Lubuva Mwenyekiti mpya Tume ya Uchaguzi!

Kwa kweli, kazi hiyo siyo ndogo ya kukabidhi nchi kwa chama kisichozoeleka. He has to be humble to roll up his sleeve for this taunting task.

Hivyo unaona ni sahihi kumteua kwa kuwa ni mwanachama wa chama kilichozoeleka! Hapo ndipo unapokosea; mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ndiye refa wa uchaguzi, akisema huyu kashinda hakuna wa kuuliza wala kukata rufaa mahakamani, sasa kama mwanaccm anataeuliwa kwa uccm wake atatoaje haki kwa cuf? - Tafakari, mnaipeleka nchi pabaya!
 
Lubuva na Kivuitu wamesoma darasa moja. Ndo wanafunzi wa kwanza wa UDSM walioanza mwaka 1961. Imekula kwenu
 
Hongera Jaji(Mst) Lubuva!
Nafasi hii ni changamoto kubwa sana kwa miaka hii, na unahitaji kuchezea kwenye fair playground, vinginevyo utakuwa KIMUNYA wa Kenya!
yule alienda kutangaza matokeo amejificha studio za kbc alikuwa anaitwa kiviutu ila niliwahi kumuona citizen tv kachoka analalamika wameshamsahau yupo kijijini.mwai kibaki akaapishwa haraka haraka

 
Natumaini Hili ni suala la muda,kwenye mchakato wa katiba mpya suala la tume huru ya uchaguzi halikwepeki
 
Yule wa Zamani kafukuzwa kwa sababu Chama Cha Makahaba kilipoteza viti vingi vya Ubunge na udiwani kama sio Usalama wa taifa kuwasaidia NEC kuhesabu kura hata Kikwete asingekuwa magogoni.
tunajua ulipenda sana padre wako awe pale lakini haikuwezekana kwani wengine hatukumpa kura zetu sasa we endelea kulalama.
 
roho onaniuma sana kwani jk kamuingiza mzee wangu kwenye matatizo makubwa

This is not good fo Judge Lubuva, ni sawa na kupewa kazi ya kuzobua vyoo baada ya kufanya kazi miaka mingi jikoni
 
tunasubiri katiba mpya huyu atatupwa ktk kapu la mageuzi
iWEJE hii tume iONGOZWE na vikongwe AU kwa vile hawana jipya?
ktk katiba mpya wananchi ndio wataamua nani awe mwenyekiti nani awe makamu na lazima iwe na wajumbe wa vyama vyote
sijaelewa mantiki ya kj kuteuwa sasa wkt anajua tangu zamani hii tume ni ya chama kimoja
au ndio keshakalia mchakato wa katiba mpya,kusaini kwaken ni danganya toto lazima kieleweke tunataka nchi mpya,katiba mpya na sio uongozi wa kupeana na hata wazee waliochoka kutoa hukumu unampa kazi kubwa kama hii.na mashaka na ufikiri wa JK,
 
Watu tunazaliwa majina hayo, karibia tunazeeka ni yale yale, halafu hii ndo demokrasia, kuna tofauti gani na tawala za kiimla ama za kifalme? aargh, only in banana republic.
 
Natumaini Hili ni suala la muda,kwenye mchakato wa katiba mpya suala la tume huru ya uchaguzi halikwepeki
Ben, muda wenyewe ni muda gani?

Kwanza alikuwa na haja gani ya kuwabadilisha kama ni kweli katiba inabadilishwa karibuni?

Whats the emergency?

Hii michezo hii, mhn!
 
Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.



Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. **Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.
Mbona wateule wote hawa wana walakini huko walikokuwa? Viongozi wa nchi hii maadlili yao yanatia shaka, alifanya nini katika hilo?

Huyu naye Mallaba, Mikataba mingi ya nchi hii ni ya kifisadifisadi, yeye kweli ni salama katika habari za ufisadi? Yangu macho!
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Imetolewa na:

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

22 Desemba, 2011

Huyo ndiye alikuwa anaipitia mikataba yote ya serikali kitaalamu! Waziri ni mwanasiasa, katibu mkuu anaongoza taaluma zote ndani ya wizara, mkurugenzi wa idara ndiye hasa mtaalamu wa sehemu husika. Katika hali hiyo huyu bwana ndiye mtaalamu wa masuala yote ya mikataba ya serikali - richmond!
Mnategemea nini kutoka kwa mtu huyu, si lazima ahakikishe hao aliohusika kupitisha mikataba yao ndio wanaendelea kushika uongozi wa nchi?
 
Kila post wanapewa "wastaafu"...ina maana hakuna watu wengine wanaoweza kuongoza vyombo/taasisi hizi? Hii tabia ya kuendelea kuwapa majukumu "wastaafu" inabidi ipigiwe kelele kwani haina tija zaidi ya kulindana. Unategemea hawa "wastaafu" wanaopewa fadhila wasimamie haki? Ndo maana kuna haja ya kuwa na katiba mpya ili majukumu ya uteuzi yasiwe kwa mtu mmoja manake hii inahalalisha hoja ya "amlipaye mpiga zunmari ndo huchagua wimbo".
 
hursday, December 22, 2011

Jaji Damian Lubuva Mwenyekiti mpya Tume ya Taifa ya Uchaguzi




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Aidha, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi. Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011. Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi. Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu, 2011. Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu. Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. **Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.

Imetolewa na: Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM. 22 Desemba, 2011


cleardot.gif





 
Wazee kama hawa wangetakiwa kupumzika kuwapa majukum magumu kama haya ni hasara kwao,aliyewateua,na taifa kwa ujumla coz efficient will be zero.
 
I have nothing against the esteemed and experienced Justice Lubuva.

But I have a problem with the system that let the president choose the National Election Commission.

Ni kama timu moja inachagua refa, ukisema mchezo hauko fair utalaumiwa?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom