Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

Sarakasi za Lowassa zinaendelea huyu jamaa hasafishiki aendelee tu kugombea ubunge wa monduli mpaka atakaposhindwa mwenyewe. Kwengineko hauziki na wakijaribu kumuuza kinguvu ndio mwisho wa CCM. Lowassa kwanini anataka madaraka si ana mali za kutosha kula pensheni mpaka uzeeni (aombe mungu asitokee chizi kama kule Misri kwani anamuona mwenzie Mubarak na familia yake wanavyopata joto ya jiwe labda wahamishe mali zao nje ya dunia hii!!!)
 
Arafat, umekaribia kukugusa haswa kuhusu hili suala.

Mikakati na mbinu ya kuwaengua RACHEL (Rostam Aziz, CHenge, Edward Lowassa) kutoka NEC ya CCM kwa vigezo vywa kujivua gamba, kamwe na asilani havina uhusiano wo wote na ufisadi.

Hii ni njia tu ya kujaribu kuwatoa kwenye chombo cha juu cha maamuzi ndani ya CCM. Na ndiyo maana haizungumziwi wao kuvuliwa uanachama au kuvuliwa ubunge. Msisitizo upo tu katika kuwaengua NEC.

Tujiulize kwanini.

Kuna wanaodai kuwa hii ni mvutano kuelekea uchaguzi wa u-Rais 2015, na nani kuwa mgombea wa CCM, na pia kuna wanaodai kuwa hii ni mojawapo ya njia ya CCM kujijenga upya na kurudisha imani kwa wananchi.

Kama lengo ni uchaguzi 2015, basi msukumo huu ndani ya CCM una walakini mkubwa sana. CCM kama chama kitafanya chaguzi zake za ngazi zote mwaka 2012, hiyo ikiwa takribani miaka 3 kabla ya uchaguzi wa 2015. Rostam, Chenge na Lowassa kama ni nuksi au karaha ndani ya CCM, basi CCM ina wakati mzuri tu wa kuwapiga chini 2012 huko NEC na kuondokana na nuksi hiyo.

Kwa nini CC (JK, Mukama, Msekwa, Nape) inatumia nguvu na mabavu kujaribu kuwafanya hawa 'mafisadi' watatu wajiuzulu kabla ya July 2011, wakati CCM hiyo hiyo inaweza kuwapiga chini 2012 bila purukushani?

Hilo CCM wanajua haliwezekani, na ni vigumu kulizuia kwani hawa watatu ndiyo siri ya JK kuwa Magogoni na ndiyo nguvu ya CCM ya kweli ndani ya NEC na Mkutano Mkuu. CC ya CCM haina meno. Meno yako NEC na Mkutano Mkuu, na huko ndiyo RACHEL wamejikita. CC ya CCM ilishindwa hata kumvua uanachama Nape, Bashe au Shibuda (kwa kutaja wachache tu), pamoja na majigambo yote ya "kufungiwa duniani, na hata mbinguni".


Kama suala ni ufisadi, pasi na ushahidi, basi Mramba, Yona, Chenge, Rostam, Manji, Malecela, Mkapa, Mwinyi.... kwa uchache tu hawa wangetakiwa 'kujivua gamba' kwa tuhuma zao za ufisadi (Mramba, Yona - Alex Stewart, Kiwira, Chenge - Rada, Madini, Rostam - Kagoda, Dowans, Manji - Kagoda, Quality Plaza, Ubungo EPZ, Malecela - EPA Jeetu, RITES Chande, Mkapa - ANBEM, Songas, Kiwira, Mwinyi - IPTL, Loliondo, Golden Tulip).

Katika orodha hiyo ukiwaacha Rostam na Chenge, wengine hawatajwi kwa kuwa nia hasa si kupambana na Ufisadi ndani ya CCM (hawa wote ni card-carrying, high profile members wa CCM).

