Lowassa, Pesa unazozitumia hivi sasa utazirudishaje?

Lowassa, Pesa unazozitumia hivi sasa utazirudishaje?

Akiingia ikulu watz tutakamuliwa mpaka tone la mwisho la damu maana jasho letu halitatosha kurudisha mtaji alioutumia kuingia ikulu. NOTHING GOES FOR NOTHING hiyo pesa anayoitoa anaiwekeza na lazima itamzalishia maradufu.
Nawashangaa sana watu ambao wanashindwa kujiuliza na kuling'amua hili.
Ha ha ha ha ha ha langu jicho wakuu make hii hali inatisha.
 
Lowasa anajua watanzania wana njaa kali na ni watu wa tamaa ya kuganga njaa ya siki kwa siku...Mbinu aliyo tumia kumuingiza JK ndiyo hiyo anayo tumia kuingia...Tatizo watanzania wengi ni vichwa maji...na kama ikishindikana uchakachuaji kama kawaida...
 
Sikilizeni niwambie, Lowasa alikosa busara ndogo tu, alidhani akitoa pesa yeye kama yeye zitamsaidia kujisafisha kumbe ndo kaongeza uchafu kwenye majeraha yake.kama ni kidonda kitakuwa ni ( septic wound) kinachihitaji Tiba ya kina.

Angegawa pesa zake kwa kujificha nyuma ya chama chake huku akisema chama chetu kimetoa pesa kadhaa yasingemkuta haya yote. Huyu mtu ni fisadi hafai jamani puuuuh!!
 
Lowassa amewaibia fedha wananchi,watakao zilipa ni wananchi haohao walioibiwa.
 
Kama kweli una Phd bila shaka itakuwa ya ZOOM College........ mumeshikwa pabaya safari hii na Jk kasema hambebi mtu hata kidogo
kama huuziki kama membe is up to you and him......

Wewe una elimu gani? Maana hii jf mtu form 4 leaver anaweza kuhoji phd ya lupumba ili mradi yeye ni ccm
 
Binadamu siku zote hufanya mahesabu kabla ya kufanya jambo lolote lile. Hakuna binadamu anayefanya jambo ilimradi tu, ukiona binadamu anafanya jambo ujue ana mategemeo fulani.

Kuna dalili zote kuwa ndugu Lowasa anataka kugeuza uraisi ni biashara. Kwamba ukiwa na mtaji wa laki mbili baada ya biashara kufanyika utakuwa na laki tano.

Lowasa, hizo pesa unazozitumia utarudisha vipi?

Nikipata majibu ya kuridhisha ya hili swali nakuhakikishia kukupa kura yangu pamoja na watu wote wanaonizunguka.

Hizo pesa utazirudishaje?

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)

Keneth Matiba wa Kenya aliishia wapi na pesa zake katika kuusaka uraisi wa Kenya? Mungu atatupa kiongozi bora tuwe na subira na tuache maneno mengi
 
Sio lazima niwe nimeumia au niwe mchaga, nilivyosoma post sikuweza kujua aliyepost ni kabila gani, sasa vijembe, kejeli na matusi vimeelekezwa kwa 'wachaga' tena wote! na sio huyo mmoja aliyepost, so, nimeshangazwa zaidi na kuhisi huyo ana kijiba cha roho na wachaga. Na wewe ni mmoja wao?

Najua ulielewa sema ukilaza ndo unakusumbua!!sjazungumzia wachaga kama kabila.mwone ulivyo mkabila.yaaan unawaza ukabila tu.shame on u!!
 
Lakini jamani wapiga kura si ndo sisi hapa,let us play our part kwa kuwafungua macho hao wanapofushwa macho na hizo pesa za EL!
 
Fanyeni kazi zenu acheni kujadili kuwa Lowassa katoa wapi fedha anazozitumia hivi katika hizi harakati ni lowassa pekee ndo anatumia pesa mbona hamuulizi hao akina mizengwe punda, maembe na January watazirudishaje...
 
Lakini jamani wapiga kura si ndo sisi hapa,let us play our part kwa kuwafungua macho hao wanapofushwa macho na hizo pesa za EL!
Naungana na wewe kumchagua lowasa ni sawa na kuchagua kitanzi cha kutunyonga kwanza mwizi,anaroho mbaya nenda monduli utashangaa wanamuogopa siyo kumheshimu ukihoji kuhusu Lowasa utapata matatizo makubwa sana.
 
hili ndo tatizo la watu wenye akili ndogo.kutwa hukaa kumjadili mtu.yaaan ni aina za tabia ambazo ni za kike kike.hivi mbna hamuwahoji hapo wengine wanaotoa misaada kila siku kua watarudishaje??hivi lowasa pekee kutoa msaada ndo imekua habari ya mjini???mbna haujahoji amezipataje???wachaga umbea na kuchafua chafua watu kama mwanamke malaya aliekimbiwa na bwanake.mnakela sana.kila siku lowasa lowasa.ngoja aingie ikulu mtaenda kuishi uamishoni somalia..time will tell na mtajibeba!!

nitajie mwingine nchi hii aliyetoa rushwa ya bil 7 ?
 
lowasa akiwa rais nitajiunga rasmi na kina kiranga na nyani ngabu kutoamini uwepo wa mungu maana huyo atakuwa mungu kanjanja tu na mimi siwezi kuabudu kanjanja anayeweza kubaliki mateso kwa viumbe wake, maana tumeaminishwa mungu ni muweza wa vyote. Mimi namsubili ajidhihirishe.
duh!
Eeee bhana eeee !
 
Last edited by a moderator:
Kama kweli una Phd bila shaka itakuwa ya ZOOM College........ mumeshikwa pabaya safari hii na Jk kasema hambebi mtu hata kidogo
kama huuziki kama membe is up to you and him......

siku zote sikujua kama wewe ni team lowasa ! Hebu tusaidie mkuu hizi hela za watu mnazogawa mtarudishaje ?
 
Back
Top Bottom