We Ocampo kwa nini unadanganya kile ambacho Lowasa kakisema na tulikisikia wenyewe! Hata hilo gazeti la rafiki yake (Rostam) ie Mtanzania halikuandika hivyo!
Gazeti hilo limeandika: 'Ndani ya siku 100 atapambana na rushwa kwa kuanzisha kituo kimoja kila wilaya kitakachotoa huduma zote za serikali - yaani one spot services center'.
Aliongea sentensi hiyo moja tu kuhusu swala la rushwa kama kawaida yake na gazeti hilo limejitahidi kuinukulu vyema bila kuongeza longo longo kama wewe unavyofanya hapa!
Sasa wenye akili timamu wanajiuliza: Hicho kituo kimoja kitakachotoa huduma zote za serikali kinawezekana kweli? Yaani kituo hicho kitoe huduma za matibabu, za kimahakama, za usalama wa raia (polisi, traffic), TRA, tanesco, ardhi na huduma zote zingine zitolewazo na idara na tasisi zote za serikali zilizokithiri kwa rushwa; inawezekana? Kwa mfano pale Muhimbili Hospital kitoe huduma za moyo, mifupa, magonjwa ya akili nk. Hata kama kingekuwa paying center hakiwezi kuondoa rushwa. Rushwa na ufisadi ni suala complex na liko nchi zote duniani isipokuwa labda Vatican. Limekuwapo tangia kuumbwa kwa Mwanadamu. Huwezi ukalimaliza kwa simple thinking ya aina hiyo wala kwa kimiujiza miujiza.
Ocampo tambua kuwa tunatafuta Rais wa nchi na si rais wa chama cha siasa. Tunatafuta Mkuu wa nchi na Amiri Mkuu wa Majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania si wanachama wa chama cho chote cha siasa, mimi nikiwa mmoja wao. Tuache ushabiki usio na tija kwenye suala hili mhimu kwa taifa letu. Kampeni si kudanganyana na kusema uwongo. Watanzania watawapima wagombea kwa weledi wao wa kujenga hoja na mikakati thabiti za kutatua matatizo ya wananchi. Watawapima kwa uadilifu wao na uchapakazi wao nk