LOWASSA ni tishio

Ukisema Mufti Mkuu ni tishio sitakuewa. Ukisema Mufti Mkuu ni tishio kwa amani ya Watanzania ndipo nitakapoelewa. Sasa Lowassa ni tishio kwa vipi?
 
Huku ni kuhamisha attention ya wachangiaji na huu ni mpango mahususi wa mafisadi. Mufti ameingiaje humu? Tanzania hii public enemy number 1 ni LOWASSA!
 
fataki data zako ni za kifataki. They are not true. Hata ulivyoandika tu bado umechakachua. Kama kitu hujui usiandike
mimi siungi mkono ufisadi bali pia siungi mkono uchafuzi kwa kutumia uongo
tunaomba data kwamba lowassa kachukua shs ngapi na wapi
tumesoma akina chenge na rada, akina manji na kagoda, akina ra na deep green
hebu tuache unafiki tuseme kile ambacho mtu amechukua na tuwe na records kama zingine vinginevyo tunapiga kelele ambazo hata kwa mwananchi wa kawaida huwezi kumwambia huyu mtu mbaya.
Watu wote waliochukuwa fedha za umma wameandikwa sana na wote sasa hivi wala hatuwasemi kila siku tunapoteza muda kwa lowassa
kama vipi huyu mtu tumpotezee lakini siyo kwa maneno ya giliba yasiyo ya kweli maana kwa hilo hakika twatenda dhambi sisi weneyewe na itaendelea kututafuna
huyu mzee mnamwekea maneno mdomoni kila siku, kwanini hayo makombora mliyonayo msiyaweka tuyatoe wakati ukifika akisema anataka urais
kwani kama yeye ni mbaya na ccm ikamsimamisha si ndiyo vizuri kwa chadema, cuf au nccr mageuzi ili tuinyang'anye ccm hati miliki ya utawala wa tanzania?
Hebu tuongeleeni tunayotaka kikwete na serikali yake watufanyie sasa watanzania, maana kwa njia moja au nyingine maneno yatamfikia tu, watu wake wa tiss ambao wamo humu ndani watamfikishia na itatusaidia!!

...Za kwako za Kweli zi Wapi?

 
Siyo sikio la kufa mkuu. Huyu na wapambe wake ni watu wenye ufinyu wa kujua sentiments za watu na kudhani kwamba utajiri wao haramu utawafikisha kwenye utukufu na ndiyo maana hawaishi kuleta thread za kuchokonoa na kupima upepo humu JF. Ndiyo maana mtu na akili zake anaweza kuibukia humu akidai kwamba Lowassa hana hatia na kwamba alijiuzulu kuiokoa serikali wakati tunajua kwamba hakuwa na hoja za kutetea aliyoyafanya pale mjengoni. Jamaa huyu hajawahi kukutana na changamoto zozote za kupima uwezo wake wa kujieleza au kujenga hoja na ndiyo maana huwa anaogopa kuwakabili hata waandishi wa habari wa ndani na nje zaidi ya wale wa Habari Corporation au magazeti aliyoyanunua kama Tanzania Daima ya akina Kibanda, Katabazi na Mullinda.

...EEEeeeh??? Kumbe ameishalinunua na Tanzania Daima??? Nilidhani alikuwa amenunua baadhi ya waandishi tu kama yule Mzee wa ukurasa wa kati wa toleo la Jumatano ambaye hawezi kuandika makala bila kusifia utendaji kazi mzuri wa Lowassa! Katabazi? Mullinda? Whew!
How Sad. There goes one of my very few favorite newspapers....!
:noidea:
 
naunga mkono hoja,na ndio anayewatia homa CDM,na ndio maana cdm wakilala wakiamka ni lowasa,huyu jamaa akisimama chadema chali coz lowasa anajua siasa za kisasa,ni msomi na ni msikivu na si mropokaji kama padri slaa! sasa wanachofanya cdm ni kumchafua kwa kashfa ambazo hawawezi kuthibitisha,wanabase kwenye rumours only! cdm need to be realistic with people na waambie sera zao na mipango yao,politics of critizing others imeshapitwa na wakati!

Acha kuwa Mjinga.
 
UMEKATIWA NGAPI NA HUYU RA?


rostam_234.jpg

Nashindwa kuelewa mtu mzima anasikia utamu gani kwa kuweka kidole puani!
 
Lowassa atawahonga mpaka dakika ya mwisho jina lake litaenda Kamati Kuu.. Majina matano (5) hatopita. Watamchuja Central Committee. Majina matatu yataenda NEC Lowassa, KWAO.. Ubaya kawanunua na TISS kwahiyo mmh! SIjui itakuwaje..
 
