LOWASSA ni tishio

Hakuna mti mwenye akili timamu anaweza amka na kuanza kumsifia mwizi kama lowasa, shida ya mgao wa umeme leo tatizo ni lowasa
na kampuni yao wezi wakubwa, mungu atalidhiirisha ili soku moja . mi binafsi siku lowasa akichaguliwa rais nitakunwa sumu. naomba
nikumbushwe akishakuwa rais
 
Hafai mwivi mkubwa anataka kila kitu hii nchi sio yao akatafute urais kuzimu
ndo kuna watu wa sampuli yake na swiba wake R,a; sisi sio wa mwaka 47.
tutamwonyesha nguvu ya umma'
 
Njaa bwana!!? Mnamtetea mpaka lowasa?? Mkitaka kuwajua watanzania wa ukweli, mpitisheni lowasa kugombea urais kwa ccm 2015.
 
poor orphan.JPG poor orphan.JPG
ccm oyeeeeeeeeeee el na ra oyeeeeeeeeeeeeeeeee jk makamba oyeeeeeeeeee haya ndo maisha bora
 
Na kwa hii hapa chini kweli huyu mtu tishio. Nimeamini sasa.
LOWASA KATIKA HARAKA ZA KUNUNUA URAIS 2015 ameanza na Sh billioni 8
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya mkataba tata wa Richmond, Edward Lowassa ameelezwa kuwa na mradi wa karibu Sh. 8 bilioni wa “kujisafisha” na kumwingiza ikulu.
Lowassa alipoulizwa na gazeti hili kuhusu mradi huo, alijibu kwa mkato, “Mimi sijui.”
MwanaHALISI limeelezwa kwamba fedha za “kumsafisha” Lowassa zimeahidiwa na swahiba wake, Rostam Aziz ambaye wamesimama pamoja muda wote wa sakata la kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond iliyothibitika kuwa feki.
Richmond ilipewa mkataba wa kufua umeme ikiwa haina fedha, wataalam wala uzoefu katika eneo hilo; huku nyaraka zilizopo juu ya kashfa hiyo zikionyesha kuwa mkataba ulipatikana kwa njia ya upendeleo – tuhuma ambazo zinamwangukia Lowassa.
Taarifa zinasema mabilioni hayo ya shilingi yamelenga kutumika kulegeza wajumbe wa vikao vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa kuelekea, na wakati wa mkutano mkuu ndani ya chama hicho ambao utafanyika mwaka kesho.
Fedha hizo pia zinadaiwa kulenga kuyumbisha jumuiya za CCM – Umoja wa Wanawake (UWT), Jumuiya ya wazazi na Umoja wa Vijana (UV-CCM).
Wengine ambao wanadaiwa kulengwa katika hatua ya kushawishi, kulegeza na kushirikisha katika mradi wa kusafisha Lowassa ni wabunge, vyombo vya habari na waandishi wa habari mmojammoja.
“Mradi wa kumsafisha Lowassa” umeelezwa kuwa chini ya kundi la watu watano. Mbali na Lowassa mwenyewe na Rostam, wengine waliotajwa ni Andrew Chenge, Makongoro Mahanga na Peter Serukamba.
Chenge ni mbunge wa Bariadi Magharibi; Mahanga ni mbunge wa Segerea na Serukamba ni wa Kigoma Mjini. Taarifa zinasema tayari baadhi ya wajumbe wa kundi hilo wamefanikiwa kushika nafasi za juu za Kamati za Kudumu za Bunge.
Walioshika nafasi hizo ni Lowassa (Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama) na Serukamba (Miundombinu).
Gazeti hili limeelezwa kuwa mgogoro unaoendelea ndani ya UV-CCM, unatokana na “kasi ya mbio za Lowassa kugombea nafasi muhimu” ndani ya chama chake na baadaye urais.
Kwa wiki mbili sasa, viongozi wa vijana wamekuwa wakisutana, kulaumiana na kutuhumiana kujenga makambi ndani ya umoja huo. Wiki iliyopita walimrukia waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye wakimtuhumu kuhujumu chama “kwa kuzungumza nje ya vikao.”
“Sikiliza bwana ee, vurumai hii ya vijana ni ya kutafuta kujenga kundi la kumsafisha Lowassa. Wapo wanaofanya kazi hiyo kwa kujua na wapo wanaofanya hivyo bila kujua,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM.
Hatua ya baadhi ya viongozi wa vijana, kurukia kila wanayeona ana uwezekano wa kupinga Lowassa na kundi lake, inaelezwa kutokana na waliokuwa wapinzani wao wakuu kubaki serikalini na wao (akina Lowassa) kuwa nje ya utawala.
Wanaotajwa kuwa serikalini, lakini wanadaiwa kuwa wapinzani wa Lowassa katika mgawanyiko wa wanaopinga ufisadi na wanaoutetea, ni pamoja na Samwel Sitta, ambaye hivi sasa ni waziri wa Afrika Mashariki.
