Lubuva Mwenyekiti mpya Tume ya Uchaguzi!

Muhimu hapa ni kupunguza mamlaka ya mkuu wa nchi kuteua na kustaafisha anapojisikia, hizo nafasi zinapaswa either kutangazwa na watu wengi kujitokeza au kuteuliwa na kuthibitishwa na chombo maalum kama bunge lenye uwakilishi wa wananchi..
 
nani huyo kapewa
katiba itabadilishwa na tume ya uchaguzi itakuwa na viongozi kutoka kila chama
huyo alowekwa atakua pambo tu la kutupwa ktk moto wa mageuzi ya nchi
soon we will have our new constitution,
 
Hata kama angekuwa hajaoa katika familia ya mke wa Lowasa, ili aweze kuteuliwa kushika nafasi hiyo, lazima atakuwa na mafungamano na mkuu wa nchi kwa namna nyengine.
Kwa hali ya siasa za sasahivi ndani ya ccm, sidhani kama kikwete anaweza kumteua mtu mwenye ukaribu wa aina yoyote na Lowasa.

kWANI UMETHIBITISHA KUWA HAWA JAMAA NI MAADUI? JAMAA HAWA WANAJUA KUCHEZA NA AKILI ZA WATATNZANIA, WANAIBUA BIFU KATI YAO HALAFU NO FA BALI KUJENGEANA MAZINGIRA YA KULINDANA TU

 
Sina shaka na utendaji wake ila sijui changamoto zilizopo kama anaweza kuungwa mkono ili atende haki kimsingi mheshimiwa sana lubuva ni mwadilifu na mchapa kazi
namshauri mhe, huyu akiona mizengwe aachie ngazi kulinda heshima yake
 
lakini hongeara sana mhe . lubuva na pia mhe, rais kwa kumuona ila muacheni afanye kazi kwa uhuru wa kutosha binafsi nimefurahishwa sana
 
Nijuavyo mimi Lubuva ana undugu na mke wa lowasa aidha kaoa ktk ukoo wa mke wa lowasa nijuavyo ni jamaa yao


Mshikaji umepatia mwanzo mwisho.......maandalizi ya kumtangaza rais mwaka 2015 ndiyo yameanza.....lazima watu kuangalia beyond huu uteuzi.
 
Tunahitaji nafasi hizi ziwe zina ombwa, ili kupata watu makini na kuwa "fair" kwa watu wote. Utaratibu huu kamwe si wa kujenga demokrasia
 
Hiyo chupa tu ndio imebadilika,
But mvinyo ni uleule wa mwanzo!!
Tunahitaji mabadiliko ya katiba ili kila chama chenye wabunge kitoe wawakilishi kwenye tume yao
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Aidha, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011.

Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.

Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu, 2011.

Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.

Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. **Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.

Imetolewa na:

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

22 Desemba, 2011
Na huyu naye mkataba wake wa ajira ya umma unaisha lini?
 
Sijui ina maana gani kwa kweli - ni kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya au ni kupokezekana kwa sababu ya kupokezana. Sina sababu ya kumpongeza bali namtakia pole kwa kuingia kwenye ukuti ukuti wa CCM. Zamu yake tu "kuingia upepo". Akitenda haki atapongezwa so far. Nasema karibu.

Mwanakijiji hii nafasi siyo ya kutenda haki ni nafasi ya kulinda masilahi ya CCM. Unafanya kazi under GP especially kwenye uchaguzi mkuu. Kazi yako wewe si kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki bali kazi yako ni kumtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi kwa vile utakavyoamrishwa na TISS.

Binafsi sifurahii uteuzi huu hata kama angeteuliwa Tundu lissu kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Kwa kuwa tunaelekea kwenye kutafuta katiba mpya, teuzi kama hizi zingeendelea kukaimiwa mpaka ikapatikana katiba mpya itakayokuwa na maelezo ya jinsi ya kuwapata watu kama hawa ambao ni muhimu kwa demokrasia na ni msingi wa madai ya katika mpya.

Ajiandae kwa worse katika kipindi hiki, amekalia kuti kavu. Vurugu zozote zile zitakazosababishwa na uchaguzi mtuhumiwa wa kwanza The hague atakuwa yeye. Ninaamini Makame sasa hivi ana enjoy kustaafu baada ya kutumika bila kupatikana kwa maafa ya uchaguzi.
 
kWANI UMETHIBITISHA KUWA HAWA JAMAA NI MAADUI? JAMAA HAWA WANAJUA KUCHEZA NA AKILI ZA WATATNZANIA, WANAIBUA BIFU KATI YAO HALAFU NO FA BALI KUJENGEANA MAZINGIRA YA KULINDANA TU


Pamoja na usanii wa JK, sidhani kama ataruhusu EL achukue uongozi wa nchi hii. Angalia vizuri jinsi maji yanavyochemka ndani ya ccm utagundua kwamba pamoja na madai ya EL kwamba hawakukutana barabarani, hawezi kumpa favor ya kuwa raisi, na ikitokea EL amesimamishwa na ccm kugombea uraisi, basi ujue ni kwa mbinu zake mwenyewe.
 
Hongera Jaji(Mst) Lubuva!
Nafasi hii ni changamoto kubwa sana kwa miaka hii, na unahitaji kuchezea kwenye fair playground, vinginevyo utakuwa KIMUNYA wa Kenya!

Rekodi ya Mh. Lubuva ni nzuri kwenye judiciary (soma hukumu zake kutoka TLRs), lakini hii post ya kisiasa, itamuaribia reputation yake!!! Hapa hakuna uanasheria ni uanaKikwete au uanaCCM- no professionalism!!!!
 
Back
Top Bottom