LOWASSA ni tishio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LOWASSA ni tishio

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Mar 30, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa nikifuatilia sana vyombo vya habari vinavyopinga Lowassa(Mwanahalisi na Raiamwema) na vinavyo msapoti(Rai na Mtanzania). Nimefuatilia sana wanasiasa wanaompinga na kumsapoti. Mwisho nimebaini kuwa Lowassa ni tishio kubwa kwa wanaoutaka urais wa muungano ndani ya chama chake na kwa upande wa upinzani. Ana nguvu kubwa sana serikalini na katika chama. Ni bingwa wa kuratibu mtandao kisomi. Ni mtendaji na haogopi. Na iwapo ataamua kugombea, hatakuwa na mpinzani mwenye nguvu ndani ya chama chake na hata ktk uchaguzi mkuu. Sote tumeshuhudia jinsi alivyoweza kuukwaa uenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama bila mtu yeyote kutia mguu kumpinga. Na sasa tumeshuhudia jinsi anavyopata sapoti kutoka kwa Mhe Beatrice Shelukindo na mumewe William Shelukindo. LOWASSA NI TISHIO
   
 2. G

  Gurti JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Una bahati nimeisoma hii thread. wengine wamekupuuza
   
 3. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  UMEKATIWA NGAPI NA HUYU RA?


  [​IMG]
   
 4. F

  Fareed JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hakuna lolote hapa. Lazima wewe umelipwa pesa na Rostam Aziz au Lowassa mwenyewe. Lowassa ni kiongozi anayeleta aibu kwa Tanzania na kwa chama chake CCM. Ni mpenda mali, ana utajiri mkubwa usioweza kuelezeka (unexplained wealth). Kama wewe unamsifia Lowassa kwa utendaji kazi je Edward Moringe Sokoine ungesemaje? Waziri Mkuu mchapa kazi na mwenye msimamo ambayo Tanzania imewahi kumpata katika historia yake ni Edward Sokoine na Julius Nyerere aliyemtangulia.

  Mawaziri wakuu wote waliofuata, ikiwemo Lowassa, ni bomu tu. Kuhusu Lowassa kuwa tishio, labda kwa CCM kwani hicho ni chama kilichotekwa na mafisadi. "Tishio" la Lowassa unalosema wewe ni kutokana na kuwa na pesa nyingi za kifisadi kuweza kununua kura za wana CCM na si kutokana na ubora wa uongozi.

  CCM ina viongozi bora na "Tishio" zaidi kuliko fisadi Lowassa kwa utendaji kazi na uadilifu ambao wanafaa kuwa Rais. Nao ni Samuel Sitta, Harisson Mwakyembe, John Magufuli na Bernard Membe.

  Lowassa na genge lake la mafisadi wakiwemo Rostam Aziz, Andrew Chenge, Nazir Karamagi, Yusuf Makamba, Peter Serukamba, Makongoro Mahanga, na wengine wanastahili kwenda jela si IKULU.
   
 5. i

  itahwa Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja,na ndio anayewatia homa CDM,na ndio maana cdm wakilala wakiamka ni lowasa,huyu jamaa akisimama chadema chali coz lowasa anajua siasa za kisasa,ni msomi na ni msikivu na si mropokaji kama padri slaa! sasa wanachofanya cdm ni kumchafua kwa kashfa ambazo hawawezi kuthibitisha,wanabase kwenye rumours only! cdm need to be realistic with people na waambie sera zao na mipango yao,politics of critizing others imeshapitwa na wakati!
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  to his wife, maybe.
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mbona hata Nyerere alishasema tangu miaka ile ya Tisini kuwa Lowasa ni Tishio na hafai kushika uongozi wa Nchi hii.
   
 8. Panga La Shaba

  Panga La Shaba JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 209
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi ni lini Watanzania tutakuwa serious..???hivi unaweza kusimama mbela ya jukwaa na kumtetea Lowasa?????????
   
 9. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Wanaganga njaa hao ndugu yangu, usishangae sana. Kwa bahati mbaya sana kwao wanadhani Watanzania wa leo ndio wa miaka ileeee!
   
