Msituaminishe ujinga ninyi CCM, mngekuwa mnajua mna nafasi kubwa yakupita katika Uchaguzi huu msingetumia Nguvu nyingi kiasi hiki.
Kukodi akina Mtikila na Startv kupiga kampeni ya kumuangusha Lowasa.
Lowasa anaweza, CCM na mafisadi wanajua kuingia kwa Lowassa ikulu nikuwapolezea mbali mafisadi na kuziba mianya ya wizi wao.
kama ingekuwa ccm wanamkataa Lowassa kwasababu wanaipenda nchi hii KIKWETE narudia BWANA JAKAYA MRISHO KIKWETE asingekaa hadharani kutuaminisha pesa ya Escrow si pesa ya Serikali.
CCM na watu wake, wangetuambia Akaunti za Stanibic ambazo hazina majina ni za nani? Mnatuambia Lowasa ni Mwizi? Vipi escrow pia kaiba yeye? Na vipi hizo akaunti pia moja ni ya Lowasa? Kama ni zake tajeni leo. Kama sio basi wenye akaunti wako CCM hadi sasa.
CCM wanawadanganya wajinga wachache sana hapa Tanzania, uwezi kutuambia Lowasa ndie ametufikisha hapa tulipo wakati miaka 8 baada ya kuachia madaraka bado nchi ina kashifa kubwa na ambazo zimetetewa hadi na Rais Jakaya Mrisho Kikwete mmoja wa Washauri wa kikwete ni MAGUFULI mgombea wa ccm kupitia baraza la MAWAZIRI.
Ni bora kuishi na mchawi mmoja kuliko kuishi na wachawi kumi watakaokuwa wakikuwangia kwa Zamu.
Nasema ni bora kuishi na mwizi mmoja kuliko wezi 20 ambao watakuibia kwa zamu kila uchwao.
Kashifa za LOWASA haiwezi kuwa kigezo cha kusema CCM inafaa, au haitoi kibali cha CCM kuwa watakatifu. basi tuambieni Lowasa hafai na Magufuli hafai... Kisha mtupatie anaefaa, lkn kama ni kusema LOWASA hafai kisha CCM iendeleee ni UJINGA tena ujinga uliotukuka.
Hatuwezi endelea kwa mtindo huu, LOWASA atafanya MABADILIKO nchi hii, akishindwa miaka mitano mpk kumi tutaondoa utawala wao, lakn kuikumbatia CCM eti kwasababu lowasa alijiuzulu kwa kashifa ni UJINGA.
Kwani huko CCM kinana si anatuhumiwa kwa biashara ya MENO ya TEMBO kaondoka CCM?
Huko CCM kikwete na Familia yake wanatuhumiwa kwa kujitwalia UKWASI mkubwa na hawakanushi mpk leo, hao familia yake si ndio viongozi hadi sasa?
Na baba anaendelea kuwa mwana ccm, tena mwenyekiti wa CCM au anaondoka ccm ili tuwaone ni wasafi kuliko Lowasa!? Au anakuja CHADEMA ili tuseme mafisadi wameamia CHADEMA?
Huko CCM chenge si ana kashifa za Rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, KAONDOKA?
MAMA tibaijuka si anatuhuma za mgao wa kashifa ya ESCROW, kahama ccm Ili tuione ni safi kuliko uchafu wa anaeitwa Lowasa?
MAGUFULI ripoti ya CAG imetuhumu wizara yake kwa ubadhirifu wa mabilioni ya fedha. Keshajibu? Kasema zilienda wapi?
Magufuli anatuhuma za kununua kivuko chakavu kwa pesa nyingi tofauti na thamani yake halisi. Huo ni utakatifu kuliko uchafu wa lowasa?
Hapa sigusi tuhuma za kuuza nyumba kwa mpenzi wake asie mfanyakazi wa serikali lkn nizungumzie hili, kama udhaifu wa magufuli kikazi..
Magufuri ndie aliepiga kelele Tanesco ibomolewe kwakuwa ipo barabarani lkn alinyamazishwa na alitii sauti ya Bosi wake.
Magufuli alizuia malori mazito yasipite katika barabara yakiwa yamezidi uzito, sawa hapa alisimamia sheria lkn Mh mizengo pinda akasema hapana, magufuli akanywea. Hapa nauona udhaifu na uoga wake.
Kama angekuwa na credibility ya utendaji na usimamiaji wa sheria kwa watu makini magufuli angejiuzuru lkn alitii sauti ya Mafisadi wenye malori barabarani.
Sasa leo ndio magufuli ataweza kusimamia kile anaamini? Nimesema kinana ambae ni katibu mkuu wa CCM anatuhuma mitaani za kuwa katika biashara ya meno ya TEMBO, magufuli anaweza mfikisha mahakamani kinana kujibu tuhuma? Wakati huyo ndie anaemnadi na kuzunguka nae nchi nzima katika kampeni?
Kama Kikwete inadaiwa alikuja na Majina matano katika mkutano mkuu likiwepo la magufuli, je kesho akiwa Rais, Magufuli anaweza chunguza tuhuma za ufisadi za familia ya Kikwete? Atawezaje atuambie.
Anasema ataanzisha mahakama ya Mafisadi na Majizi, sawa, Tunakubali anamlenga Lowasa, tukubali lowasa atafungwa na kukutwa na hatia.
Je iyo mahakama itakuwa ya lowasa pekee? Wenye tuhuma kama chenge, kikwete, tibaijuka, mwakyembe, na wengine wengi Magufuli atuambie atawashikia wapi, atawafikishaje? Na atawezaje ikiwa anao ndani ya CCM na ndio wanabeba kampeni zake. Au iyo mahakama ni kwaajili ya Lowasa pekee?
Maana bila shaka akianzisha iyo mahaka atapaswa serikali yake yote iwe mahakamani akianza na yeye na wanaompigia kampeni hadi leo.
Ukweli unabaki hatuwezikataa LOWASA ili CCM ibaki madarakani iyo nikujiibia pesa kushoto na kuweka mfuko wa kulia na Kujisifu eti mimi ni mwizi bora. (kwa wale wanaodhani lowasa kuitwa fisadi ni nafuu ya kuwapa nafasi CCM walikojaa wezi) waendelee kutawala. NI UJINGA NA UJINGA MKUU.
WATANZAIA mnaomkataa Lowasa, tupatieni mbadala wa Lowasa (Chadema) mbali na (CCM) na Magufuli.
Lakn kama hakuna mbadala wa CCM na magufuri anapokataliwa Lowasa na CHADEMA . MIMI NASEMA, BORA lowasa na CHADEMA mara elfu, kuliko CCM na mtekenyaji wake anaebeba NDOTO hewa MAGUFULI.
BORA KUISHI NA GONJWA MOJA UTAKALOTIBU KWA AMANI KULIKO KUISHI NA MAGONJWA MIA KATIKA MWILI MMOJA. UTAKUFA TU
LOWASA KUITWA FISADI SI NAFUU YA CCM KUENDELEA KUAPATA HAKI YA KUIIBIA NCHI HII.