Lubuva Mwenyekiti mpya Tume ya Uchaguzi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lubuva Mwenyekiti mpya Tume ya Uchaguzi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Dec 22, 2011.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone: 255-22-2114512, 2116539
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENTÂ’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  Aidha, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.

  Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011.

  Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.

  Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu, 2011.

  Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.

  Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. **Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.

  Imetolewa na:

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  22 Desemba, 2011
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,233
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hongera Jaji(Mst) Lubuva!
  Nafasi hii ni changamoto kubwa sana kwa miaka hii, na unahitaji kuchezea kwenye fair playground, vinginevyo utakuwa KIMUNYA wa Kenya!
   
 3. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sarakasi kuelekea katiba mpya zimeshaanza!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 30,761
  Likes Received: 4,132
  Trophy Points: 280
  Sijui ina maana gani kwa kweli - ni kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya au ni kupokezekana kwa sababu ya kupokezana. Sina sababu ya kumpongeza bali namtakia pole kwa kuingia kwenye ukuti ukuti wa CCM. Zamu yake tu "kuingia upepo". Akitenda haki atapongezwa so far. Nasema karibu.
   
 5. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,319
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Uadilifu wao ndo hoja yangu? Hongereni kupata nafasi.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 19,493
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  hakuna jipya yote haya majizi tu bana ...yaani hapo yatakuwa busy kusoma excell jinsi ya kumanipulate matokeo ...aaaagh
   
 7. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,042
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Huyu Lubuva aliwahi kuwa waziri wa sheria na mwanasheria mkuu kama sijakosea.Wacha tusubiri kama watakuja na jipya.
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Dereva mpya, ki-fodi cha zamani bado kuna matumaini yoyote ya mwendo na safari salama hapo 2015 tofauti na yale yale ya Makame?

  Wannchi wala hatukuomba kitu chochote jirani na Dereva Mpya isipokua 'Gari Jipya' chaguo la wananchi wenyewe bila kuzongwa na mtu.

  Ukishangaa ya Makame utaona ya Kivuitu uchaguzi ujao.
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,725
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ni wale wale... Hakuna jipya hapo.
   
 10. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,721
  Likes Received: 782
  Trophy Points: 280
  hii ni nini tena,kwani huyu mwenyekiti wa ccm bado anaendelea kuchagua wana ccm wenzake kwenye tume ya uchaguzi?mbona sielewi hii jamani?????
   
 11. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Hivi mimi Fairplayer siiwezi hiyo kazi au lazima hizo kazi wapewe WASTAAFU!

  Mimi nina miaka 45, ukinipa kazi hiyo mwenye miaka 40 anasogea kwangu na mwenye miaka 36 anasogea kwenye kazi ya mwenye miaka 40 na mwenye miaka 30 anasogelea kazi ya aliepanda ..inaenda mpaka FRESH GRADUATE naye anapata kazi.

  Au mie naona vibaya wananchi?
   
 12. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,106
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli mh. Rais hatumii busara hata kidogo kwenye hizi teuzi zake, mtu ambaye alikuwa na jukumu la kuhakikisha viongozi wa umma wanakuwa na maadili, licha ya kuonyesha kushindwa kwa 100% leo hii anateuliwa kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, au ndio malipo ya kuwalinda viongozi wezi wa mali za umma.
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,150
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Umefika wakati kazi zote ziwe zinatangazwa na watu wawajibike kuomba.

  Tunajuaje kuwa Huyo aliyeomba ni bora kuliko watanzania wingine.
   
 14. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 28,608
  Likes Received: 3,725
  Trophy Points: 280
  Lubuva alizimia wakati ue Rais Mwinyi alipowaambia mawaziri wote wajiuzulu....Any way nafasi hizi zimekuwa wazi kwa muda sasa na ninadhai Mh amenusa chaguzi ndogo za Arumeru Mashariki , Kigoma Kusini na ..........(Maswa!!!???)
   
 15. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,853
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kateuliwa na mh rais,hata siku moja hataacha kuwa mtii kwake kwa lolote hata lenye maslahi kwa umma maadamu linakinzana na maslahi ya aliyemteua. wiski mpya kwa glass ya zamani
   
 16. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sitoi hongera kwa kuteuliwa, Nawapo pole kwa kuteuliwa kupambana na changamoto za kutoa haki kwa washindi halali au kuwachakachua, na mkichakachua 2015 dhambi ya damu isiyo na hatia itakuuwa juu yenu
   
 17. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,042
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Wawi je??????
   
 18. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,339
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Yule wa Zamani kafukuzwa kwa sababu Chama Cha Makahaba kilipoteza viti vingi vya Ubunge na udiwani kama sio Usalama wa taifa kuwasaidia NEC kuhesabu kura hata Kikwete asingekuwa magogoni.
   
 19. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 487
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ujinga uleule unaendelea"Divai mpya ktk viliba vya zamani" ila hongereni kwa kupata ulaji.
   
 20. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,269
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwakweli mwenye nacho anaendelea kuongezewa! Ila sioni kama kuna tofauti
   
Loading...