Wengine ambao akina Lowassa hawakutegemea kuwemo serikalini, ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Benard Membe; naibu waziri wa ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe na mkuu wa wilaya ya Masasi, Nape Nnauye.
Lowassa hakuwa na simile pale alipohojiwa kwa njia ya simu kuhusu “mradi wa kujisafisha.”
Swali: Mheshimiwa, tumepata taarifa kuwa una mradi wa Sh. 8 bilioni kwa ajili ya “kujisafisha kisiasa.” Je, hii ni kweli?
Lowassa: Muulizeni huyo mpuuzi aliyewaambieni.
Swali: Gazeti linakuliza wewe kwa kuwa ndiyo mwenye mradi.
Lowassa: Mimi sijui. Sitaki kusikia mambo ya kijinga…”
MwanaHALISI liliripoti katika toleo lake la Machi 9 – 15 mwaka huu, chini ya kichwa cha habari kisemacho, “ Siri ya Edward Lowassa nje,” juhudi za mbunge Beatrice Shelukindo “kumsafisha” Lowassa.
Katika ujumbe wake wa maandishi kwa mbunge mwenzake, Pindi Chana, Shelukindo alisema ameambiwa na Nabii Joshua wa Nigeria kuwa “rais ajaye ni Edward Lowassa” na kwamba maisha yake ya nyuma yanayomhusisha na kashfa ya ufisadi, “si kitu.”
Joto la Shelukindo katika mawasiliano haya lilitokana na kile alichoeleza kuwa, “Mungu ni wa ajabu. Lowassa ameniombea kura pasipo maelezo. Ameandaa lunch na dinner (vyakula vya mchana na usiku) ambako amekuwa akiniombea kura. Mungu ana njia za ajabu za kufanya mambo.”
Shelukindo alikuwa akirejea fadhila za Lowassa kumwombea kura wakati wa kugombea nafasi ya kamishena wa bunge. Alishinda.
Naye Rostam alitafutwa kwa simu bila kupatikana. Hatimaye alipelekewa swali kwa njia ya sms.
Swali: Kuna taarifa kuwa umeahidi kumwezesha Mhe. Edward Lowassa kwa Sh. 8 bilioni katika kile kinachoitwa “mradi wake wa kujisafisha kisiasa.” Je, hii ni kweli? Simu yako haiitiki.
Tofauti na Lowassa aliyesema hataki kusikia “mambo ya kijinga,” Rostam alijibu kwa sms, “Sidhani Lowassa anahitaji mradi wa kumsafisha maana si mchafu,” kauli ambayo haikushangaza kwa kuwa ilitoka kwa swahiba mkuu wa wakati wa jua na mvua.
Rostam aliandika, “Isipokuwa nimetenga pesa kuwasaidia nyie MwanaHALISI mnunue mtambo wa kuchapisha gazeti bila bughdha!”
Hata hivyo, gazeti hili lina uhakika kuwa Rostam hana mtambo wa kuchapa magazeti yake ya Mtanzania, Rai, The African, Bingwa na Dimba. Anayachapia kampuni ya Mwananchi Communications Limited.
Majibu ya Rostam yameelezwa kuwa ya kumfariji swahiba wake kwa msingi mmoja tu; kwamba wameshiriki – kwa njia mbalimbali – katika kutafuta miradi ya kufua umeme, ambayo imeleta kashfa na kumfikisha Lowassa alipo sasa.
Mtoa taarifa amesema kundi la watu watano limekuwa likifanya vikao; lakini ni kikao cha Dar es Salaam cha mwishoni mwa mwaka jana, ambacho kiliweka mkakati wa Lowassa kujitokeza hadharani “kila inapobidi,” kushiriki mikutano na kutolea matamko hoja kadhaa zinazoibuka ili aonekane karibu na wananchi.
Maswali yaliyotumwa kwa wajumbe wengine wa kundi hili ambao simu zao ziliita bila kujibiwa au hazikupatikana, hayakujibiwa.
Wakati hayo yakifanyika, taarifa zinasema baadhi ya wajumbe wa NEC wamejipanga kupeleka hoja katika vikao vya juu kutaka watuhumiwa wote wa ufisadi waenguliwe kwenye nafasi zao za uongozi ndani ya chama.
“Tunakwenda kwenye NEC tukiwa na dhamira moja ya kumuondoa Rostam, Lowassa na Chenge katika vikao vya maamuzi vya chama chetu. Huo ndio mkakati wetu na lazima tuutekeleze ili kukinusuru chama,” ameeleza mmoja wa wajumbe wa NEC.
Katika minyukano hiyo, vijana ambao wasiokubali kuingia katika mradi wa kumsafisha Lowassa wameanza kusakamwa. Tayari mjumbe wa Baraza Kuu la uongozi la UV-CCM kupitia mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesimamishwa uongozi na baraza la vijana la mkoa huo.

