Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

sasa ni chama kimekutana nao na kuwahoji au mzee msekwa amekutana nao faragha?? Hivi hizi ndio party protocols sio??

and where was mwenyekiti na katibu mkuu ??

nosediving :whistle:
 
sasa ni chama kimekutana nao na kuwahoji au mzee msekwa amekutana nao faragha?? Hivi hizi ndio party protocols sio??

and where was mwenyekiti na katibu mkuu ??

nosediving :whistle:

Wana ubavu wa kukutana uso na uso na mapacha watatu? Kikwete watamwambia yote tuliyoyatenda katika kufanikisha wewe kuingia Ikulu 2005 sasa tunayaanika hadharani, basi kijasho chembamba kitamtoka maana anajua ndio urais wake utafikia kikomo kama uchafu mbali mbali walioufanya ikiwemo wa kumchafua SAS utawekwa hadharani. Sasa kasakiziwa kazi hiyo Msekwa ambaye mwenyewe pia hana maadili yoyote ya uongozi.
 
Rejea mwanahalisi ya J5 wiki hii utaona habari hiyo kwa undani mpaka utafurahi jinsi Lowassa alivyokomaa.
 
Wagarifu wanakaa nao meza moja kuwahoji? Kwanini wasipewe barua ya kuwapiga chini uanachama kwani issue yao inajulikana wazi!
 
Saturday, 04 June 2011 10:17

chenge21.jpg


Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge

Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimethibitisha kwamba kimewahoji Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ikiwa ni moja ya hatua ya kutekeleza maazimio ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho uliofanyika Aprili 10 hadi 11 mjini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Willison Mukama ilisema kuwa hiyo ni moja hatua za awali zilizochukuliwa na kuongeza kuwa nyingine zitafuata baadaye.

Alisema hatua hiyo ya awali, Makamu Mwenyekiti CCM (Bara), Pius Msekwa alikutana na wanaotajwa katika tuhuma hizo katika sura mbili, kwanza ya nafasi yake ndani ya chama na pia kama mzee wa CCM.

Mukama alisema Mei 26, mwaka huu Msekwa alikutana na Rostam ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na siku Iliyofuata alikutana na Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

Alisema siku hiyo hiyo ya Mei 27, mwaka huu alikutana na Mjumbe mwingine wa Halmashauri Kuu, Chenge."Kwa vile Msekwa alikutana kwa faragha na viongozi hao mmoja mmoja, hakuna anayejua kilichozungumzwa. Ni Mzee Msekwa na wao peke yao," alisema katika taarifa hiyo.

Alisema hatua itakayofuata baada ya hapo ni kufikisha kwenye vikao vya chama taarifa ya mambo yaliyojiri wakati wa mazungumzo baina ya Msekwa na viongozi hao."Endapo vikao husika vitaamua lolote kuhusiana na taarifa hiyo, umma utajulishwa," alisema.

Katika mkutano huo wa Halmashauri pamoja na mambo mengine, uliwataka viongozi wa CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi kutafakari, kujipima na kuchukua hatua wenyewe kwa maslahi ya chama na kwamba wasipofanya hivyo chama kitawawajibisha.

Kimsingi ni kwamba inatakiwa haki itendeke na siyo kutoana kafara tu!
 
Mwalimu mkuu wa watu anajenga hoja kua kuna ukweli ameficha na asimame aseme ni kwa nn baada ya mwakyembe na sitta kushindwa hilo na kwa kua mpaka sasa anaweza kujinasua anazidi kuifanya jamii ijae hasira na chuki kvifuani vyao je yawezekana kuna ukweli na asimame na atoe ujasiri kama jk anaweza kumtumia nae aseme hayo nasi tujue nae mola atamusnusuru kwa huruma hiyo
 
Mwalimu mkuu wa watu anajenga hoja kua kuna ukweli ameficha na asimame aseme ni kwa nn baada ya mwakyembe na sitta kushindwa hilo na kwa kua mpaka sasa anaweza kujinasua anazidi kuifanya jamii ijae hasira na chuki kvifuani vyao je yawezekana kuna ukweli na asimame na atoe ujasiri kama jk anaweza kumtumia nae aseme hayo nasi tujue nae mola atamusnusuru kwa huruma hiyo

Amesharudi toka kwa Askofu Joshua? bongo bwana nyie acheni tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom