LOWASSA ni tishio

Pamoja na ukweli kuwa mimi si mwanachama wa ccm lakini kwa sasa huyu ndiyo tishio kwa wale wote watakao taka kugombea nafasi ya urais 2011 kwa ccm. .
Nani anaitaka CCM, mafisadi? yes, vitoto vyao vilivyoko uvccm? yes, wapambe wanaokula makombo ya ufisadi kama Anold, Nanu, Salimia, Majimshindo, Nduka,Kaumza, Kashaga, itahwa et al? yeeeeeeeeeees!
Wananchi? HELL NNOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
CCM Mpitisheni Lowasa kugombea urais 2015, wananchi tupate nafasi ya kumhukumu, kumsulubu, kumrudi jambazi, fisadi, nyang'anyi, jangili lililomshinda JK na CCM yake.
 
nawaonea huruma kambi ya rowasa sababu hata adui yenu hamumfahamu poleni sana! najua mnalipwa pesa nyingi ila mjue adui yenu mkubwa yumo ndani ya ccm VILAZA NINYI!

Wa kwanza Rstam, pili Kikwete na familia yake
 
Lowasa ningemuunga mkono sana kama angemtoa kafara Rostam, Watz tungeweza kujaribu kufanya jambo lakini kwa hali ya Rostam hawezi kuwa safi, ningemshauri aachane na mtandao wa akina Chenge atafute uhusiano mzuri na akina Mwakyembe atatoboa.

mamaaaaaaaaaaaaaa!!
Yani fisi aache urafiki na kina mbweha na chatu atafute uhusiano mzuri na kondoo! Are you serious? Hebu angalia Avatar hii!
avatar38134_3.gif
Halafu jaribu ku-imagine fisi anasogea karibu nae!! What'll happen next JF?
 
mamaaaaaaaaaaaaaa!!
Yani fisi aache urafiki na kina mbweha na chatu atafute uhusiano mzuri na kondoo! Are you serious? Hebu angalia Avatar hii!
avatar38134_3.gif
Halafu jaribu ku-imagine fisi anasogea karibu nae!! What'll happen next JF?

Umeniuaaaaaaa! Kumbe nimepoteza muda kumshauri shetani akamwombe Mungu msamaha!
 
Kama sisi ni wazalendo wa nchi hii Tusimwangalie lowassa. Tukiweka macho yetu kwa lowassa ina maana ccm hata wakituwekea bogus yeyote yule isipokuwa lowassa basi tunaridhika.
Hapa jf nilidhani tulikuwa intellectuals lakini kwa sasa hata watoto wa shule ya msingi hawachangii mada kwa namna hii (naomba samahani kwa kusema haya).

Unajiita mzalendo, halaf intellectual. Na humwangalii na unahamasisha watu wasahau ya Lowasa.
Mzalendo na intellectual ambaye unamuona Lowasa aliye mweupe kama nywele zake kichwani, bila mawaa yoyote, mkarimu, mpenda watu, kwa ajili ya watu, anayeweka maslahi ya umma mbele, anayechukia mtu yeyote anayepora haki ya wanyonge, role model, kiongozi wa kuigwa. mwenye ma-vision ya kitaifa.
WanaJF nadhani nikishaandika hivi jamvini nina haki ya kumtafuta Lowasa nimuonyeshe nilivyomsafisha na kukubalika JF, na bila shaka nitapewa changu, jioni viti virefu siulizi bia sh ngapi.
Nanu Naomba kontakt za lowasa na mimi nikachukue mgawo kwa maana najua ni sehemu ya kodi yangu.
 
