Lowassa ni msafi, Lakini kuna kitu hiki...

Lowassa ni msafi, Lakini kuna kitu hiki...

Invisible, is this an evidence that Lowassa is Fisadi? Nikienda Brela nitapata majina yenu wote mnaomiliki JF, does it make you Fisadi kwa kumiliki JF. Jibu ni hapana.

Ningefarijika sana kama tungeenda kwenye sheria za nchi na kujiuliza Barare wanalipa kodi? je wameajiri watanzania wangapi? mtaji wa kuanzisha kampuni ulitoka wapi? Kisha tuweke ushahidi unaoonyesha kuwa mtaji ulipatikana kwa wizi, udanganyifu au njia isiyo halali.

Hivi nikiwa na hela zangu siruhusiwi kuziwekeza? mbona Ndesamburo anamiliki Hotel Uingereza, amefisadi wapi? We should be objective my dear brothers. Hizi fikira za kuona mtu mwenye pesa ni fisadi ni fikira mufilisi kabisa.

Tukio
Miezi miwili iliyopita, maeneo ya kawe bwana mmoja akiwa kwenye Land Cruiser 105 anaelekea mjini, daldala likampiga pasi, liliposimama akashuka kwenda kumuuliza dereva kwanini kafanya hivyo. Kwa kuwa Dereva ni jeuri akaanza kumtukana na kumwambia fisadi, katikati ya malumbano abiria wakapokea fisadi, fisadi maraumati ukaanza kujaa bila hata kuuliza kuna nini wote wakaanza kuimba fisadi. Yule bwana kuona hali inakuwa tofauti akarudi kwenye gari yake akaondoka. kila mwenye kitu tofauti anaitwa fisadi hata kama ni mkopo kutoka benki hakuna anayeona zaidi ya kujenga chuki ya ufisadi.

My Take
450Ml ni pesa ambazo leo hii ukienda saccos unaweza kukopeshwa, siyo lazima uwe umeiba ndiyo uwe na 450ml.
 
Invisible, is this an evidence that Lowassa is Fisadi? Nikienda Brela nitapata majina yenu wote mnaomiliki JF, does it make you Fisadi kwa kumiliki JF. Jibu ni hapana.

Ningefarijika sana kama tungeenda kwenye sheria za nchi na kujiuliza Barare wanalipa kodi? je wameajiri watanzania wangapi? mtaji wa kuanzisha kampuni ulitoka wapi? Kisha tuweke ushahidi unaoonyesha kuwa mtaji ulipatikana kwa wizi, udanganyifu au njia isiyo halali......
Sijui ni aina gani ya ufunuo na hekima ulizonazo kama umeshindwa kutambua hata hili lililo wazi kabisa. Nyaraka za Brela zimewekwa hapa kama kielelezo cha kuthibitisha kwamba EL ni mmiliki wa kampuni ya Barare na kwamba uhamishaji wa fedha umefanywa na familia ya EL. Sasa je, ni biashara gani anayofanya inayoweza kumpa turnover ya 8 bilion
Kwa mwezi kama si biashara haramu na mavuno ya matumizi yake ya madaraka?

Pata ufunuo huu ukusaidie!
 
Unajuaje labda huyu ni mzee wa Hekima na Ufunuo kutoka katika yale makanisa anayotumia kujisafisha!!

Uwezi jua bana!!
 
Jamani Jamani tumwogope Mungu Hata Ukiwa Waziri kwa Miaka 5 Huwezi kuwa na mtaji wa 8Billions. lazima ziwe zimetoka mikono ovu!
 
Hekima Ufunuo Pound Sterling 475,000.00 ni sawa na Tsh 450Million? hebu kapitie upya exchange rate ya P0UND STERLING against Tanzanian shilling! Huyo aliyeitwa Fisadi ni reflection ya GAP kubwa kati ya walionacho na wasio nacho!!
 
Last edited by a moderator:
Hili suala la Gap kati ya walionacho na wasionacho is mis-leading na inatumiwa na wanasiasa zaidi kwa sababu obvious wafanyabiashara lazima weweze ku-control fedha nyingi. Pamoja na kwamba hizo fedha wanazimiliki wao, ni vizuri kujua kwamba hizo fedha ni kwa ajili ya biashara zao!

