Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

Vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotakiwa wajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi wamekutana na uongozi wa juu wa chama chao, na taarifa zinasema bado mvutano haujaisha kati ya pande mbili hizo. Taarifa za hakika zimeliarifu Raia mwema kwamba walikutana na makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa, wiki iliyopita, na kwamba mmoja wao, Edward Lowassa, Bado ana donge.
Habari zinaeleza kwamba Lowassa (Mbunge wa Monduli), Rostam Aziz(Mbunge wa Igunga) na Andrew Chenge (Mbunge wa Bariadi magharibi) waliitwa ofisi ndogo ya CCM, Lumumba Dar es Salaam wakitakiwa kutekeleza uamuzi wa NEC.
Lakini habari kutoka kwa watu wa karibu na Lowassa zinaeleza kwamba mwanasiasa huyo amebainisha kwamba hakubaliani na uamuzi wa NEC. “Mzee (Lowassa) amesema kwamba aliitwa na kwamba alitakiwa kuachana na suala la urais ili mambo yaishe, lakini amewaambia uamuzi wowote kisiasa ni haki yake kikatiba, na hivyo hakubaliani nao” anasema Mbunge mmoja ambaye yuko katika kambi ya Lowassa akiongeza: “Ila wajue kwamba wao wakimwaga mboga sisi tunamwaga ugali”. Kwa mujibu wa Mbunge huyo, Rostam Aziz na Chenge wanaonekana kulegeza kamba katika suala hilo.
Anasema mbunge huyo “Rostam amesema wazi kwamba hawezi kushindana na Rais aliye madarakani hata kama watakuwa wameonewa. Chenge anakubali tu kwasababu anaona hana jinsi. Lowassa bado moyo wake ni mzito”…………………………………………………………………………………………………….Gazeti lilipotaka Lowassa alizungumzie suala hilo alijibu “No coment, No coment, No coment”

Taarifa ambazo Raia mwema limezipata zinaeleza kuwa tayari viongozi hao ambao wote ni wajumbe wa NEC na walihudhuria kikao kilichoazimia wajiuzuru, wameshakabidhiwa barua rasmi za kuwataka wajiuzuru zikirejea uamuzi wa vikao vya juu vya CCM.


Source: Raia Mwema June1-June7, 2011

Mene mene tekele na peresi CCM na serikali yake. Wenye akili anzeni kukimbia kwenye hilo gofu litaungua siku si nyingi. Sasa Bwana Mungu yuko vitani kukomboa maskini wa TZ kutoka kwenye mdomo wa Joka CCM.
 
Wakiweka, hutanunua hard copy mitaani na ofisi zao zitafungwa hivyo itakuwa ngumu wewe kupata hata hiki kisehemu cha habari zao.

Asante Ezan, tuko mbali sana na upeo wa hard copy ndo maana tegemeo ni mtandaoni tu
 
lowassa unatishia nyau! tumeyazoea maneno yako ya kila siku. kama vipi na iwe vipi lowassa. tatizo ni urais ndo unakuhumiza bichwa lako. kwan lazima uwe rais? ubunge wa monduli si unakutosha? kama umeshatolewa sadaka bila wewe kujua tulia tu bro. ndo mambo ya siasa yanakupanda na kushuka. wewe ndo umeshashuka ivyo hauwezi panda tena bro!
 
Mwanahalisi la leo limembeba Lowassa katika aspect gani?

Ukisoma kwa utulivu mkubwa na umakini'MAFISADI CCM WAGEUKA MBOGO"unagundua moja kwa moja aliyetoa siri za kikao ni lowasa, kwa sababu mukama,msekwa awawezi kufanya hivyo,na hicho kikao kilikuwa cha watu 5 nadhani.Kitu kingine kunakulipizana visasi hapa kama umesoma na kugundua,maana wamezungumziwa lowasa,chenge na RA.kama kawaida mwishoni wakagusia kuhusu waanzilishi wa ccj mwakyembe na sitta,Lowasa nataka kuondoka na wengi akiwemo mwakyembe na sitta.
 
