Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

Mimi nadhani Lowassa kama Mwanasiasa mkongwe alitakiwa a-step down tu, kwasababu system haimtaki tena kwasababu kaichafua. sasa akimwaga ugali yeye itamsaidia nini? afanye kitu ambacho kitamfanya arudishe heshma yake na siyo kuwa na "moyo wa tukose wote"

mikataba fek,jino kwa jino wakimwaga mboga lowasa mwaga ugali BWAH BWAH MADENGO NTIMA
 
Edward Ngoyai Lowassa, Baba Fred kweli mbishi, kama hukuwa peke yalo kwenye deal basi lazima muondoke wote
 
sasa atamwaga lini mbona na yeye anatishia tu?? si afanye sasa? haoni kuwa huu ndio muda muafaka kwake na kwa familia yake na kwa jamii kama kweli anaipenda???
 
Wananchi Kikwete anawachezea akili wanachama wa ccm; haiwezekani kabisa kumtosa Lowassa na yeye akapona!! Hii yote wanayofanya ni mchezo wa kuigiza, Kikwete na Lowassa kama ni pete na chanda na ndio maana hata hapa juzi wake zao walikuwa pamoja kwenye sherehe za kampuni yao ya WAMA!!
 
Huyu anatishia nyau! Hana lolote...! Mimi nahesabu siku, zimebaki nane. Nataka nione akimwaga hiyo mboga. Ccm wamejichokea na hapo walipo ni zaidi ya ICU, hawajui la kufanya, wanachokifanya ni kutujaribu mwitikio wetu. Hata huyo aliyesema hivyo nae atakuwa katumwa kupima kina cha maji! Kwa taarifa yake ni kwamba, tunazihesabu siku zao za kuongoza maana ni chache kama umri wa inzi!
 
Mwanangu Lowassa komaa nao tuu hao. Wao wanataka Membe apite 2015 kama anaenda uani kuwania uraisi.. Komaaa nao mpaka kieleweke.. Kama kujivua gamba basi hata aliyetumia hela za EPA kwenye uchaguzi mkuu 2005 zaidi bilion 30 aanze yeye wengine mfwatie. JK lazima awe KILONGOLA katika hili
 
Anacho kifanya sasa Lowasa ni kumchanganya Jk kwa kila mbinu chafu,kwa hiyo jk anatakiwa kuwa makini sana,na anatumia mwanahalisi kufikisha ujumbe kwa JK,Kwa mfano aangalia maneno haya kutoka kwenye gazeti la mwanahalisi lenye kichwa cha habari "MAFISADI CCM WAGEUKA MBOGO"kuna baadhi ya mambo ambayo serikali ya JK aizungumzii sana ni swala la kagoda.kAGODA ni moja ya ishu ambayo ilitumika kumuingiza jk madarakani na JK nahusika na hii ishuu kwa upande mmoja au mwingine.SASA nije kwenye nukuu kutoka mwanahalisi "Kampuni ya kagoda ni miongoni mwa makampuni 22 yaliyothibitika kuchota mabilioni ya shilingi kwenye akaunti ya madeni ya nje(EPA) ndani ya benk kuu ya tanzania(BOT).Gazeti hili limeshindwa kufahamu mara moja kilichosababisha msekwa na wenzake kushindwa kumweleza rostam ushiriki wake katika kagoda.Hata hivyo kwa zaidi ya miaka minne sasa ccm imekuwa ikituhumiwa kunufaika na fedha za EPA hasa sh.40 bilionizilizoibwa na kagoda"mwisho wa kunukuu kutoka mwanahalisi
HAPA KUNA MCHEZO UNATAKA KUCHEZWA AU NDIO UNAENDELEA KUCHEZWA BILA BAADHI YA WATU MAKINI KUJUWA KINACHO ENDELEA,ILI KUNYAMAZISHA SWALA ZIMA LA UVUAJI GAMBA.
 
Hakuna mahala nilipoandika didi, thibitisha

Acha ligi kijana..umeazimia kuandika dini..umeandika didi..mwingine anaweza asikuelewe....Hakuna anayemwandama JK kwa dini yake..haya ni maneno ya kupotosha ama kuukwepa ukweli...JK ameshindwa kuongoza nchi hii iko wazi hata ukuiwauliza watoto wa darasa lasaba wanaojitambua watakueleza...Mwinyi alikuwa raisi Tanzania nani alimuandama kwa dini yake?? embu tumia akili yako katika kuchanganua mambo sio ku copy and paste kila propaganda chafu zinazoenezwa na Magamba...Tanzania hatuchagui rais kwa dini na ndio maana 2005 alishinda kwa asilimia 85% je hii ilikuwa ni wa dini moja wamemchagua..kati ya hiyo 85% leo haifiki hata 40% watu wamechoshwa na uongozi mbaya wa Magamba na uoga na uvumilivu wa watanzania ndio sababu mpaka leo 2011..Magamba yanatawala.....Amka kijana!!
 
Wananchi Kikwete anawachezea akili wanachama wa ccm; haiwezekani kabisa kumtosa Lowassa na yeye akapona!! Hii yote wanayofanya ni mchezo wa kuigiza, Kikwete na Lowassa kama ni pete na chanda na ndio maana hata hapa juzi wake zao walikuwa pamoja kwenye sherehe za kampuni yao ya WAMA!!

kimjin mjin
 
Na huko ndiko tunako elekea,lowasa anafanya kila njia ili kuweza kumuaribia JK hasa kitika serikali yake,ndio maana kwa sasa Lowasa ana mtumia sana kubenea ili kuweza kuwaharibia wakina sitta na mwakyembe ili tu aweze kuyumbisha serikali ya jk.Na kwa hili atafanikiwa tu maana inaonekana amejipanga,hata ukisoma mwanahalisi ya leo kuna kitu unaweza gundua,Mwanahalisi wanachokifanya kwa sasa ni kuwapiga Mwakyembe na Sitta kwa ishu ya CCJ toleo lililopita na toleo la wiki hii mada nyingi ni zile zile.Wanaanza kwa kuwapiga mapacha watatu kidogo halafu wanahamia kwa Sitta na mwakyembe na hili ndio dhumuni la mwanahalisi kwa sasa.

Lowasa atamuharibiaje JK ? kwani nani ni raisi wa nchi hii. JK ni dhaifu ndio na hiyo ndo loophole anayotumia Lowasa. Angekuwa Lowasa ndo Rais na JK ndo PM mambo yangekuwa tofauti. Lowansa anagetumia madaraka yake yote kufanya chochote kwenda na rythm ya public.

Ndio maana japo simubali sana JK naona ana uvumilivu sijui upole sijui ni umbayuwayu wa ajabu ambao hauna hata cehmbe ya maslahi kwa taifa.
 
Ni faida kwa wapinzani amwage tu huo ugali

mimi nadhani lowassa kama mwanasiasa mkongwe alitakiwa a-step down tu, kwasababu system haimtaki tena kwasababu kaichafua. Sasa akimwaga ugali yeye itamsaidia nini? Afanye kitu ambacho kitamfanya arudishe heshma yake na siyo kuwa na "moyo wa tukose wote"
 
Mwanangu Lowassa komaa nao tuu hao. Wao wanataka Membe apite 2015 kama anaenda uani kuwania uraisi.. Komaaa nao mpaka kieleweke.. Kama kujivua gamba basi hata aliyetumia hela za EPA kwenye uchaguzi mkuu 2005 zaidi bilion 30 aanze yeye wengine mfwatie. JK lazima awe KILONGOLA katika hili

Mkuu chaguo la Kikwete si Membe hata siku moja.Chaguo la Kikwete ni Dr Hussein Mwinyi utakuja kuniambia siku moja nimerithi mikoba ya Sheikh Yahaya.
 