Pamoja na kutuhumiwa kuhujumu kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini, Baltida Buriani, Gambo anatuhumiwa kumweleza mmoja wa watu walio karibu na Lowassa kuwa “hafai kabisa”, akitumia maneno ambayo, kwa kuzingatia maadili, gazeti hili haliwezi kuyachapisha.

Kauli ya Gambo ilipofikishwa kwa mtoto wa Lowassa, Frederick, mtoto huyo alimwandikia Gambo sms ifuatayo: “Gambo unayo haki ya kumchagu mtu yeyote unayemtaka na siyo kumutukana mzee wangu. Hiyo siyo siasa, lakini endelea.” Ilikuwa 4 Machi 2011, saa 2:14:39 usiku. Gazeti hili limeona mawasiliano hayo.
Uhusiano wa Gambo na wafuasi wa Lowassa ulizidi kuwa mbaya kutokana na kunukuliwa akielezea wajumbe wa baraza la vijana la taifa mjini Dodoma wiki mbili zilizopita kuwa, sababu kubwa iliyofanya CCM kufanya vibaya katika uchaguzi uliopita, “ni chama kukumbatia watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini.”
“Lowassa na Rostam ndio wanakipotezea mvuto CCM. Tusitafute mchawi. Watanzania wanakerwa sana na Richmond na Dowans na lazima CCM iwashughulikie wahusika wote ili kujenga taswira mpya kwa chama chetu,” alieleza.

msource wanahalisi​
 
Lowasa hawezi kuwa Rais wa nchi hii kwasababu hana uwezo wa kuongoza, ni mbinafsi, ni mkabila, ni mbaguzi, ukiongezea ile sifa mbaya zaidi aliyonayo tangu enzi za shuleni,"WIZI".Na hataacha kuiba hadi siku ya mwisho hapa duniani. Sasa imeongezeka sifa jeuri zaidi ya Ufisadi. Lowasa ni Muongo wa kutupwa. Amekuwa akiwaambia watu kwamba yeye ni Mmasai, siyo kweli. Baba yake ni Mchagga, kwahiyo Lowasa ni Mchagga, hataki ajulikane hivyo. Sifa mbaya zote hizo alizo nazo Lowasa, zinamfanya asiweze kuongoza hata kikundi cha watu wawili, mmoja-wapo akiwa yeye.
 
