Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

hawezi mwaga chochote.......anajua nini anafanya.........muulizeni walipokutana na jk siku ile kule zenji jk alimwambia nini katika yale mazungumzo yao?.........

jk ni ndumilakuwili sana na bonge la nafiki lile.........

Penye nyekundu ni useful.
 
mwisho wa ccm ni kumalizana wenyewe kwa wenyewe


Ndiyo maana wachambuzi wa masuala ya siasa wamekuwa wakisema kuwa
gamba la CCM ni CCM yenyewe, hivyo kujivua gamba inamaanisha kukiua chama.
Duh, sisi yetu macho kujionea sinema ya bure jinsi wakubwa watakavyovuana nguo
hadharani.
 
Hii ni ile dhambi ya Uzanzibari na unzazibara inawatafuna CCM, hahaha na watachapana bakora wenyeweeeeeee
 
Ee Mola endelea kunipa uhai ili niweze kuona madudu zaidi yaliyofanyika kumwingiza JK madarakani...Niweze kuona mwisho wa unafiki wa JK...Niweze kuona mihtasari ya mikutano ya siri iliyoongozwa na EL kupanga njama za kukwapua fedha za EPA ili JK aingie madarakani..Niweze kuona CCM ikimeguka mapande matatu..Niweze kupata ukweli wa chanzo cha chuki ya JK kwa Cigwiyemisi, Mkapa na Dr Salim..Niweze kupata ukweli kuhusu uhusiano wa JK, RA na Kagoda..........Aaamin!

Mola husikia maombi ya waja wake.
 
Vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotakiwa wajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi wamekutana na uongozi wa juu wa chama chao, na taarifa zinasema bado mvutano haujaisha kati ya pande mbili hizo. Taarifa za hakika zimeliarifu Raia mwema kwamba walikutana na makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa, wiki iliyopita, na kwamba mmoja wao, Edward Lowassa, Bado ana donge.
Habari zinaeleza kwamba Lowassa (Mbunge wa Monduli), Rostam Aziz(Mbunge wa Igunga) na Andrew Chenge (Mbunge wa Bariadi magharibi) waliitwa ofisi ndogo ya CCM, Lumumba Dar es Salaam wakitakiwa kutekeleza uamuzi wa NEC.
Lakini habari kutoka kwa watu wa karibu na Lowassa zinaeleza kwamba mwanasiasa huyo amebainisha kwamba hakubaliani na uamuzi wa NEC. “Mzee (Lowassa) amesema kwamba aliitwa na kwamba alitakiwa kuachana na suala la urais ili mambo yaishe, lakini amewaambia uamuzi wowote kisiasa ni haki yake kikatiba, na hivyo hakubaliani nao” anasema Mbunge mmoja ambaye yuko katika kambi ya Lowassa akiongeza: “Ila wajue kwamba wao wakimwaga mboga sisi tunamwaga ugali”. Kwa mujibu wa Mbunge huyo, Rostam Aziz na Chenge wanaonekana kulegeza kamba katika suala hilo.
Anasema mbunge huyo “Rostam amesema wazi kwamba hawezi kushindana na Rais aliye madarakani hata kama watakuwa wameonewa. Chenge anakubali tu kwasababu anaona hana jinsi. Lowassa bado moyo wake ni mzito”…………………………………………………………………………………………………….Gazeti lilipotaka Lowassa alizungumzie suala hilo alijibu “No coment, No coment, No coment”

Taarifa ambazo Raia mwema limezipata zinaeleza kuwa tayari viongozi hao ambao wote ni wajumbe wa NEC na walihudhuria kikao kilichoazimia wajiuzuru, wameshakabidhiwa barua rasmi za kuwataka wajiuzuru zikirejea uamuzi wa vikao vya juu vya CCM.