Mwanangu Lowassa komaa nao tuu hao. Wao wanataka Membe apite 2015 kama anaenda uani kuwania uraisi.. Komaaa nao mpaka kieleweke.. Kama kujivua gamba basi hata aliyetumia hela za EPA kwenye uchaguzi mkuu 2005 zaidi bilion 30 aanze yeye wengine mfwatie. JK lazima awe KILONGOLA katika hili

Lowasa hawa watu atakomaa nao mwanzo mwisho.
 
Acha ligi kijana..umeazimia kuandika dini..umeandika didi..mwingine anaweza asikuelewe....Hakuna anayemwandama JK kwa dini yake..haya ni maneno ya kupotosha ama kuukwepa ukweli...JK ameshindwa kuongoza nchi hii iko wazi hata ukuiwauliza watoto wa darasa lasaba wanaojitambua watakueleza...Mwinyi alikuwa raisi Tanzania nani alimuandama kwa dini yake?? embu tumia akili yako katika kuchanganua mambo sio ku copy and paste kila propaganda chafu zinazoenezwa na Magamba...Tanzania hatuchagui rais kwa dini na ndio maana 2005 alishinda kwa asilimia 85% je hii ilikuwa ni wa dini moja wamemchagua..kati ya hiyo 85% leo haifiki hata 40% watu wamechoshwa na uongozi mbaya wa Magamba na uoga na uvumilivu wa watanzania ndio sababu mpaka leo 2011..Magamba yanatawala.....Amka kijana!!

Naamin amekuelewa, ni utoto tu unamsumbua!
 
Na huko ndiko tunako elekea,lowasa anafanya kila njia ili kuweza kumuaribia JK hasa kitika serikali yake,ndio maana kwa sasa Lowasa ana mtumia sana kubenea ili kuweza kuwaharibia wakina sitta na mwakyembe ili tu aweze kuyumbisha serikali ya jk.Na kwa hili atafanikiwa tu maana inaonekana amejipanga,hata ukisoma mwanahalisi ya leo kuna kitu unaweza gundua,Mwanahalisi wanachokifanya kwa sasa ni kuwapiga Mwakyembe na Sitta kwa ishu ya CCJ toleo lililopita na toleo la wiki hii mada nyingi ni zile zile.Wanaanza kwa kuwapiga mapacha watatu kidogo halafu wanahamia kwa Sitta na mwakyembe na hili ndio dhumuni la mwanahalisi kwa sasa.

Mwanahalisi la leo limembeba Lowassa katika aspect gani?
 
Lowassa usikubali kutoka peke yako hakikisha mnaondoka na jk haiwezekani utumie fedha ulizoiba kumweka madarakani halafu akuone wewe mhalifu halafu urais wake uwe safi kaza buti chomokeni wote
 
Lowasa atamuharibiaje JK ? kwani nani ni raisi wa nchi hii. JK ni dhaifu ndio na hiyo ndo loophole anayotumia Lowasa. Angekuwa Lowasa ndo Rais na JK ndo PM mambo yangekuwa tofauti. Lowansa anagetumia madaraka yake yote kufanya chochote kwenda na rythm ya public.

Ndio maana japo simubali sana JK naona ana uvumilivu sijui upole sijui ni umbayuwayu wa ajabu ambao hauna hata cehmbe ya maslahi kwa taifa.

Nadhani unafahamu fika kuwa lowasa ni rafiki mkubwa wa jk na walishajitokeza hadharani na kusema kuwa awakukutana barabarani,kwa maneno hayo inaonesha wazi kuwa siri za lowasa,jk anazijua and vice versa is true.Lowasa anadiliki kusema wakimwaga mboga mm nitamwaga ugali unadhani nini kitatokea kwa Rais wa MBAYUWAYU?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom