Lowassa: Nitadhibiti rushwa kwa siku 100

Lowassa: Nitadhibiti rushwa kwa siku 100

Mafisadi kama Home shopping centre, Escrow, Richmond, Meremeta, Kagoda, zile Bl 8 za TCRA, waanze kukimbia mapema. Kiama kimefika, bado siku 27 tu

na waliojilimbikizia mashamba makubwa,wenye kuhifadhi pesa ughaibuni.
 
Ishu sio kuziba mianya bali kuyafunga mafisadi.Magufuli ameshaweka kibano cha Mahakama ya mafisadi.Magufuli anaeleweka ndie Rais
 
Kwakweli bora tu wakomeshe kuna wafalme wao hawalipi kodi kontena zapita buree umshikishe wakala tu umepeta khaa tumeibiwa sana na sasa baaasiii na hii haitoshi wakamatwe wapukutishwe kodi zoote walizokwepa ikiwezekana wafilisiwe hadi nguo watembee uchiii
 
Magufuli hawezi sasa si atawafunga ccm nzima hahaha hayo maneno tuu aisee magufuli usitudanganye mana haoo wooote unao ambatana nao kwenye kampeni ni mafisadi wala rushwaaaa sasa itakuaje kama si danganya toto lowasa anaweza kufanya hivyo mana hayupo tena kwenye kampuni ya mafisadi wanyanganyi ccm
 
Ishu sio kuziba mianya bali kuyafunga mafisadi.Magufuli ameshaweka kibano cha Mahakama ya mafisadi.Magufuli anaeleweka ndie Rais

sasa unafunga watatu alafu chama hichohicho na kwa mianya hiyo hiyo wanazaliwa mafisadi 100 utakua umefanya nini?
 
Matusi ndio jadi yenu ccm fungua kichwa mkuu unajidhalilisha

Una upeo mdogo kiongozi. Umeanza wewe, nimekuambia ukweli, sasa unakuja na hoja urojo. Nani kasema mie ccm, unaona hata kufikiri kidogo tu ni tatizo!!!
 
Katika watu wa Hovyo wewe ni No.1
Je? Baada ya kuondoka Lowasa ccm Rushwa na Ufisadi umeisha?
Kama ndiyo.
Je? Chenge, Mwambalaswa, Prof. Muhongo, Prof. Tibaijuka, Ngeleje na Mkapa Kiwira si Mafisadi na Wala Rushwa?
Kama ndiyo.
Je? ilikuwaje wahusishwe na Escrow na Kiwira?
Je? Kwanini Magufuli anahusishwa na Ufisadi wa kuhonga Nyumba?
Je? Bado unaimani na CCM au ni sehemu ya wanufaika?

Nnaona utaanza kuielewa dhanna ya kuvuwa gamba tartiiiiibu.

Lowassa yuko wapi? Kumbuka na bado kuna kesi zinamsubiri, tunangoja mambo ya uchaguzi yaishe.

Mramba yuko wapi?

Yona yuko wapi?

Na wengi zaidi pitia tovuti ya PCCB utawakuta huko kwa maelfu.

Hayo ndiyo mabadiliko tuyatakayo, tumeona Kikwete akiyaanza na sasa tunasubiri Magufuli ayaendeleze kwa kasi kubwa sana.

Misingi kishawekewa sasa yeye ni kujenga tu.

#HapaKaziTu
 
Una upeo mdogo kiongozi. Umeanza wewe, nimekuambia ukweli, sasa unakuja na hoja urojo. Nani kasema mie ccm, unaona hata kufikiri kidogo tu ni tatizo!!!

Haha haha unajikana wwe mwenyewe OK jumapili njema
 
.... ndani ya siku 100!! Tena kama atapewa ushahidi!! Ina maana kina Tundu Lisu hawajampatia ushahidi bado?
 
Na hiyo technologia ipo sana tu.... Thailand wanaitumia, Ufaransa kaskazini na hata Benin wanatumia hiyo technolojia..... CCM wamefanya watu kuwa wajin.ga sana, yaani hata vinavyowezekana wenyewe wanona kama haviwezekani

Hapo kwenye;vinavyowezekana wenyewe wanaona kama haviwezekani nakubaliana na wewe mkuu!kama Elimu kuwa bure na vivuko kuwa bure.
 
Elewa ujumbe. Atadhibiti maana yake zote zitakuwa zake. Hatakubali deal zichukuliwe na wengine.

Nakuona Daktari mwenye PhD katika ubora wako.... Vipi Magamba hawajakupatia nafasi ya kugombea ubunge jimbo lolote!?
 
Iwe Lowassa, iwe Magufuli... Seriously tunahitaji hizi rushwa zitokomezwe.
Tunaweza kuongea kwa ushabiki wa vyama lakini beyond vyama vyetu tunahitaji nchi yenye maendeleo.
Haiwezekani miaka yote tunateseka na matatizo yale yale tu... maji, dawa, chakula, umeme... hadi lini?

Tuko;
Hadi utakapo chagua UKAWA kwa mabadiliko ya kweli. Msikilize asemaye kuwa atamaliza huu wizi. Fedha yoote ya maendeleo inaingia mfukoni mwa familia moja tuuu. Jamani, fungukeni.
Kama hatafanya hivyo, tunampiga chini
 
tutapitia upya mikataba ya bandari.madini,gesi,ndani siku mia nchi yetu itakuwa inakimbia kiuchumi
 
Katika watu wa Hovyo wewe ni No.1
Je? Baada ya kuondoka Lowasa ccm Rushwa na Ufisadi umeisha?
Kama ndiyo.
Je? Chenge, Mwambalaswa, Prof. Muhongo, Prof. Tibaijuka, Ngeleje na Mkapa Kiwira si Mafisadi na Wala Rushwa?
Kama ndiyo.
Je? ilikuwaje wahusishwe na Escrow na Kiwira?
Je? Kwanini Magufuli anahusishwa na Ufisadi wa kuhonga Nyumba?
Je? Bado unaimani na CCM au ni sehemu ya wanufaika?

Naona hii post imerudiwa kama mara kumi na anayetoa like ni yule yule.Halafu mnawalalamikia mods
 
Waziri Mkuu mstafu na mgombea wa umoja wa Ukawa Ndg. Edward Lowassa katema cheche na kusema Ukawa wakipewa ushindi, ndani ya siku 100 ataziba mianya yote ya rushwa, ufisadi akianza na bandarini ambapo zaidi ya Billioni 21 upotea kwa siku..

Lowassa kasema kuwa serikali ya Ukawa itakuwa na wajibu mmoja tu, ambao ni kutoa huduma iliyobora kwa wananchi na kwa wakati. Hiyo ndio serikali ninayotaka kuiona, na hayo ndio mabadiliko wanayoyataka wananchi. Hili litaendana na kuziba mianya ya rushwa, na nawahidi ndani ya siku 100 mianya hiyo itazibwa.... Alisema

Kwa hii hatua na kauli ya Lowassa ni wazi wananchi wanaelekea kufaidi matunda ya nchi yao, na sio kikundi kidogo cha watu.. Hatua kama hizi zilifanikiwa sana Singapore, Malaysia, Taiwan na Korea Kusini.. Na hata Rwanda baada ya Kagame kuingia ndani ya siku chache alifanikiwa kuthibiti rushwa, ufisadi na aina zote za dhuluma...

Mytake: Nafurahi kuona serikali ya Ukawa kutupeleka katika speed ya maendeleo kama Singapore, Korea Kusini au Malysia....

je baada ya siku 100 rushwa iendelee??
 
Back
Top Bottom