Na ndiyo maana katika orodha za watuhumiwa wakuu wa ufisadi waliyotajwa Mwembeyanga (2006) na Tabora (2011), ni watu wawili tu (Rostam, Chenge) kati ya watu takribani 20 waliotajwa, ambao wanaambiwa wajitoe NEC. Ufisadi haukuwa msamiati wa CCM kwa miaka yote hiyo, na bado si msamiati wao sasa na hata kuelekea mbele.

Kwa hiyo tunarudi pale pale kuwa nia hasa ni kujaribu kuchukua control ya NEC na Mkutano Mkuu kutoka kwa RACHEL, ila sijui control itakwenda wapi, lakini nakuhakikishia siyo kwa JK.


Suala la CCM kujivua ufisadi kupitia kwa RACHEL, lingefanya hata Makinda asiupate u-Spika (na alikuwa mkweli kuwa aliombwa na Rostam kugombea), lakini kinyume na hayo JK mwenyewe alilishikia bango na kuhakikisha kuwa Makinda anaupata u-spika, ije mvua, ije jua. Na akamtuliza Sita na u-waziri mchecheto.


Suala la CCM kujivua ufisadi kupitia RACHEL, lingefanya serikali kukataa kwa dhati kuilipa Dowans Bil 94, lakini kinyume na hayo Werema alisema (akiwa Ikulu), kuwa lazima walipwe, CC ya CCM ikakutana ikulu wakasema lazima walipwe, JK hadi leo hii hajawahi kamwe kusema wasilipwe (kawahi kusema mara nyingi tu kuwa itabidi 'waangalie' badala ya kukimbilia kulipa).


Suala la CCM kujivua ufisadi kupitia RACHEL, lingefanya Ridhiwan (mwana wa mfalme) aepuke kama ukoma kukutana faragha na El-Adawi, wakati huo huo JK akituhumiwa kutumiwa na Rostam na El-Adawi kufanikisha malipo haramu ya Dowans.

Na tukirudi kwenye suala la kurudisha imani kwa wananchi kuhusu CCM, hao RACHEL walipigiwa kura na hao hao wananchi na kupewa ubunge kwa zaidi ya asilimia 90 katika majimbo yao, wakati JK alipata pungufu ya asilimia hizo katika majimbo hayo hayo. Je, hapo ni nani ambaye wananchi hawana imani naye?


Hili sakata sioni kama litakuwa na mwisho mzuri, na nikirejea kauli ya Lowassa wakati Nape anaanza safari zake za kujitambulisha ni kuwa, je , ili upate umaarufu ndani ya CCM ni lazima uonekane kuwa unapambana na Lowassa? Toka lini mapambano dhidi ya Lowassa imekuwa ni sera za Chama?

Hoja zote ulizoongea nakubaliana nawe kama nilivyosema awali kasoro hii ya kutumia wingi wa kura kuonyesha kuwa ndio wananchni wanampenda mtu! kumbuka maswala ya kura bado yana utata hapa Tanzania hasa hizi kura za CCM ambazo tunajua jinsi wanavyozipata, mfano mzuri wa kura ni Dr Slaa na Kikwete; hakika ya wazi Watanzania takribani 90% wanamtaka Slaa awe Raia wao lakini cha ajabu aliyepata kura zaidi ya Slaa anaitwa kikwete!! ajabu.

Kama nilivyosema awali na kama ulivyounga mkono ni sawa ila umekosea kuhitimisha (Conclusion) kuwa hawana kosa ila wanachogombania ni kuwapunguzia hawa mapacha nguvu ndani chama, huu ni uongo dhahiri shahiri! Makosa yao hayapo katika black box yapo wazi kila mtu anayajua na yanaoneka juani hata gizani! cha ajabu sijui kwanini serikali ya CCM haitaki kuwashitaki na hapa ndipo hoja yangu iliposimamia.

Swala la iwapo hawa watu wanamakosa au la! silakujadili hapa ambaye hayajui basi ana matatizo na ninadhani si member wa JF, maana hata JF makosa ya hao jamaa yamejadiliwa kwa mapana na marefu sana. Hapa hoja ingejikita ni kwanini hawataki kuwashtaki? na hapo ndipo nilipoacha wazi maana hawaongelei kuwashtaki wala kuwanyanganya Ubunge ok fine kwanini husi-hitimishe kuwa hawafanyi hivyo kwasababu wizi waliofanya hawajamaa ulimnufahisha pia Kikwete! au hata ulienda mbali ukawa wizi wa CCM na hivyo chama chote kinahusika na si hawa watatu tu!

Tunahitaji washitakiwe ilitujue hizo fedha waliiba kwa niaba ya nani? lasivyo wasiposhtakiwa mimi binafsi nitaendelea kuamini kuwa huo wizi ulifanywa kwa mpango mahsusi kwa ajili ya CCM
 
Gazeti la KULIKONI la leo moto!....



BAJETI YA SERIKALI 2011-2012

Mafisadi waleta
balaa Tanzania

* Wasababisha serikali inyimwe misaada
* CCM yatakiwa kuwafukuza mara moja
* Richmond, rada, Kagoda zaumiza nchi


MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

WAFADHILI wanaotoa msaada kwa Tanzania wamekata misaada kwenye bajeti ya serikali ya 2011/12 itakayosomwa Dodoma wiki ijayo kutokana na kukithiri kwa ufisadi, huku wakisema kuwa mafisadi wameharibu sifa nzuri ya Tanzania.

Kundi la wafadhili 12 wakubwa -- Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Canada, Denmark, Jumuiya ya Ulaya, Finland, Ujerumani, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki ya Dunia -- wameelezwa kuchoshwa kwao na ufisadi unaoendelea nchini.

Nchi hizo zimepunguza tena msaada kwa Tanzania kwa bajeti ijayo ya Tanzania na kuamua kutoa dola za Marekani milioni 453 tu ikilinganishwa na msaada wa dola za Marekani milioni 534 kwenye bajeti iliyopita.

Tayari wafadhili walipunguza misaada kwa karibu robo ya dola bilioni moja za Marekani kwenye bajeti ya 2010/11 ikifananishwa na mwaka uliotangulia kwa sababu ya ufisadi na serikali kuwa na kasi ndogo ya kufanya mabadiliko mbalimbali.

Punguzo la misaada kwa bajeti ijayo ni adhabu ya mara pili mfululizo kwa Tanzania kutoka kwa wafadhili kutokana na tatizo la ufisadi.

Wafadhili hao walieleza bayana katika taarifa yao hivi karibuni kuwa kutofikishwa mahakamani kwa baadhi ya watuhumiwa wakubwa wa ufisadi ni moja ya sababu zinazowafanya wasite kuendelea kutoa misaada zaidi kwa serikali.

Uamuzi huo wa wafadhili unakuja huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa katika jitihada za "kujivua gamba" kwa kuwaondoa kwenye nafasi za uongozi wanasiasa waandamizi maarufu kama "Mapacha Watatu" ambao wamehusishwa kwa muda mrefu na tuhuma kubwa za ufisadi nchini ikiwemo kashfa ya Richmond, rada, Kagoda na Tangold/Meremeta.

"Serikali imechukua hatua nzuri ambazo zimesaidia kurejesha imani, lakini badi tuna hofu kuwa kesi hizi nyingi (za ufisadi) hazijapatiwa ufumbuzi," ilisema taarifa ya wafadhili hao.

Mapacha Watatu wa CCM -- Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa, waziri wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya rada Andrew Chenge na mfanyabiashara mwenye tuhuma lukuki za ufisadi, Rostam Aziz -- wamekuwa wakitajwa muda mrefu kuwa wanakivuruga chama tawala.

