constitution issue.Haya ndiyo mamlaka ya Raisi kwa mujibu wa katiba iliyopo... Pengine kwa katiba mpya tunanotarajiwa kuiandika WOTE tutaainisha nini maana ya Tume huru ya uchaguzi na inapatikanaje? wenzetu walio kwenye demokrasia zilizoendelea ( za miaka mingi) tume hizi zinaongozwa na watu wasiojitambulisha na chama chochote cha siasa ili wawe kweli huru na ushawishi wa siasa za vyama!!! Si vibaya sisi tukaiga hilo..
:flypig:
No comment on this let me run away
Kimunya au kivuitu?Hongera Jaji(Mst) Lubuva!
Nafasi hii ni changamoto kubwa sana kwa miaka hii, na unahitaji kuchezea kwenye fair playground, vinginevyo utakuwa KIMUNYA wa Kenya!
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENTS OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Aidha, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.
Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu, 2011.
Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.
Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. **Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.
Imetolewa na:
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22 Desemba, 2011
Hivi sifa mojawapo ya kushika hizi nafasi ni kuwa mstaafu, mm naona mtu akiwa mstaafu anaweza kutumiwa kirahisi kwa kuwa hana cha kupoteza. Hii bado ni tume ya uchaguzi ya CCM.
Kenya baada ya katiba mpya wazee kama hawa ni nadra kupata nafasi. Hakuna uteuzi unaofanywa na rais direct. Usaili unafanyika na rais anapewa jina au majina ya watu waliofanya vizuri ndipo anateua na hata akiteua hawana kazi mpaka wapitishwe na bunge. Katiba mpya ni dawa ya matatizo. Kenya itapaa kama watampata mrithi wa Kibaki aliye na msimamo. Wakijroga kuchagua wezi kama Uhuru Kenyata na kumwacha Kamanda aliyewapeleka hapo kwa kukokota mkokoteni unaoitwa Kenya yaani Raila watarudi nyuma enzi za Moi.Wazee kama hawa wangetakiwa kupumzika kuwapa majukum magumu kama haya ni hasara kwao,aliyewateua,na taifa kwa ujumla coz efficient will be zero.
Hongera Jaji(Mst) Lubuva!
Nafasi hii ni changamoto kubwa sana kwa miaka hii, na unahitaji kuchezea kwenye fair playground, vinginevyo utakuwa KIMUNYA wa Kenya!