Source: Raia Mwema June1-June7, 2011

Jamani mbona mtandaoni bado hawajaweka toleo (June1-June7) hili?? msaada tuna hamu na hizi habari nzuri zenye dalili za kukiangamiza chama cha magamba
 
Ieleweke kwamba Lowassa sio yeye peke yake aliyehusika katika masuala mazito ya ufisadi yaliyomchafua..ni dhahiri yalikuwa na baraka ama maagizo ya mkubwa wake..Sasa leo hii yeye ndiyo watanzania wote tuthibitishiwe kwamba ni mbaya..itamuuma tu na ninabashiri makubwa kutokea na CCM kuanguka kama zigo la kuni..Ama sivyo ile hali ya kuuwana ndani ya CCM inaweza chukua nafasi ili kuepukana Chama Kusambaratika..Tume ya Mwakyembe iliposoma ripoti ya Richmond ilithibitisha kuweka kapuni baadhi ya mambo ili kulinda amani ya nchi..mnafikiri yalikuwa ni mambo gani? na mnapata picha gani Lowassa anaposema hata angepewa nafasi tena angefanya kama alivyofanya?hamuoni kuna uwezekano mkubwa alitelekeza maagizo...Binafsi nitapenda kuona Lowassa akimwaga mboga baada ya wao kumwaga ugali ili yatimie
 
Jamani mbona mtandaoni bado hawajaweka toleo (June1-June7) hili?? msaada tuna hamu na hizi habari nzuri zenye dalili za kukiangamiza chama cha magamba

Wakiweka, hutanunua hard copy mitaani na ofisi zao zitafungwa hivyo itakuwa ngumu wewe kupata hata hiki kisehemu cha habari zao.
 
Yanayo mkuta Kikwete ni kwamba anaandamwa kwasababu ya dini yake, yanayomkuta Lowasa ni haki yake lazima asurubiwe.
 
Mimi nadhani Lowassa kama Mwanasiasa mkongwe alitakiwa a-step down tu, kwasababu system haimtaki tena kwasababu kaichafua. sasa akimwaga ugali yeye itamsaidia nini? afanye kitu ambacho kitamfanya arudishe heshma yake na siyo kuwa na "moyo wa tukose wote"

nimaatunda ya ccm ndo walichokipanda wanasitaili wakivune
 
Mmmmmh mimi kwwli kwa mwenendo wa sasa wa serikali mi naona kuna mvutano mkubwa sana wa mambo yafuatayo.

1. kuna kundi ambalo linaona kweli wameshindwa kuongoza serikali na hawastahili so wanataka kujivua gamba serikalini kabisa........nadhani hata JK anataka sema hasemi tu.

2. kuna kundi ambalo wanaona wameshindwa kuongoza kabisa ila wanagangamala tu kibongobongo butua liende.

3. kuna wale wenzangu na mimi ambao hata ukiwasha moto machoni mwao hawaoni... wenyewe wanaona wako sawa kabisa na wanaongoza vizuri so nao wanagangamala na upuuuzi wao.


IPO SIKU MKULIMA ATASHIKA JEMBE NA ALIME KICHWA CHA MTU NDIPO TUTAMBUE KUMBE ANAHITAJI HAKI
 
Eddy usikubali kabisa, yaani wewe na RA muuibe mihela yote ili badala ya kutumia na familia zenu hela mkazipeleka CCM ili JK apange pale Magogoni leo yuko pale anawabadilikia, hata msikubali kama noma na iwe noma kama jela wote muende huo ndio uana ume kama alivyokusifia SS kuwa wewe ni mwanaume wa shoka, onyesha ujabali wako.
 
yanayo mkuta kikwete ni kwamba anaandamwa kwasababu ya dini yake, yanayomkuta lowasa ni haki yake lazima asurubiwe.

hakuna cha udini wala nini..........hawezi kuongoza tu ndio shida 100% anasitahili kutoka aachie wengine
 
Eddy usikubali kabisa, yaani wewe na RA muuibe mihela yote ili badala ya kutumia na familia zenu hela mkazipeleka CCM ili JK apange pale Magogoni leo yuko pale anawabadilikia, hata msikubali kama noma na iwe noma kama jela wote muende huo ndio uana ume kama alivyokusifia SS kuwa wewe ni mwanaume wa shoka, onyesha ujabali wako.



HAHAHAHA dOUGLAS BANA...... HAYA NDIO YANATUUA WABONGO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom