Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

Lowassa: Wakimwaga mboga namwaga ugali

Ndugu Wana JF,

Haya maelewano na vikao vya siri baina ya makamo mwenyekiti wa CCM na watuhumiwa wa ufisadi je kunatoa picha gani juu ya uwezo, ujasiri na nia ya dhati ya kupambana na ufisadi ndani ya chama cha mapinduzi.

Soma hapa chini habari kamili kutoka gazeti la Habari leo la jana,

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, amekutana na viongozi watatu wa chama hicho wanaotuhumiwa kwa ufisadi, katika utekelezaji wa uamuzi wa kujivua gamba uliofanywa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) uliofanyika Dodoma Aprili 10 hadi 11, mwaka huu.

Yaliyozungumzwa katika kikao hicho yameelezwa kuwa siri kati ya Msekwa na watuhumiwa hao, Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge, lakini yalihusu agizo walilopewa watafakari, wajipime na kuchukua hatua wao wenyewe kwa masilahi ya CCM, la sivyo wawajibishwe na chama.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM mjini Dar es Salaam, ilisema Msekwa
alikutana na viongozi hao kila mmoja kwa wakati wake na kuzungumza nao kwa faragha kama Makamu Mwenyekiti wa CCM na kama mzee wa chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Msekwa alikutana na viongozi hao Mei 26 mwaka huu na wa kwanza alikuwa Rostam ambaye ni Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Igunga. Walikutana saa 2.30 asubuhi.

Baada ya hapo kwa mujibu wa taarifa hiyo, alifuata Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu, Mbunge wa Monduli na Mjumbe wa NEC na wa mwisho alikuwa Chenge, Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Bariadi Magharibi.

“Kwa vile Msekwa alikutana kwa faragha na viongozi hao mmoja mmoja, anayejua kilichozungumzwa ni Mzee Msekwa na wao peke yao,” ilisema taarifa hiyo ya CCM.

Gazeti hili lilizungumza na Lowassa, kutaka kujua kama alikutana na Msekwa na kama atachukua uamuzi wa kujivua gamba kama maagizo ya NEC yanavyotaka lakini baada ya kusikiliza hoja hizo, alijibu “No comment.”

Alipotafutwa Rostam, simu yake ilipokewa na msaidizi wake ambaye hakutaka kujitambulisha
jina, akasema Mbunge huyo yuko nje ya nchi na ameacha simu kwake. Chenge simu yake iliita bila majibu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua itakayofuata baada ya mazungumzo hayo ni kufikisha
kwenye vikao vya CCM taarifa ya mambo yaliyojiri wakati wa mazungumzo hayo na vikao hivyo vitatoa uamuzi utakaotangazwa kwa umma.

CCM pia imekanusha taarifa kwamba viongozi hao walipokutana na Msekwa walikabidhiwa
barua za kuwataka wajiuzulu na zile zilizodai kuwa barua hizo zimefungiwa kabatini na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

“Taarifa zote hizo zilizoandikwa na kutangazwa katika vyombo vya habari, si za kweli, ni uongo na uzushi mtupu. Hakuna barua iliyoandikwa, hakuna aliyepewa barua na wala hakuna barua iliyofungiwa kabatini,” ilifafanua taarifa hiyo.
 
Hivi Msekwa bado ni board member wa VODACOM? If yes, huoni itakua vigumu sana kupingana na Rostam kwenye kitu chochote watakachojadili? Naona CCM wameshamalizana sasa hamna barua wala nini. Ok lets wait and see.
 
Ccm wanawadanganya wa tz. Ila kuna mwezi uzao huu utasema hapana mmetudanganya vya kutosha, tunataka nchi yetu. Na hapo itakuwa kilio na kusaga meno kwa watawala wote.
 
kipande hiki cha habari ndo kinadhihirisha kujivua gamba ni usanii kama CCM imefikia hatua ya kuwapigia magoti RACHEL! Mhhhhhh...........

Nanukuu

"CCM pia imekanusha taarifa kwamba viongozi hao walipokutana na Msekwa walikabidhiwa
barua za kuwataka wajiuzulu na zile zilizodai kuwa barua hizo zimefungiwa kabatini na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

"Taarifa zote hizo zilizoandikwa na kutangazwa katika vyombo vya habari, si za kweli, ni uongo na uzushi mtupu. Hakuna barua iliyoandikwa, hakuna aliyepewa barua na wala hakuna barua iliyofungiwa kabatini," ilifafanua taarifa hiyo.
 
Narudia kusema kuwa Wanatudanganya kwakua tumewadokeza ! Wanadhani sie bongo lala. . . Hapana wakati umepita kwakasi , lazima wachanganyikiwe.
Mungu mwema , wanaumbuka, wanaumbuana , mahayawani hawa watakufa kibudu siku moja. MAGEUZI HAYAKWEPEKI.
 