"Lowassa, Chenge na Rostam wana tuhuma nzito za ufisadi, kuendelea kuwepo kwao ndani ya CCM kwenye nafasi nyeti na kutofikishwa kwao mahakamani kumeleta picha mbaya kuwa chama tawala kimakumbatia mafisadi," alisema kada mmoja wa CCM.

"Hata TAKUKURU wenyewe wamekuwa wanaogopa kuwachunguza na kuwafikisha mahakamani watu kama hawa kwa kuwa bado wanashikilia nafasi za uongozi ndani ya CCM."

Kitendo cha wafadhili kupunguza msaada kwa Tanzania kimeleta pigo kubwa kwa jitihada za serikali ya Rais Jakaya Kikwete ya kupiga vita umasikini nchini na kuleta maendeleo.

Miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa barabara, elimu, maji, afya na huduma nyingine za jamii itaathiriwa na hatua hii ya wafadhili kama hatua za haraka hazitachukuliwa na serikali na chama tawala cha CCM.

"Kwa kweli CCM ikiendelea kuwakumbatia hawa watu wenye tuhuma kubwa za ufisadi basi si chama peke yake kitaathirika, bali taifa zima kutokana na wafadhili kupunguza misaada," alisema afisa mmoja wa serikali.

"Utaratibu wa utawala bora ni pale mtu anapokuwa na tuhuma nzito za ufisadi kujiuzulu yeye mwenyewe nafasi zote za uongozi kwenye serikali na chama ili kuviachia vyombo vya uchunguzi na hatimaye mahakama zifanye kazi zao."

Tayari ndani ya CCM kumekupo mashinikizo ya kuwataka watuhumiwa hao wakuu kujiondoa ndani ya chama hicho, sambamba na hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yao.

Lowassa na marafiki wake wa karibu, Mbunge wa Igunga Rostam Aziz na Waziri wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya rada, Andrew Chenge, wametajwa kuwa chanzo cha CCM kuchukiwa na wananchi wengi kwa kuonekana kuwakumbatia wanasiasa wenye tuhuma nzito za ufisadi.

Kumekuwa na maoni kutoka kwa wananachama wengi waandamizi wa CCM kuwa ni vyema Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho ikafanya kikao cha dharura ili kuwafukuza wanasiasa hao kwenye chama.

Viongozi wa juu wa chama, wajumbe wa jumuiya za chama pamoja na wanachama wa CCM wamekuwa na hofu kubwa kuwa huenda kundi hilo la wanasiasa maarufu kama "Mapacha Watatu" litasababisha chama hicho kianguke kabisa katika uchaguzi wa 2015 baada ya kufanya vibaya uchaguzi uliopita wa 2010.

Mjumbe mmoja wa NEC aliliambia KULIKONI wiki iliyopita kwamba ‘Mapacha Watatu' ni sumu kubwa kwenye chama akisema wanakipasua chama kutokana na Watanzania kutokuwa na imani nao.

"CCM imeshutumiwa kuwa inakumbatia rushwa kwa kuwa na viongozi kama hawa waliochafuka sana kwa tuhuma za ufisadi, ni vyema NEC ikafanya kikao cha dharura ili tufanye uamizi wa haraka wa kuwafukuza kabisa kina Lowassa, Rostam na Chenge kwenye chama. Wamekichafuachama chetu mno," alisema.

Kwa mujibu wa makada wa CCM, "Operesheni Okoa Mapacha Watatu" inaendelea kwa kasi kubwa kwa kutumia mamilioni ya shilingi, huku baadhi ya magazeti maarufu yakitumiwa kwenye kampeni hiyo.

"Lengo la operesheni hii ni kujaribu kuwachafua viongozi wanaoheshimika ndani ya CCM kama Rais Jakaya Kikwete na mawaziri wake wakiwemo Samuel Sitta, Harisson Mwakyembe, Bernard Membe na John Magufuli," alisema mjumbe huyo wa NEC kutoka kanda ya kaskazini.