Yanayo mkuta Kikwete ni kwamba anaandamwa kwasababu ya dini yake, yanayomkuta Lowasa ni haki yake lazima asurubiwe.
we ezan nikutukane ? kama kweliunamaanisha hivi wewe akili yako iko matakoni. kama hujamaanisha basi haya nmatusi hajakustahili wewe.
ngoja nikuulize yale yakiyotokea misri ni kwa sababu mubarak ni mwislam au ni mkristo?au wale wanaoandamana kule bengazi wote ni wakristo?
usiongee kama vile umekalia gunzi
 
Hiiii sinema inayo endelea kwa ccm ni kali sana yaani kama picha la kihindi.
 
Lowasa mwacheni na amwage Mboga tu! sindiyo mwisho mwisho wao huu asipomwaga leo hata mwaga tena atamwaga akiwa gerezani
 
Mimi nadhani Lowassa kama Mwanasiasa mkongwe alitakiwa a-step down tu, kwasababu system haimtaki tena kwasababu kaichafua. sasa akimwaga ugali yeye itamsaidia nini? afanye kitu ambacho kitamfanya arudishe heshma yake na siyo kuwa na "moyo wa tukose wote"


mheshimiwa Lowassa kwa kweli amekuwa victimized. Kama akifuatilia sakata la Richmond, ni wangapi walitakiwa wachuliwe maamuzi ya kinidhamu, na hata kupelekwa mahakamani lakini hawajatendwa hivyo. Hio ilikua ni long project kwa ajili ya urais 2010.
Kila kiongozi ana kashfa tena nzito sana, na lowassa anayajua hayo. Kama Watanzania mkimtumia vizuri Lowassa, upo uwezekano mkubwa kwa serikali hii kutofika 2015. Ana sababu za msingi kutokubaliana na haya maamuzi kwa sababu hakuna chombo chochote cha serikali kilichomshuhudia kuwa ni mchafu sana, na vile vile hajapata nafasi ya kujisafisha.

Lowasa is a real great threat kwa watawala cause can do anything, na akawaangusha. Hata chadema inajua hili.

Kama mnabisha mpeni nafasi


CCM kama mpo makini, shughulikieni na hawa waanzilishi wa CCJ.
 
we ezan nikutukane ? kama kweliunamaanisha hivi wewe akili yako iko matakoni. kama hujamaanisha basi haya nmatusi hajakustahili wewe.
ngoja nikuulize yale yakiyotokea misri ni kwa sababu mubarak ni mwislam au ni mkristo?au wale wanaoandamana kule bengazi wote ni wakristo?
usiongee kama vile umekalia gunzi

Duh! Basi Mkuu.....!
 
End of CCM is arround the corner, Jamaa kashindwa kabisa kumanage nchi na chama, mwalimu aliyaona haya toka kwa hawa boyz 11 men they are still boys.
 
Lowasa mkuu usikubali hata siku moja kutoka hapo,
wewe waziri mkuu mstaafu ufukuzwe kizembe hivyo,
Kwanza lichama lenyewe limekufa hili!
 
Tungekuwa kwenye nchi za wenzetu, haya yanayotokea sasa tungekuwa tumesha yasahau siku nyingi.

1. tuhuma za ufisadi - watu wangekuwa wamesha fikishwa mahakamani siku nyingi,
2. kiongozi kushindwa kuongoza - vote of no confidence siku nyingi,
3. matumizi mabaya ya ofisi ( hata kama ni tuhuma tu) - huna kazi

Ndio maana wenzetu wanaendelea na kutuacha tumesimama. Watanzania tunasubiri nini?
 
Mimi nasema hiviiiiiiiiiiii, wote JK,EL ,RA,AC na wengineo mahali wanapostahilikuwa sasa hivi ni JELA.
 
Lowassa usithubutu kusema lolote.Ukifanya hivyo,nasema ulivyoniambia kuwa......................jaribu uone.
 
Lowassa ana qualities zote za kuwa CCM, kama JK ni mwanaume wa shoka ajaribu kumwondoa tujionee vituko.
 
Yanayo mkuta Kikwete ni kwamba anaandamwa kwasababu ya dini yake, yanayomkuta Lowasa ni haki yake lazima asurubiwe.

EWE MWANA WA MTU jizamishe maneno yaliyo fichwa.
Siku nyingi zimepita juu yako ukiwa unajishughulisha na mawazo yako na fikira za upuzi. kwa muda gani utaendeleya kusinzia katika kitanda cha ujinga inua kicwa chako toka usingizini kwa maana jua limechomoza na kupanda hadi kichwani kwa fulaha huenda likakuangazia nuru ya uzuri
 
Back
Top Bottom