Wana ogopana lakini sisi wananchi kwa hasira iliyo njema kabisa tuta waonyesha kwa vitendo 2015
 
Sasa ni dhahiri ili CCM kurudisha imani kwa wanachama na wananchi ni kuwatumia Mapacha watatu kama hoja ya kuwakutanisha na wananchi as if ni Lowassa,Chenge na Rostam tu ndio kiini cha shida na taabu za Watanzania.Je taabu hizi na matatizo haya yataisha pindi RACHEL watakapotoswa? Na kwa sababu RACHEL wametoswa basi hakuna haja ya kubadilisha chama bali CCM iendelee kutawala? Je ni kweli RACHEL ndio uozo pekee ndani ya chama na serikali yake? Tafakari!
 
Hilo nalo neno. Hivi huwa najiuliza Kikwete na wenzange wana usafi gani mpaka wao waendelee na nyazifa zo?
 
Hao mapacha watatu ni mzao wa mfumo mbovu wa kiutawala ulioanza wakati wa BMW. Hawa jamaa wajiimarisha kipesa kiasi kwamba wamehonga vikaragosi wengi tu ndani ya CCM.
Wakitoswa na chama kinakufa pia hivyo Tz inapata uongozi mpya wa kuleta maendeleo kwetu.
 
Walikubaliana kuwa huo ni usanii tu na washirikiane kujenga chama kwani watanzania wengi bado ni mbumbumbu na hivyo ni kazi rahisi kuganganyika et kuwa wachache wanaojua abcd wapo mijini tu!

Ndio maana wameelekeza nguvu zao vijijini kuanzia Sumbawanga, Mpanda, Vijiji vya Mugumu nk. Kama utakumbuka bango la Nape la Mpamba wameweka wazi kuwa Ufisadi kwa CCM sasa si tatizo tena na wamekuja na kauri mbiu kuwa Fisadi ni mtu binafsi na anaweza kuwepo chama chocho cha siasa! hii ina maana kuwa waachiwe mafisadi wao.
 
Basi mimi hio "Title" peke yake ndio imenitisha sana; nikajua sasa huyu Mzee anataka awafanyeje wenzio kumbe aaaahh ni mambo yao ya kutuibia sisi wanyonge, pambaf kabisa.
 
Narudia kusema kuwa Wanatudanganya kwakua tumewadokeza ! Wanadhani sie bongo lala. . . Hapana wakati umepita kwakasi , lazima wachanganyikiwe.
Mungu mwema , wanaumbuka, wanaumbuana , mahayawani hawa watakufa kibudu siku moja. MAGEUZI HAYAKWEPEKI.

wanaahirisha mda tu, mageuzi yapo pale pale.
 
Tungekuwa na Lowasa (as PM) tungefika mbali kimaendeleo.
 
Hiyo ndio CCM ninayoijua mimi....
Chini ya Mwenyekiti ninayemjua mimi...
Wamejivirngisha wee sasa ni hawawezi kutoka tena...
Bado huyo muimba pambio wao Nape, na hadaa anazoziendeleza..
 
Saturday, 04 June 2011 10:17

chenge21.jpg


Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge

Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimethibitisha kwamba kimewahoji Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ikiwa ni moja ya hatua ya kutekeleza maazimio ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho uliofanyika Aprili 10 hadi 11 mjini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Willison Mukama ilisema kuwa hiyo ni moja hatua za awali zilizochukuliwa na kuongeza kuwa nyingine zitafuata baadaye.

Alisema hatua hiyo ya awali, Makamu Mwenyekiti CCM (Bara), Pius Msekwa alikutana na wanaotajwa katika tuhuma hizo katika sura mbili, kwanza ya nafasi yake ndani ya chama na pia kama mzee wa CCM.

Mukama alisema Mei 26, mwaka huu Msekwa alikutana na Rostam ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na siku Iliyofuata alikutana na Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

Alisema siku hiyo hiyo ya Mei 27, mwaka huu alikutana na Mjumbe mwingine wa Halmashauri Kuu, Chenge."Kwa vile Msekwa alikutana kwa faragha na viongozi hao mmoja mmoja, hakuna anayejua kilichozungumzwa. Ni Mzee Msekwa na wao peke yao," alisema katika taarifa hiyo.

Alisema hatua itakayofuata baada ya hapo ni kufikisha kwenye vikao vya chama taarifa ya mambo yaliyojiri wakati wa mazungumzo baina ya Msekwa na viongozi hao."Endapo vikao husika vitaamua lolote kuhusiana na taarifa hiyo, umma utajulishwa," alisema.

Katika mkutano huo wa Halmashauri pamoja na mambo mengine, uliwataka viongozi wa CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi kutafakari, kujipima na kuchukua hatua wenyewe kwa maslahi ya chama na kwamba wasipofanya hivyo chama kitawawajibisha.
 
Hakika kwa kiongozi kushindwa kutekeleza maamuzi ya kikao ni udhaifu Mkubwa unaokuondolea sifa ya kuwa kiongozi. Haya mambo ya kuhujiana yanatokea wapi???? Eti Mzee wa Chama kwani ameambiwa hawa waheshimiwa sana wanataka kwenda kuoa? Hakuna mambo ya uzee katika utekelezaji wa maelekezo ya kikao halali
 
Back
Top Bottom