 10. Muro

  Muro Senior Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Viongozi wote wa CCM ni mafisadi papa,hata huyo Sokoine, alikuwa fisadi bahati mbaya mauti yalimkuta pasipokujipanga sawasawa,mali zake nyingi aliwekeza kwa watu hasa wahindi Arusha na wote waliiliza familia yake,hivyo sishangai kwa Lowasa, amejitayarisha kwa ajili ya kugombea Urais 2015,waswahili wanasema samaki mkaange na mafuta yake mwenyewe,fedha zetu wenyewe zinatukaanga,LAKINI NGUVU YA UMMA NDIYO ITAKAYOAMUA.TUNAMSUBIRI AJE,KAMA ATAWEZA KUHONGA UMMA WOTE WA TANZANIA.
   
 11. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Duh! Ama kweli njaa mbaya.
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  nawaonea huruma kambi ya rowasa sababu hata adui yenu hamumfahamu poleni sana! najua mnalipwa pesa nyingi ila mjue adui yenu mkubwa yumo ndani ya ccm VILAZA NINYI!
   
 13. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Doh! hadi mtoto wa shule ya msingi anajua jamaa MWIZI anajisafishaje?
   
 14. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  LOWASSA kweli ni tishio; na kwa maana hiyo hafai kuongoza nchi yetu. CHADEMA inamwaogopa LOWASSA kwa wizi wake na si kwa uimara katika medani ya siasa. Waziri Mkuu wa kwanza kujiuzulu kwa kashfa.
   
 15. BongoLogik

  BongoLogik JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha kuleta utumbo wa kizushi wewe! una evidence yoyote kuhusu ufisadi wa Sokoine au unaropoka tu kuongeza idadi ya posts?
   
 16. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sishangai kuwa hatuko sayari moja, unatoka sayari ya mafisadi, we have nothing, nothing at all in common.
  Kwenye Bluu; Za kukkwapua mabillioni ya hela za waTZ, kujilimbikizia, hadi kuvimbiwa na kuzitumia kuingia madarakani, if yes then Lowasa anajua siasa za kisasa.
  Kwenye nyekundu: anasikiliza nani? Au unamaanisha alivowasikiliza wachawi wa Thailand na kuwaleta TZ kunya Mvua?
  Anawasikiliza mafisadi wenzake wanapopanga uharamia kwa TZ. Au ulikuwa unamaanisha kuwa Lowasa anasikilizia wananchi wanavolalama na hali ngumu ilhali ana limbikizi la milenium?
  Kwenye Purple: Lowasa anachafuliwa? Hivi utasema jalala/dampo linachafuliwa?
  Anyways, Kamati ya Mwakyembe iliyomwondoa EL uPM ilikuwa na wajumbe wangapi wa CDM? Hii kashfa Richmond ilichunguzwa na nani?
  Kwenye Black; kwa nini haendi court kwa kuchafuliwa jina?

  Kama uko kwenye sayari hii tunayoiishi, basi ni mgonjwa wa akili, Kuna kitengo kiko Muhimbili utapata msaada.
   
 17. M

  MkuuMtarajiwa Member

  #17
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna ukweli fulani katika jambo hili, hivi unajua viongozi wote waliokwenda Loliondo kwa Babu walikwenda baada ya kusikia Lowasa amekunywa kikombe cha Babu!! ...na kadri siku zinavyozidi utasikia wengi zaidi wakimiminika Loliondo!
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,497
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Inaelekea Mafisadi walikuchagua bila kupitia CV yako.

  Hebu tuletee ushahidi ni lini CDM wamemzungumzia Lowasa. Waliomzungumzia Lowasa hivi karibuni ni UVCCM na Sumaye. Actually, CDM watasherehekea siku Lowasa atakapopitishwa kuwa mgombea.
   
 19. L

  LAT JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  lowasa hata ukimmilikisha keep left ya samora avenue au ile ya pale new Arusha hoteli atajenga gorofa ... tamaa ipo mbele
   
 20. l

  lemberwa Member

  #20
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lowassa hafai kuiga wala kuwa ndugu
  Sisi tuliopo huku kanda ya kaskazini tunaomba achaguliwe na ssim hata monduli hawamtaki
   
Loading...