Lubuva Mwenyekiti mpya Tume ya Uchaguzi!

Rais asiyekuwa na huruma na wananchi wake wa Dar kuhusu mafuriko anaendeleza sarakasi zake za kutowajali wananchi
 
Nilidhani nafasi hiyo ingeachwa wazi mpaka tume mpya huru ya uchaguzi itakapokuwa imepatikana...
 
Hivi hii post ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kigezo ni lazima uwe mstaafu au??? Walioweka retirement age walikuwa na akili sasa sijui hawa jamaa wanafikiria nini?? Ndiyo maana hata bible inasema umri wa binadamu ni miaka 70. Sasa wao wanataka wafanye kazi mpaka wafe wakiwa kazini??? Waende wakalee wajukuu!!
 
Sijui ina maana gani kwa kweli - ni kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya au ni kupokezekana kwa sababu ya kupokezana. Sina sababu ya kumpongeza bali namtakia pole kwa kuingia kwenye ukuti ukuti wa CCM. Zamu yake tu "kuingia upepo". Akitenda haki atapongezwa so far. Nasema karibu.

kwa mwenendo huu hakuna cha katiba mpya wala nini
 
kwa nini wastaaafu?? Si wangeachwa wapumzike! Kwani hakuna vijana wa kitanzania wabobeaji wa fani hizo?? Hii kazi inatakiwa itangazwe watu wawe lively interviewed publicly ktk televishen na kuwe na kamisheni itakayowachija na waidhinishwe na bunge Katiba mpya inatakiwa iconsider hiyo
 
Hongera mheshimiwa. Usikubali kuburuzwa katika maamuzi yako. Kinachotakiwa ni haki kwa wote ccm ikishinda kwa haki ipewe ushindi na upinzani ukishinda kwa haki wapewe. Kipimo chako ni jimbo la kigoma kusini kama litatangazwa wazi.
 
Wadau Jaji Lewis Makame na Rajavu Kiravu wamerithiwa na Jaji Daminia Lubuva na Benedicto Mallaba. Taarifa ya ikulu hii hapa:

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
*
Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
*


*
PRESIDENTS OFFICE,
***** THE STATE HOUSE,
****** P.O. BOX 9120,**
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
*
*
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
*
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
*
Aidha, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bwana Julius Benedicto Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
*
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011.
*
Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi.
*
Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu, 2011.
*
*
Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.
*
Naye Bw. Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. **Bw. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.
*
Imetolewa na:
*
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
*
22 Desemba, 2011
 
Hizi ni ajira ambazo watanzania tumezipoteza tena: kwanini wasitaafu ndo wanapewa hizo nafasi ilhali bado kuna wasio na kazi na wanazitafuta kwa udi na uvumba?
 
Jamani hivi huyu Lubuva ana umri gani???? Hakuna wa 50s?? Atakuwa na kipya lipi??? Pole zetu duh
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Nafikiri hii sio tume ya taifa ya uchaguzi, bali tume ya yule anaye wateua wanayoiunda!

Hakuna jipya, hatutegemei jipya toka huyu mteule na tume yake.

Hongera
 
Hiki kitu ndicho kimeleta mgogoro kuhusu mchakato wa katiba. Rais kuwa na madaraka jumuishi, Umefika wkt tukubaliane kuwa uteuzi wa watu/viongozi wa taasisi za uma kuwekewa utaratibu maalum wa kuwapata. Hali hii ndiyo inayoleta uswahiba usioisha serikalini na madhara ya uswahiba ni kushuka kwa uwajibikaji na kupotea kwa maadili.

Jk nitamkumbuka kwa kuteua watendaji a taasisi mbalimbali na kupandisha watu vyeo hasa wastaafu kupewa ulaji.
 
Tunatakiwa kusema kwa pamoja kuwa wastaafu wapatiwe fursa hizi pale tu inapotokea hakuna watu/vijana wenye nguvu wanaoweza kufanya hizo kazi. Tubadilike inakera sana! Someni alama za nyakati.
 
Sijui ina maana gani kwa kweli - ni kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya au ni kupokezekana kwa sababu ya kupokezana. Sina sababu ya kumpongeza bali namtakia pole kwa kuingia kwenye ukuti ukuti wa CCM. Zamu yake tu "kuingia upepo". Akitenda haki atapongezwa so far. Nasema karibu.
Kwa kweli, kazi hiyo siyo ndogo ya kukabidhi nchi kwa chama kisichozoeleka. He has to be humble to roll up his sleeve for this taunting task.
 
Jamani hapa mbona kama kuna Changa la Macho?? Ni formula Gani inatumika kuwateua hawa viongozi hasa wa Tume ya Uchaguzi?? Mizee imeshastaafu walikukowa wanafanya kazi sasa wanateuliwa kuwa Tume ya Uchaguzi...HIVI HAKUNA WALIO WACHAPA KAZI DAMU MOTO MPAKA IONGOZWE NA WAZEE?? Wenye miaka 40 kuendelea wakiwekwa watakuwa na Madhara Gani kwa Tume? People let us think this twice...I am creating new Topic now.
 
Mimi hii nchi huwa inanishangaza sana, post mhimu kama hii anapewa mstaafu. Sasa kuna haja gani ya kuwa na wastaafu. Kwa uelewa wangu mtu anastaafu baada ya uwezo wake wa kiutendaji kushuka na kwamba kwa umri wake hawazi kutoa mawazo au kugundua vitu vipya vya manufaa kwa taifa au kampuni au shirika analolifanyia kazi. Sasa niyaje mtu huyu aliyechoka kifikira na kiutendaji apewe nafasi nyeti kama hii? Na hapo tunalia nchi haina ajira? Badala ya kuwapa nafasi waliopo kazini ili watengeneze vacancy za vijana fresh from school tunawapa nafasi wazee waliochoka, wamekula wameshiba, bado tu wana tamaa ya kuendelea kula tu. Huu ni upuuzi kabisa.
 
Back
Top Bottom