Tabia iliyojengeka kwa wa-TZ kuona matajiri kama watu wasiotakiwa itakula kwetu kwa sababu tunaishia kuchukia wajasiriamali na hivyo kutokuwa-probusiness katika mitazamo yetu mingi; ki-sera na vinginevyo.

tunahitaji kubadilika! Tunahitaji kujua kwamba wengine ni lazima wawe na fedha nyingi ili kwa sababu wana mawazo ya kuzipata hizo fedha nyingi, mawazo ambayo pia yanaeweza kutusaidia wengine wakapata ujira wao, kazi n.k. Na hapo utofauti wetu pia huonekana. Hao wanaita wenzao mafisadi bila hata kujua kama kweli ndivyo hivyo, wengi wao wana tatizo la kutokujua au wanaamini yanayosemwa na vyombo vya habari na maneno ya mitaani.

Ufisadi nao pia upo, ni kweli. Lakini pia ufisadi unaweza kuwa na faida kama matokeo yake yakawa ni kuongezeka kwa ujasiriamali, siyo kupeleka fedha kuweka benki huko ughaibuni n.k. ...

.....
 
Hata CCM wajifarague namna gani sijamuona mchapakazi kama Lowassa. Tena walikuwa na bahati wakaichezea. Kwa vile Rais wao alikuwa dhaifu, kuwepo kwa Lowassa kungeziba pengo hilo na ombwe la uongozi lililopo lisingeonekana sana. Kosa la pili, lilikuwa kumteua Pinda Waziri Mkuu ambaye alikuwa chini ya Lowassa. Kibinadamu kila Pinda anapotaka ajitahidi huona kivuli cha Lowasa kiutendaji. Yaani Pinda anamuona Lowassa kama boss wake, milele na huo ndo ukweli.
Hebu hao mabingwa wa kupambana na ufisadi watwambie, hivi serikali ilipata hasara gani katika suala la Richmond? Si ni Lowassa huyuhuyu ndiye alipambana na Citywater hadi wakang'oka na hata kesi waliyofungua tukashinda.
Iweje iweje, ipo siku umma utakubali kuwa CCM waliteleza na hadi sasa hakuna mchapa kazi na anaekubalika kama Lowassa ndani ya CCM, nani? Mtaje. Lakini kosa la CCM wamempaka matope sana kiasi cha kwamba amechafuliwa mno, huenda inaweza kuwa vigumu kumsafisha na kumtengeneza kama Rais mtarajiwa tukizingatia nguvu za upinzani.
Ukweli CCM mliteleza, na mtajuta!
 
Tehe tehe tehe, yetu macho bana. Jambo la msingi nchi hii kwa sasa haina msafi hata mwanafunzi akitoka chuo na kupata kazi anawaza kupiga dili na kuingiza fedha fasta, iwapo atakwama atatafuta pori jingine la kuvuna. Ila kasi ya vigogo kwenda kisutu inatupa somo.
 
Dili anaaza kupiga akiwa mwana-chuo angalia watu wanavyo jaza fomu za mikopo....serikali inamlipia na wazazi wake wana mlipia.
 
Huyu hafai na wala asiogopwe wala kutegemea kwani kambi aliyoipanga imsaidie imeshavurugwa (Halmashauri Kuu, Wakuu wa wilaya na Mikoa hawapo) ndio wangempigia kura za uteuzi
 
You don't need Hosea's boys to prove this dude is guilty of corruption...I think things have gone too far, Lowassa should join Mramba and others in court...

Good job invisible!
ni nani atakaye mfunga paka kengele? Lowassa ana nguvu, na ameiweka serikali yote mfukoni mwake.
Juzijuzi huyo mwanawe alimgonga kwa makusudi trafiki, na mtoto huyo akaondoka Oysterbay polisi huku akipigiwa salute
 
Hata mimi hii subjectivity ya watz inanipa hofu sana. Matajiri wenye makampuni makubwa tu na wamewekeza hadi nje ya nchi, tunaambiwa WAFANYABIASHARA. Wengine wakifanya hivyo wanaitwa MAFISADI. Tuache ushabiki na uvivu wa kufikiri
 
Lowasa ni fisadi na mwizi full stop. Ana pesa zetu nyingi sana huko Uswisi. Urafiki wake na RA ulikuwa ni wa kuiibia tu hii nchi. Huyu mzee wa majenereta ni balaa, hafai hata kidogo.
 
Naamini watu mtaweza kukipakua na kutoa maoni yenu...

Kumbuka: Nyaraka hizi ni za SIRI KUBWA

...NYARAKA ZA SIRI ZINGEWEKWA HAPA
icon10.png
icon12.png
icon12.png
 
Lowasa ni fisadi na mwizi full stop. Ana pesa zetu nyingi sana huko Uswisi. Urafiki wake na RA ulikuwa ni wa kuiibia tu hii nchi. Huyu mzee wa majenereta ni balaa, hafai hata kidogo.

Haya majibu mepesi mno kwa hoja nzito kama hii
 
Back
Top Bottom