Hapana mkuu samahani kama post yangu sujaieleza sawa sawa. Lowassa hana usafi wowote, naamini kabisa ameshiriki kwenye Richmond. Lakini ndugu wa karibu wa Lowassa na baadhi ya viongozi wa dini wanaamini Lowassa alitumiwa tu na mkubwa, alijiuzulu ili kumuokoa rafiki yake. Lakini ukweli ni kwamba maovu ya Lowassa na maovu ya JK ni hayo hayo, wote walikua pamoja, walifahamishana na walipeana go ahead/support. Lakini JK anataka kujionyesha safi kwa watanzania hasa wanachama wake, kwahiyo ni lazima ahakikishe RACHEL wanaondoka kwenye mawazo ya watanzania. Lowassa & grp kukubali kupotea kwenye ramani ni kukubali kosa kwamba yeye ndio gamba kuu la chama wananchi wanaolipigia kelele. Lakini Lowassa makubaliano yake na JK ni kuwa at one point na yeye aje apiganie uraisi na apewe support na JK. JK inawezekana alikua anamkubalia tu kisanii ili aingie Ikulu, au labda amebadilisha mawazo na anamtaka mtu mwingine. JK ni ndumilakuwili so ni vigumu kujua akiwa na Lowassa anamwambia nini, na akiwa na kina Msekwa anawaambia nini. However Lowassa anahaki ya katiba kuomba apendekezwe kupigania uraisi kwanini wanamuita ku-negotiate? Kama wananchi wa CCM wako-serious then hawatampitisha kwenye vikao vyao. Kwanini wasimuondoe tu bila ku-negotiate? Kama mwizi mwizi tu! Unless CCM wanataka kutuambia Lowassa ni fisadi lakini pia bila Lowassa hamna CCM.