Watanzania wanzangu mbona ni mapema mno kuanza kampeni za uchaguzi wa 2015. Ni vema tukafikiria masuala mengine ya kimaendeleo kama vile kuboresha shule zetu hususani za kata, namna ya kupata umeme wa uhakika kufufua viwanda vyetu vilivyokufa baada ya ubinafsishaji, nk
 
Ndugu,
Nimefuatilia kwa mamini majibu ya wengi humu. Inaonyesha dhahiri kwamba bila kujali itikadi za kichama, wengi hawamkubali LOWASSA. Na mimi mmojawapo. Si kwa ushabiki wa kichama wala nini, ni kwa masilahi ya Taifa tu.
Ila sasa, lisemwalo lipo, kama tumeshajua hivi na nia ya mtu huyu iliyojaa tamaa, nawaomba tusimame kidete kwa pamoja na kuondoa tofauti za kichama ili kumpinga huyu mtu. Ni TISHIO kwa nchi hii.
Tumpinge kwa nguvu zote kwa sababu itatugharimu. Nina maana kusema kwamba maoni haya mnayotoa yasiishie humu tu kwa kumjibu huyu kibaraka KAUMZA sijui KAUZU, ambaye sina hakika amelipwa kiasi gani kuandika utumbo kama huu.
Kama ni Rais niko tayari kumuunga mkono mwingine yeyote awe Slaa, Sitta, Membe au Magufuli lakini si Lowassa.

Join the club salimia.
 
Watanzania wanzangu mbona ni mapema mno kuanza kampeni za uchaguzi wa 2015. Ni vema tukafikiria masuala mengine ya kimaendeleo kama vile kuboresha shule zetu hususani za kata, namna ya kupata umeme wa uhakika kufufua viwanda vyetu vilivyokufa baada ya ubinafsishaji, nk

Tulianza kuboresha shule tangu 2006 rejea MMES, umeme tumeanza kuongeza jitihada za kufua tangu 2006 chini ya Richmond na dowans etc na bado tunaendelea. Hebu tuambie japo a single achievement utakayotembea nayo kifua mbele ukijisifu?
Si bora tuangalie tu jinsi ya ku-topple failed regime?
 
Nashangaa bado waTz wanaomuota Raisi Lowassa. Jamaa huyu hana mtaji wowote wa kisiasa anaoweza kujivunia mbele ya wanasiasa. Lets talk clean politics. Aaaghhh!
 
naunga mkono hoja,na ndio anayewatia homa CDM,na ndio maana cdm wakilala wakiamka ni lowasa,huyu jamaa akisimama chadema chali coz lowasa anajua siasa za kisasa,ni msomi na ni msikivu na si mropokaji kama padri slaa! sasa wanachofanya cdm ni kumchafua kwa kashfa ambazo hawawezi kuthibitisha,wanabase kwenye rumours only! cdm need to be realistic with people na waambie sera zao na mipango yao,politics of critizing others imeshapitwa na wakati!

Hivi unaposema msomi katika zama hizi unamaanisha nini na unalinganisha na nani, Makamba? Maana kama unazungumzia wasomi hamfikii Mwakyembe, Magufuli na Mwandosya ambao wana shahada za uzamivu na watafiti wa kweli. Huyo Lowassa amesoma nini? Au unazungumzia ile shahada yake ya sanaa za maigizo na kucheza ngoma ambayo inampa sifa za kuwa mwalimu wa chuo cha sanaa bagamoyo kuliko kuwa hata mshauri wa rais pale ikulu. Ni vizuri ukawa mwangalifu unapozungumzia usomi maana katika zama hizi na hata katika baraza la mawaziri kila mtu msomi labda akina Lukuvi lakini hata kijana wake Nchimbi anamzidi sasa anataka kumringishia nani na hiyo sanaa ambayo hata Mgunga mwa Mnyenyelwa ameisomea vizuri kuliko huyo "Mungu wenu" Lowassa mnayemsujudia? Kama hujasoma ni wewe tu lakini sisi wengine wazazi wetu waliwekeza kwenye elimu zetu na tuko huru na tumesomea vitu vya maana siyo mirindimo kama yeye. Kama wazazi wako walikunywa bia tu na wewe hukwenda shule basi matamko yako ya kitumwa yaishie huko huko!
 
