Natamani sana kupewa ushahidi kwamba lowasa ana mali nyingi sana na anaccount nje na ni mwizi wa mali ya umma.
Tamaa yangu inatokana na sababu nyingi, na nyingine ni za kihistoria ila sababu kubwa ni kwamba sitaki kuingia kwenye dhambi ya kuhukumu bila ushahidi.
Wakati kambona anarejea nchini baada ya mfumo wa vyama vingi kufika nchini, mchungaji mtikila na wakina Fundikira. RIP. walituaminisha kuwa Kambona atatuletea ushahidi wa account za Mwl Nyerere alizokuwa nazo huko ulaya na watahakikisha pesa hizo zinarudishwa nchini. Waandishi walimwandama sana Mwl ajibu hizo hoja. Mwl akawaambia muulizeni aliyesema mpaka awape ushahidi na Mwl hakujibu ama kwa kukanusha au kukubali. Leo kila mmoja anaujua ukweli.
Wakati wa kumpata mgombea wa CCm 2005, Wanamtandao walituaminisha kuwa Dk Salim A Salim, ndiye aliyemuua Karume na Wazanzibar wakaamua kumpa Jk kura zao, wakasahau kabisa swala la zamu ya bara na visiwani, kwa sababu waliaminishwa vyema kwamba Dr ni Muuaji wa Kiongozi pendwa kwao. Omarilyas unalijua hili vizuri. Leo hii Kila mmoja anaujua ukweli.
RAISI AJAYE ATAAMULIWA NA WATANZANIA KUTOKANA NA UZURI WA SERA NA UWEZO WA KUSIMAMIA SERA ZA CHAMA CHAKE, NA KAMWE HAWEZI KUAMULIWA KWA PROPAGANDA ZA UFISADI, WIZI, UMALAYA NA MENGINEYO YASIYOKUWA NA USHAHIDI.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.