Nimekuwa nikifuatilia sana vyombo vya habari vinavyopinga Lowassa(Mwanahalisi na Raiamwema) na vinavyo msapoti(Rai na Mtanzania). Nimefuatilia sana wanasiasa wanaompinga na kumsapoti. Mwisho nimebaini kuwa Lowassa ni tishio kubwa kwa wanaoutaka urais wa muungano ndani ya chama chake na kwa upande wa upinzani. Ana nguvu kubwa sana serikalini na katika chama. Ni bingwa wa kuratibu mtandao kisomi. Ni mtendaji na haogopi. Na iwapo ataamua kugombea, hatakuwa na mpinzani mwenye nguvu ndani ya chama chake na hata ktk uchaguzi mkuu. Sote tumeshuhudia jinsi alivyoweza kuukwaa uenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama bila mtu yeyote kutia mguu kumpinga. Na sasa tumeshuhudia jinsi anavyopata sapoti kutoka kwa Mhe Beatrice Shelukindo na mumewe William Shelukindo. LOWASSA NI TISHIO

Najiuliza kwa nini iwe hivyo kwa mtu ambaye amejiuzuru kwa fedheha kiasi hicho! mtu ambaye amekuwa madarakani siku nyingi bila mafanikio kwa nchi tunayoweza kuyakumbuka.

Wale muliouliza ufisadi wake;
1. Hebu tuachane na matendo yake pale AICC
2. Alianza na pesa ya mafuriko ya Tanga.
3. Baadaye akauza viwanja vya mnazi mmoja.
4. Baadaye anasifika kwa Richmond na dowans.
5. Wizara ya maji pia hakupita hivi hivi maana nasikia kila mwezi akaunti yake ilinona kwa kipato toka kwa kila injinia wa maji wa mkoa.
6. Hapo Arusha vipi vioski vya stationery vinavyolazimisha kila mkutano ununue kwake?
7. Hapo Dar kwa wenye mahoteli vipi vurugu za kulazimishwa kupeleka mashuka kwenye laundry zake? Nasikia musipofanya hivyo TRA wanawazonga.

Lazima kama hizo kwa sasa, je, vipi akipewa U-rais itakuwaje? Mbona tutalawitiwa kwa nguvu!


Hitimisho dogo kwangu kwamba anaweza kuwa tishio kwa CCM lakini siyo kwa wa-Tz wote na hasa walio timamu. Tatizo ni mpangilio wa CCM na kamati zake. Hebu angalia viwango vya ufahamu vya wajumbe wa kamati kuu ya CCM. Ni ndogo kiasi kwamba bado mtu kama Kingunge ndo thinkers wao. Enzi hizi za dot com. Engine ya chama huanzia kwa katibu wake, vipi huyo katibu wa CCM? Vijana wanasema kama ni moto, kuni mbichi. Hauwaki hata siku moja.

Sasa waangalie vijana wa CCM. Nani wa kutumainiwa kwa ufahamu wa mambo ya nchi na Dunia? Hao ni vijana wa wakati ambao nchi ina vijana zaidi ya laki moja ktk vyuo vya elimu ya juu. Enzi za mkongo wa mawasiliano ili kila mtu aione dunia nyumbani kwake. Kwa nini hakuna kijana mwelevu huko UVCCM?

Ukisha iona structure kama hiyo huyu mtu hawezi kutoa bilioni mbili wakagoma kutoa support.

Ni Tishio lao huko huko CCM.
 
Mimi nauliza Lowasa tishio kwa nani?? Watanzania awamtaki kabisa kama atajaribu mwaka 2015 basi ajipendi kwa sababu atamalizika na kama atapita kama anavyo jimarisha basi nchi hii ya TANZANIA itauzwa na WaTanzania ndani ya nchi yao. Kweli kama anataka uraisi mwaka 2015 then arudishe mali zote alipata kwa ufisadi na wizi kwa WaTanzania bila kusita. Alafu akiri kwa dhati kua yeye ni fisadi na kuunda hiyo kampuni ya RICHMOND na wote wanaosika.

Kwanza huyo mIran Rostam dawa yake iko jikoni. Anatujafua nchi yetu nakujidai yeye ni Mafia sisi ni zaidi. AJARIBU ataiona. Pesa za WaTanzania ameiba inamtia kiwewe kwa na dharao na kiburi asubiri tuu. Tunajua sana kwa ameweka wavijana wa CLOUDS FM kama kanyaboy tunasubiri. Heri yako Rostam umezoea ----
 
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa....ni njaa yakusumbua au hauna akili timamu.
huyu jamaa anaweza kuwa tishio kwako pekee
 
Nani anaitaka CCM, mafisadi? yes, vitoto vyao vilivyoko uvccm? yes, wapambe wanaokula makombo ya ufisadi kama Anold, Nanu, Salimia, Majimshindo, Nduka,Kaumza, Kashaga, itahwa et al? yeeeeeeeeeees!
Wananchi? HELL NNOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
CCM Mpitisheni Lowasa kugombea urais 2015, wananchi tupate nafasi ya kumhukumu, kumsulubu, kumrudi jambazi, fisadi, nyang'anyi, jangili lililomshinda JK na CCM yake.
Mkuu vipi tena mbona unaingia kimugongo mugongo huku ukitaja majina hovyo hovyo? Mbona unaleta maajabu ya sisimizi kumeza dafu?
Kuhusu Lowassa kwangu ni kama malaria..... haikubaliki
 
nawaonea huruma kambi ya rowasa sababu hata adui yenu hamumfahamu poleni sana! najua mnalipwa pesa nyingi ila mjue adui yenu mkubwa yumo ndani ya ccm VILAZA NINYI!