Sishangai kuwa hatuko sayari moja, unatoka sayari ya mafisadi, we have nothing, nothing at all in common.
Kwenye Bluu; Za kukkwapua mabillioni ya hela za waTZ, kujilimbikizia, hadi kuvimbiwa na kuzitumia kuingia madarakani, if yes then Lowasa anajua siasa za kisasa.
Kwenye nyekundu: anasikiliza nani? Au unamaanisha alivowasikiliza wachawi wa Thailand na kuwaleta TZ kunya Mvua?
Anawasikiliza mafisadi wenzake wanapopanga uharamia kwa TZ. Au ulikuwa unamaanisha kuwa Lowasa anasikilizia wananchi wanavolalama na hali ngumu ilhali ana limbikizi la milenium?
Kwenye Purple: Lowasa anachafuliwa? Hivi utasema jalala/dampo linachafuliwa?
Anyways, Kamati ya Mwakyembe iliyomwondoa EL uPM ilikuwa na wajumbe wangapi wa CDM? Hii kashfa Richmond ilichunguzwa na nani?
Kwenye Black; kwa nini haendi court kwa kuchafuliwa jina?

Kama uko kwenye sayari hii tunayoiishi, basi ni mgonjwa wa akili, Kuna kitengo kiko Muhimbili utapata msaada.

Kweli wewe ni mchambuzi mahiri. Jamaa aliko anjiona kinyesi kabisa! Kwani ukila hela ni lazima uje hapa JF kuitumikia? Si ulipe kwa njia nyingine hata ya kumtungia wimbo wa kumsifu? Ona sasa unavyogeuka toilet
 
LOWASSA TISHIO?!
Tusiandike kwa mate wakati wino upo:

1972 - 1973 Milambo High School (combi: Swahili, History na English - SHE) Division III

1975 - 1970 University of Dar es Salaam (B.A. Theatre Arts "Sanaa ya maigizo") Pass

AMA KWELI TISHIO!


Sasa hapo si ni bora tumchukue profesa Amandina Lihamba ambaye uwezo wake wa kucheza ngoma unafahamika kuliko huyu mtu ambaye ana-masquarade hata kabila kwa kujiita mmasai wakati yeye ni mmeru. Ni mdanganyifu katika kila kitu hata mambo madogo kama kabila lake!
 
itahwa, najaribu kukupata asili yako napata wasiwasi kidogo. Watanzania wote sasa hv wanalia na madeni makubwa ya nishati kwa sababu ya huyu unayesema ni msomi, siasa za kisasa zikoje unazozizungumzia?Hz za kulazimisha tenda? Hz za kulazimisha wananchi kujenga miundombinu ya kijamii ilhali pesa za serikali ambazo zingefanya kazi hizo zikitiwa ktk mifuko yao binafsi? Msipeleke siasa za ushabiki hata mahali palipo wazi makosa kutendeka. Kwani alipotakiwa kujiuzulu haikuthibitishwa kwamba alihusika moja kwa moja na kashfa ya Richmond? Richmond mpaka leo tunapozungumza si kashfa kwa serikali? Na mtendaji unapojihusisha na chombo chenye kashfa unakwepaje kuwa mwenye kashfa? Hakupewa nafasi huyu kujisafisha na kashfa hiyo? Je, alifanikiwa kujisafisha?
Mimi sitaki kusema na wewe umelipwa pia lkn hebu jitolee doa hilo mwenyewe!

Ndugu yangu unapoteza muda kupiga muziki laini kwa mbuzi. Huyu jamaa na wenzake wengi ni vifaa vya kazi ambavyo vinatumika kudaka punje za mkate wa bwana mkubwa hata kama kwa kufanya hivyo wanavua nguo hadharani. Lugha hiyo ya uchapa kazi, kutoa maamuzi na ujinga mwingine wa aina hiyo umekuwa ndiyo silaha yao ambayo kwa bahati mbaya haijawahi kuwapa mafanikio. Nchi hii ina wachapakazi waadilifu wengi na hawahitaji mtu anayetoboa mtumbwi katikati ya bahari. Kwa ufupi ni kwamba LOWASSA HAFAI NA HANA SIFA ZA KUWA RAISI\ WA NCHI HII. HATUMTAKI NA UCHAPAKAZI WAKE AKAWASAIDIE KULE MONDULI AMBAKO KUNA SHIDA LUKUKI LAKINI YEYE ANAWAPELEKEA FULANA NA KUZINDUA NYIMBO ZA INJILI, KANA KWAMBA INJILI HIYO INAMUINGIA!
 
