Huo si utawala wa sheria hata kidogo!
Kama Lowasa, RA na Chenge wana makosa basi makosa yao yawekwe adharani na pia ushahidi uperekwe mahakamani ili wapate haki yao; mahakama ndicho chombo cha kuprove mtu kuwa gilty! Lasivyo wanaonewa kwasababu ambazo Kikwete ndio anazijua mwenyewe.
Mbona Yona na Mramba walishtakiwa kwa makosa yao bila kufukwa chamani! Kama mahakama ita-prove kuwa wao wanamakosa ndipo chama kiwafukuze, hapa CCM iache kiini macho kwa kutaka kubambikiza watu watatu tu uchafu wote wa chama. Hivi katika nchni hii ukiibia taifa adhabu yake ni kufukuzwa katika chama? na Je ni hao watatu tu! kwanini hawapewi nafasi ya kujitetea na kwanini hakuna chombo kinacho tekeleza haki juu yao! wanahukumiwa kwa vigezo gani? mbona hawaperekwi mahakamani kama kweli ni mafisadi?
Arafat, umekaribia kukugusa haswa kuhusu hili suala.
Mikakati na mbinu ya kuwaengua RACHEL (Rostam Aziz, CHenge, Edward Lowassa) kutoka NEC ya CCM kwa vigezo vywa kujivua gamba, kamwe na asilani havina uhusiano wo wote na ufisadi.
Hii ni njia tu ya kujaribu kuwatoa kwenye chombo cha juu cha maamuzi ndani ya CCM. Na ndiyo maana haizungumziwi wao kuvuliwa uanachama au kuvuliwa ubunge. Msisitizo upo tu katika kuwaengua NEC.
Tujiulize kwanini.
Kuna wanaodai kuwa hii ni mvutano kuelekea uchaguzi wa u-Rais 2015, na nani kuwa mgombea wa CCM, na pia kuna wanaodai kuwa hii ni mojawapo ya njia ya CCM kujijenga upya na kurudisha imani kwa wananchi.
Kama lengo ni uchaguzi 2015, basi msukumo huu ndani ya CCM una walakini mkubwa sana. CCM kama chama kitafanya chaguzi zake za ngazi zote mwaka 2012, hiyo ikiwa takribani miaka 3 kabla ya uchaguzi wa 2015. Rostam, Chenge na Lowassa kama ni nuksi au karaha ndani ya CCM, basi CCM ina wakati mzuri tu wa kuwapiga chini 2012 huko NEC na kuondokana na nuksi hiyo.
Kwa nini CC (JK, Mukama, Msekwa, Nape) inatumia nguvu na mabavu kujaribu kuwafanya hawa 'mafisadi' watatu wajiuzulu kabla ya July 2011, wakati CCM hiyo hiyo inaweza kuwapiga chini 2012 bila purukushani?
Hilo CCM wanajua haliwezekani, na ni vigumu kulizuia kwani hawa watatu ndiyo siri ya JK kuwa Magogoni na ndiyo nguvu ya CCM ya kweli ndani ya NEC na Mkutano Mkuu. CC ya CCM haina meno. Meno yako NEC na Mkutano Mkuu, na huko ndiyo RACHEL wamejikita. CC ya CCM ilishindwa hata kumvua uanachama Nape, Bashe au Shibuda (kwa kutaja wachache tu), pamoja na majigambo yote ya "kufungiwa duniani, na hata mbinguni".
Kama suala ni ufisadi, pasi na ushahidi, basi Mramba, Yona, Chenge, Rostam, Manji, Malecela, Mkapa, Mwinyi.... kwa uchache tu hawa wangetakiwa 'kujivua gamba' kwa tuhuma zao za ufisadi (Mramba, Yona - Alex Stewart, Kiwira, Chenge - Rada, Madini, Rostam - Kagoda, Dowans, Manji - Kagoda, Quality Plaza, Ubungo EPZ, Malecela - EPA Jeetu, RITES Chande, Mkapa - ANBEM, Songas, Kiwira, Mwinyi - IPTL, Loliondo, Golden Tulip).
Katika orodha hiyo ukiwaacha Rostam na Chenge, wengine hawatajwi kwa kuwa nia hasa si kupambana na Ufisadi ndani ya CCM (hawa wote ni card-carrying, high profile members wa CCM).
Na ndiyo maana katika orodha za watuhumiwa wakuu wa ufisadi waliyotajwa Mwembeyanga (2006) na Tabora (2011), ni watu wawili tu (Rostam, Chenge) kati ya watu takribani 20 waliotajwa, ambao wanaambiwa wajitoe NEC. Ufisadi haukuwa msamiati wa CCM kwa miaka yote hiyo, na bado si msamiati wao sasa na hata kuelekea mbele.
Kwa hiyo tunarudi pale pale kuwa nia hasa ni kujaribu kuchukua control ya NEC na Mkutano Mkuu kutoka kwa RACHEL, ila sijui control itakwenda wapi, lakini nakuhakikishia siyo kwa JK.
Suala la CCM kujivua ufisadi kupitia kwa RACHEL, lingefanya hata Makinda asiupate u-Spika (na alikuwa mkweli kuwa aliombwa na Rostam kugombea), lakini kinyume na hayo JK mwenyewe alilishikia bango na kuhakikisha kuwa Makinda anaupata u-spika, ije mvua, ije jua. Na akamtuliza Sita na u-waziri mchecheto.
Suala la CCM kujivua ufisadi kupitia RACHEL, lingefanya serikali kukataa kwa dhati kuilipa Dowans Bil 94, lakini kinyume na hayo Werema alisema (akiwa Ikulu), kuwa lazima walipwe, CC ya CCM ikakutana ikulu wakasema lazima walipwe, JK hadi leo hii hajawahi kamwe kusema wasilipwe (kawahi kusema mara nyingi tu kuwa itabidi 'waangalie' badala ya kukimbilia kulipa).
Suala la CCM kujivua ufisadi kupitia RACHEL, lingefanya Ridhiwan (mwana wa mfalme) aepuke kama ukoma kukutana faragha na El-Adawi, wakati huo huo JK akituhumiwa kutumiwa na Rostam na El-Adawi kufanikisha malipo haramu ya Dowans.
Na tukirudi kwenye suala la kurudisha imani kwa wananchi kuhusu CCM, hao RACHEL walipigiwa kura na hao hao wananchi na kupewa ubunge kwa zaidi ya asilimia 90 katika majimbo yao, wakati JK alipata pungufu ya asilimia hizo katika majimbo hayo hayo. Je, hapo ni nani ambaye wananchi hawana imani naye?
Hili sakata sioni kama litakuwa na mwisho mzuri, na nikirejea kauli ya Lowassa wakati Nape anaanza safari zake za kujitambulisha ni kuwa, je , ili upate umaarufu ndani ya CCM ni lazima uonekane kuwa unapambana na Lowassa? Toka lini mapambano dhidi ya Lowassa imekuwa ni sera za Chama?