Very true! Lowassa na wenzie watamalizana na siasa za Ki-kaskazini na siasa za Pwani na sio upinzani.
 
Yaani lowasa akiwa rais wa tz, nadhani ategemee katiba ya sasa mchakachuo wanaotaka leta katiba mpya 2014, vinginevyo no
 
Duuu
Hii sokuijua kabisaaa

LOWASSA TISHIO?!
Tusiandike kwa mate wakati wino upo:

1972 - 1973 Milambo High School (combi: Swahili, History na English - SHE) Division III

1975 - 1970 University of Dar es Salaam (B.A. Theatre Arts "Sanaa ya maigizo") Pass

AMA KWELI TISHIO!

 
Hivi ni lini Watanzania tutakuwa serious..???hivi unaweza kusimama mbela ya jukwaa na kumtetea Lowasa?????????

Hebu tuwekee jamvini ubaya wake ukilinganisha na wana ccm wengine. Maana kabla ya Mambo ya Dowans kila mtu alikuwa anamsifia sasa kwakuwa nimi ni adui mkubwa wa watu wanafiki hebu tuambie ubaya wake ukiachiria mbali huu wa Dowans ambao serikali yote ilihusika.
 
Najiuliza kwa nini iwe hivyo kwa mtu ambaye amejiuzuru kwa fedheha kiasi hicho! mtu ambaye amekuwa madarakani siku nyingi bila mafanikio kwa nchi tunayoweza kuyakumbuka.

Wale muliouliza ufisadi wake;
1. Hebu tuachane na matendo yake pale AICC
2. Alianza na pesa ya mafuriko ya Tanga.
3. Baadaye akauza viwanja vya mnazi mmoja.
4. Baadaye anasifika kwa Richmond na dowans.
5. Wizara ya maji pia hakupita hivi hivi maana nasikia kila mwezi akaunti yake ilinona kwa kipato toka kwa kila injinia wa maji wa mkoa.
6. Hapo Arusha vipi vioski vya stationery vinavyolazimisha kila mkutano ununue kwake?
7. Hapo Dar kwa wenye mahoteli vipi vurugu za kulazimishwa kupeleka mashuka kwenye laundry zake? Nasikia musipofanya hivyo TRA wanawazonga.

Lazima kama hizo kwa sasa, je, vipi akipewa U-rais itakuwaje? Mbona tutalawitiwa kwa nguvu!


Hitimisho dogo kwangu kwamba anaweza kuwa tishio kwa CCM lakini siyo kwa wa-Tz wote na hasa walio timamu. Tatizo ni mpangilio wa CCM na kamati zake. Hebu angalia viwango vya ufahamu vya wajumbe wa kamati kuu ya CCM. Ni ndogo kiasi kwamba bado mtu kama Kingunge ndo thinkers wao. Enzi hizi za dot com. Engine ya chama huanzia kwa katibu wake, vipi huyo katibu wa CCM? Vijana wanasema kama ni moto, kuni mbichi. Hauwaki hata siku moja.

Sasa waangalie vijana wa CCM. Nani wa kutumainiwa kwa ufahamu wa mambo ya nchi na Dunia? Hao ni vijana wa wakati ambao nchi ina vijana zaidi ya laki moja ktk vyuo vya elimu ya juu. Enzi za mkongo wa mawasiliano ili kila mtu aione dunia nyumbani kwake. Kwa nini hakuna kijana mwelevu huko UVCCM?

Ukisha iona structure kama hiyo huyu mtu hawezi kutoa bilioni mbili wakagoma kutoa support.

Ni Tishio lao huko huko CCM.

Ndiyo maana nikasema hakuna mwenye hoja ya maana ya kumshitaki Lowasa!! Huu ulioandika hapa ni UZUSHI MKUBWA. kwa mfano hakuna asiyejua kuwa aliyeuza viwanja vya Mnazi mmoja miaka ya 1993 ni Rais Mwinyi hii hata taahira anajua, Lowasa kipindi hicho aliingia kwenye mgogoro mkubwa na mzee mwinyi kupinga uuzaji wa viwanja hivyo ambapo alitoa masaa kadhaa kwa manispaa ya ilala iwe imeondoa uzio wa mabati uliokuwa umewekwa hapo. baada ya muda kupita bila manispaa kuondoa wananchi walienda wenyewe kuyaondoa kitu kilichompa heshima kubwa Lowasa leo hii unatuambia Lowasa ndiye aliyeuza viwanja? HUU NI UONGO.
 
Back
Top Bottom