Huo ndiyo ukweli ambao wengi hawataki kuusikia. Nakuhakikishia kuwa Lowasa kama atapata nafasi ya kugombea kituchochote katika nchi hii, kwa mtandao alio nao na kwa idadi ya watu wanaomuunga mkono nakuhakikishia kuwa kura atakazopata zitakuwa za ajabu. Pamoja na ukweli kuwa mimi si mwanachama wa ccm lakini kwa sasa huyu ndiyo tishio kwa wale wote watakao taka kugombea nafasi ya urais 2011 kwa ccm. Nyota ya Lowasa inawaka kwa kiasi kikubwa ndiyo maana waandishi wa habari kama Saed Kubenea wanafanya kila linalowezekana kujaribu kukumbusha watanzania maisha ya Lowasa ili wasije wakamkubali. Ni bahati mbaya sana kuwa inavyoonyesha wengi wanamuunga mkono kisirisiri moyoni ila mbele za umma wanajifanya kumpinga. Na hii ndiyo kusema kuwa wengi hawataki kujionyesha misimamo yao kwani endapo atafanikiwa kupenya 2011 basi siasa za visasi zinaweza kuwazoa wale wote wanaompinga hadharani, ndiyo maana hata viongozi waandamizi wa ccm pamoja na vyama vingine huwezi kukuta wanamsema Lowasa vibaya. Hao wenye ujasiri wa kumkosoa ni wale wasiojua hatari inyoweza kuwa mbele ya safari kama bahati itamrudia na hawa ni watu wa kawaida ambao hawana sauti za kutosha kuwaeleza wananchi.

Kukubalika ni kutisha watu na kuwafukuzisha kazi wale wanaompinga? Gambo kamfanya nini? Mungu atamuadhibu kwa jinsi anavyogharimu maisha ya vijana wadogo ambao anawaadhibu kwa sababu tu hawamkubali shetani na dikteta huyu mnayemlamba makwapa!
 
Again another mental disorder of some jf members

mtoa maada kaeleza vizuri kwa nini ni tishio...nilidhani mngekuja na hoja ya kusema ni jinsi gani ya kumzuia

wengi mmechukulia kuwa mtoa maada anamsafisha lowassa!!!! What a shame?? Shame!!! Shame!!!! Shame!!!!

You think people here have low level of comprehension? People are able to anticipate where you were going and rightly so, they have realised that this yet another laundry mission that has terribly misfired. We have all along known that Lowassa will try to resurrect in many ways, confusing even right thinking members of JF. Thank God, people are clever enough to separate kernel from the chaff and, sadly you happen to fall on an unenviable side of the chaff, along with your fellow mercenaries. We need not read too much into your rubbish. You are just another gun for hire and your mission is very clear, to serve as a detergent all out to clean what is uncleanable!
 
nimekuwa nkifuatilia kwa makini hoja za wanasiasa wa nchi hii kuanzia chama tawala mpaka vya upinzani nkagundua kuwa wote wanamuogopa lowassa.si mbowe,padri dk slaa ,prof lipumba ,mbatia.hata mwakyembe na sitta.huwa wanazungumzia ufisadi na kuponda watu wengine lakini sijawai sikia wakimsema jamaa hadharani kwanin?
 
Mbona hata Nyerere alishasema tangu miaka ile ya Tisini kuwa Lowasa ni Tishio na hafai kushika uongozi wa Nchi hii.

Asante Ndibalema kidole changu kilikuwa juu kuomba kutoa hoja lakini nilivyosoma comment yako nimeshusha mkono
 
Kaumza, tangu lowassa akupe usafiri wa kwenda kwa babu kupata kikombe basi imekuwa nongwa unaropokaropoka tu kama unataka kukata roho au ndiyo furaha ya kupata hicho kikombe!!! Umepona lakin????

Watu wenye akili zetu tunamjua lowassa ni mtu wa aina gani wala hatuhitaji huo upuuzi wako wa kusifia mtu kama lowassa, kama huna cha kuandika soma walichoandika wengine na toa mchango wako kama unapenda kufanya hivyo.

Acha kuendekeza njaa itakufikisha pabaya........
 
Back
Top Bottom