"Hawa watu wanafanya kampeni chafu sana kutumia magezeti yaliyowekwa mfukoni mwao eti wakijaribu kuwachafua viongozi wote ndani ya CCM ili kuwaokoa Mapacha Watatu."

Tayari baadhi ya wana CCM maarufu wakiwamo wazee wenye nguvu ndani ya chama hicho wamekwishatamka kwamba kuendelea kubishana na Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu ni uhaini hasa kwa wale ambao wameonyesha nia ya kulipiza kisasi.

Mwana CCM mmoja aliye karibu na mwasisi mmoja wa CCM ameliambia KULIKONI kwamba mzee huyo (jina tunalihifadhi hadi tutakapompata) ametamka wazi kwamba Lowassa na wenzake wanachofanya ni uhaini.

"Mzee anasema anashangaa sana hawa mafisadi wakisema kwamba Mwenyekiti ‘akimwaga mboga wao wanamwaga ugali', huo ni uhaini," alisema kijana huyo ambaye ni mwanasheria ambaye yumo karibu na dola.

<Source: KULIKONI la Ijumaa, Juni 3, 2011>
 
Hawa kina RACHEL (Rostam Aziz, Chenge na Lowassa) ni kaburi la CCM na ni janga la kitaifa!
 
Hawa kina RACHEL (Rostam Aziz, Chenge na Lowassa) ni kaburi la CCM na ni janga la kitaifa!
Napinga kwa nguvu zote hawa jamaa hawawezi na hawataweza kuwa janga la taifa, nchi wameikuta watakufa na wataiacha labda ni kaburi la CCM.
 
ndio hapo tunapowashauri Nape na Mukama lakini hawataki kusikia/kuelewa.....wao wapo bize kupambana na kunyamazisha CDM na wanaharakati wote Tanzania hii lakini siku hizi dunia ni kijiji....kinachofanyika Maramba (Tanga) au Marangu kinafika USA, UK nk instantly.....wao wanaeneza propaganda kwa watanzania maamuma lakini wenye akili zao wanaona na kuelewa.....sasa wakimaliza mikutano yao ya kufafanua falsafa ya kujivua gamba huko mikoani, wataenda kwa hao wafadhili kuwafafanulia pia!!
 
Mkullo na JK wataleta siasa (propaganda) kwenye hiyo bajeti na kusema 'bajeti imeongezeka kutoka 11.6 trilioni TShs (2010/2011) hadi 12.8 trilioni TShs (2011/2012) sawa na ongezeko la 1.2 trilioni TShs na kwa hiyo hatujayumbishwa na wafadhili kupunguza misaada'. Hapa watajifanya mbumbumbu kuto-consider inflation iliyopo
 
wametumwa na samweli sitta
mroho wa madaraka msaliti na
mwanzilishi wa ccj aliyeifisadi cda
dodoma

Na wewe nani kakutuma???? Lowassa, Chenge au baba lao Rostam
 
Kina Rachel wataendelea kudunda tu, CCM hawawawezi mapacha hao maana ndio walioshikilia mpini wa CCM. Pesa ni kitu cha ajabu sana hasa ikikutana na mpenda pesa. Watamwaga pesa na msishangae mwaka 2015 Rais na Msaidizi wake na Waziri Mkuu wakawa ndio wenyewe.
 
Mwenyekiti Kikwete hana nia ya dhati kuwaondoa mafisadi kwenye chama chake. Hofu yake kubwa ni kwamba hawa jamaa wanamjua vizuri sana A hadi Z, hivyo anaogopa ataumbuka! Yuko radhi tuendelee kukosa misaada ya maendeleo kuliko kuwatosa maswahiba wake. Yangu macho!!!
 