Hakuna lolote hapa. Lazima wewe umelipwa pesa na Rostam Aziz au Lowassa mwenyewe. Lowassa ni kiongozi anayeleta aibu kwa Tanzania na kwa chama chake CCM. Ni mpenda mali, ana utajiri mkubwa usioweza kuelezeka (unexplained wealth). Kama wewe unamsifia Lowassa kwa utendaji kazi je Edward Moringe Sokoine ungesemaje? Waziri Mkuu mchapa kazi na mwenye msimamo ambayo Tanzania imewahi kumpata katika historia yake ni Edward Sokoine na Julius Nyerere aliyemtangulia.

Mawaziri wakuu wote waliofuata, ikiwemo Lowassa, ni bomu tu. Kuhusu Lowassa kuwa tishio, labda kwa CCM kwani hicho ni chama kilichotekwa na mafisadi. "Tishio" la Lowassa unalosema wewe ni kutokana na kuwa na pesa nyingi za kifisadi kuweza kununua kura za wana CCM na si kutokana na ubora wa uongozi.

CCM ina viongozi bora na "Tishio" zaidi kuliko fisadi Lowassa kwa utendaji kazi na uadilifu ambao wanafaa kuwa Rais. Nao ni Samuel Sitta, Harisson Mwakyembe, John Magufuli na Bernard Membe.

Lowassa na genge lake la mafisadi wakiwemo Rostam Aziz, Andrew Chenge, Nazir Karamagi, Yusuf Makamba, Peter Serukamba, Makongoro Mahanga, na wengine wanastahili kwenda jela si IKULU.

Hapo kweny red ndipo ulipochemsha. Kama sio vita ya uwaziri mkuu 2005 tusingeyajua yote ya RICHMOND. Huyo mwingine kitendo cha kuchukua Prime Properties za Serikali na kuziweka mikononi mwa m watu binafsi kinyume cha ibara 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni doa kubwa sana. hao wote ni MAFISADI TU.
 
aliye msafi zaidi ya huyu mwanamke malaya na awe wa kwanza kumrushia jiwe......., tumewasikia ccm,cdm na cuf, tumewasoma raia mwema, rai, mwanahalisi na dira ya mtanzania... Mwenye macho haambiwi tazama ila wahenga husema "subira huvuta heri" huo ndio msimamo wangu.

mie ni shabiki wa liverpool na hivi majuzimajuzi mzee wetu daglish ameyatamka haya" no one individual is bigger than this club(country). There never has been and never will be" liverpool boss-kenny daglish

siyo wanaohimiza kujivua magamba, siyo wanaoitwa mafisadi, siyo ccm, siyo cdm/cuf na siyo media industry yetu iliyo juu zaidi ya tanzania na watu wake. Always tanzania will be higher and higher zaidi yetu sote licha mabavu, pesa na ushawishi tulionano.
tuwe na subira time will tell.
mungu ibariki tanzania
 
Hapo kweny red ndipo ulipochemsha. Kama sio vita ya uwaziri mkuu 2005 tusingeyajua yote ya RICHMOND. Huyo mwingine kitendo cha kuchukua Prime Properties za Serikali na kuziweka mikononi mwa m watu binafsi kinyume cha ibara 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni doa kubwa sana. hao wote ni MAFISADI TU.

Usitake kupotosha watu hapa. Hakukuwa na vita vya uwaziri mkuu 2005 na hakuna aliyekuwa anautaka zaidi ya huyo Lowassa mwenyewe. Huyu jamaa hana hata uwezo wa kufanya hata mahojiano na waandishi wa habari ili kupima hata uwezo wake wa kuelewa issues za kitaifa na kimataifa. Lakini suala muhimu la kujiuliza ni: Je, kweli nchi hii haina watu wa maana wa kuongoza zaidi ya huyu bwana mwenye elimu ya kucheza ngoma na maigizo? Yeye aendelee na kile alichokichagua, kuwaibia watanzania lakini URAIS ASAHAU NA WAPAMBE WAKE WATAFUTE NAMNA NYINGINE YA KUMSUJUDIA!
 
Ni kweli LOWASA ni tishio ila si ktk kujenga , yeye ni tishio ktk KUBOMOA!!!!!!!!!!!!. Amechangia kwa hali na mali kukibomoa CHAMA (CCM),,.:redfaces:
 
Back
Top Bottom