Kwanini JK asitubu na kuconfess kwa watanzania madudu waliyofanya sirini na mapacha watatu ili awe na nguvu ya kuwamwaga tufungue ukurasa mpya? Pengine watanzania wangeweza kumsamehe kuliko hivi anavyofanya sasa hivi, anakiadhibu chama chake kwa misuguano na mbaya zaidi analizamisha Taifa kwenye lindi la umaskini ambao recovery yake itakuwa decades!!
I wish angetubu alipoingia awamu ya pili halafu apitishe fagio la chuma.


Mwenyekiti Kikwete hana nia ya dhati kuwaondoa mafisadi kwenye chama chake. Hofu yake kubwa ni kwamba hawa jamaa wanamjua vizuri sana A hadi Z, hivyo anaogopa ataumbuka! Yuko radhi tuendelee kukosa misaada ya maendeleo kuliko kuwatosa maswahiba wake. Yangu macho!!!
 
Wanasubiri nini kushitakiwa? Hivi ufisadi unasemwa tu mdomoni? Kwanini hawaendi mahakamani? Hilo ni bomu na wakicheza litawamaliza wenyewe hadi waishe kama hawatafanya maamuzi sasa na si baadae ama kesho. Nadhani hata leo wamechelewa, ingekuwa kule kwenye kikao cha Butiama cha NEC ya CCM
 
Mwenyekiti Kikwete hana nia ya dhati kuwaondoa mafisadi kwenye chama chake. Hofu yake kubwa ni kwamba hawa jamaa wanamjua vizuri sana A hadi Z, hivyo anaogopa ataumbuka! Yuko radhi tuendelee kukosa misaada ya maendeleo kuliko kuwatosa maswahiba wake. Yangu macho!!!

hawa jamaa wanatakiwa wamrahisishie wenyewe jk, wanalitikisa tawi walilokalia...wasingoje wakaangukia kwa slaa
 
Lowasa mwagaaaaaaaa! Ndio wakati wa Chama cha Magamba kung'ooka

Edward Ngoyai Lowassa usikubali kutumika kama daraja, jamaa ulimbeba kwenye mtandao leo anatakakukugeuzia kibao, kataa kabisa. Tunajua na tunaukubali utendaji wako. Ungekuwa wewe ndo yeye leo mafisadi wote wangeshajipeleka wenyewe gerezani!

Komaa mwana wa kimaasai mpaka kieleweke, kwani nini bwana-kama kupasuka acha joka lipasuke!
 
Kina Rachel wataendelea kudunda tu, CCM hawawawezi mapacha hao maana ndio walioshikilia mpini wa CCM. Pesa ni kitu cha ajabu sana hasa ikikutana na mpenda pesa. Watamwaga pesa na msishangae mwaka 2015 Rais na Msaidizi wake na Waziri Mkuu wakawa ndio wenyewe.

Hata hivyo nasi tumezidi. Tuliona wapi mama au baba wa miaka hamsini akiendelea kunyonya? Mpaka leo bado tunahitaji msaada wa waliokuwa wakoloni wetu kweli? Tuko sawa? Miaka hamsini baada ya uhuru! Muangalie mtu mwenye umri huo wa miaka hamsini halafu ufikirie kuwa anahitaji kunyonya kwa mama yake. Ni zaidi ya aibu, ni fedheha. Wakate misaada yao yote tupate akili. Nchi nyingi zilipata maendeleo endelevu wakati zimewekewa vikwazo, lakini huu mlegezo wa TZ unatisha.
Wajinga ndio waliwao. Tunawapa misamaha ya kodi kama wawekezaji halafu baadaye tunapeleka bakuli kuomba msaada. Tuko sawa?

Dawa ya mjinga ni kuumia!
 
Siku RACHEL watakapofungua midomo yao kutueleza Watz kilichofichika ndani ya mioyo yao, ndio siku mabadiliko ya kweli yatakapotokea, maana tutajua maswali yote ya WHAT? WHO? WHY? WHEN? HOW? hayo yakijibiwa tutapata a way forward!
 
Back
Top Bottom